Rais Samia: Kama haumpendi Rais aliyeko, penda nchi yako

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
1642074880114.png

Rais Samia Suluhu Hassan amesema urais sio mtu ni taasisi lakini kikatiba kunakuwa na mtu pale juu. Amewaambia Mawaziri kuwa kama hawampendi Rais aliyepo basi wapende nchi yao

Amesema hata kama haumpendi Rais Samia isiwe kigezo cha kupuuza mambo yote ambayo serikali inafanya. Ameruhusu watu kumchukia lakini sio kuchukia mambo ya serikali

Amewataka kuheshimu viapo vyao kwa kuwa wameapa kwa kushika vitabu vya Imani zao
 
Mimi siwezi kumchukia mtu ila nachukia matendo yake ya ubaguzi
Alisema anawafukuza kazi mawaziri wanaotaka urais wakajiandae na urais ila yule anaekesha akiwavurigia wenzao ili akalie kiti ameachwa wameonewa mawaziri wasiohusika
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema urais sio mtu ni taasisi lakini kikatiba kunakuwa na mtu pale juu. Amewaambia Mawaziri kuwa kama hawampendi Rais aliyepo basi wapende nchi yao...
Watu wanamchukia yeye kwasababu ya mambo ya serikali.

Watu wakipenda mambo ya serikali, “automatically” wanampenda na yeye. Wakumchukia hawawezi kukosekana. Lakini hawatakuwa wengi kama mambo ya serikali yanapendwa.

Hapa rais anaweza kuwa anazungumza kwa “codes” kwamba kuna watu wanamchukia yeye binafsi kwasababu ambazo hazihusiani na mwenendo wa serikali anayoiongoza. Sikubaliani naye. Maana ni yale yale ya kutumia “gender card” pamoja na uzanzibari.

Hata kigezo cha rais kutaka ama kuomba kuchaguliwa tena, kinapimwa na jinsi ambavyo serikali imefanya mambo yanayowagusa wananchi.
 
Mmmmmmh, yangu macho ila ninacho umia ni hii buku bubu ya umeme ya kila mwezi, miamala ya simu,

mbole kupanda bei mara dufu hii ndo mbaya zaidi kwa sisi watu wa Inshamba
 
Back
Top Bottom