James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,206
- 1,509
Mimi kama Mtanzania nipendaye lugha yangu ya Kiswahili nasikitika sana kuona lugha hii ikiharibika. Chakusikitisha zaidi ni kwamba hakuna kiongozi yeyote wa juu kuanzia Rais, waziri wa utamaduni n.k. anayefanya jitihada madhubuti ya kukienzi Kiswahili.
Kwenye hotuba yake ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa nimemsikia rais Samia akisema kwamba kuna fedha imetengwa ili kukuza lugha ya Kiswahili. Alitaja fedha hiyo itatumika kama kuchapisha nakala za Kiswashili kwenye jumuiya ta SADC. Lakini kutoa pesa ya kuchapisha nakala za Kiswahili ni kazi bure kama sisi wenyewe hatuongei Kiswashili fasaha.
Mimi binafsi nafikiri Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuharibu lugha ya Kiswahili. Siku hizi kumeibuka wimbi la maneno ya kijinga kabisa kwenye lugha yetu, kwa mfano,
mdada - dada
mboga mboga - mboga
fasta fasta - haraka
Haya ni baadhi ya maneno ambayo mimi binafsi nayachukia kabisa.
Hatuna haki miliki lakini mimi nasema Kiswahili ni mali yetu! Ni lugha yetu ya taifa na Watanzania tunakitumia Kiswahili kuliko nchi yeyote duniani. Faida za Kiswahili ni kama kuunganisha watu, kuwafanya wanamuziki wetu kuuza nyimbo zao nje ya Tanzania na mwisho Kiswahili kinalinda heshima ya Tanzania kwasababu ni lugha yetu.
Moja ya hatua ninayopendekeza ni kwa vyombo husika kuvipiga faini vituo vya utangazaji na magazeti pale wanaposhindwa kutumia Kiswahili fasaha.
Watu wa nje wanafikiri eti Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuongea Kiswahili fasaha, lakini hawajui kuwa Tanzania pia ndio nchi inayoongoza kwa kuharibu lugha ya Kiswahili!