PostGE2025 Rais Samia: JWTZ ijiepushe na mashinikizo ya kisiasa

PostGE2025 Rais Samia: JWTZ ijiepushe na mashinikizo ya kisiasa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
505
Reaction score
887
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuepuka mashikizo ya kisisa akieleza kuwa kuwa mshikamano kati ya uongozi wa kisiasa na uongozi wa kijeshi ni nguzo muhimu ya usalama wa Taifa, hata hivyo amesisitiza kuwa JWTZ ni jeshi la wananchi na linapaswa kubaki huru na siasa za vyama, likiwa na utii kwa Serikali halali iliyopo madarakani.

Rais Samia ameyasema hayo akizungumza na Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi na Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kabla ya kufungua mkutano wa 9 wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Makamanda uliofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) mkoani Tanga tarehe 15 Desemba 2025.





Samia jeshi.jpg


Samia jeshi 1.jpg
 
JWTZ jeshi la CCM toka enzi za mwalimu.

Zidumu fikra za mwenyekiti zidumu.

Yule mzee jinga sana aliharibu nchi kila mahali kisa kuipenda kwake CCM sasa hivi nchi imevuja kila mahali kwa mamifumo mabovu aliyoyasuka na kuyaishi yeye.
 
Huyu mwanamke ni mnafiki sana,ajabu wanaume wazima na ndevu zao wamekaa hapo wanamsikiliza.
Hawa wanaojiita wanaume wamekaa wanamsikiliza mwanamke aliyejivika nguo za jeshi huku hajui hata kuinua bunduki akiwahutubia kuacha kuwasikiliza wananchi, wakati yeye anawaua ni jambo linaloshangaza sana!! Hawa wanajeshi ndio kimbilio la mwisho la wananchi wasio na silaha pale wanaposhambuliwa na kuuwawa na makundi ya wahuni!!
Inashangaza sana kuona JWTZ wanakaa kimya wakati mtoto wa rais [ Abdul] anaunda jeshi lake la wahuni [GOONS] ndani ya nchi linaloua wananchi wasio na hatia lakini jeshi hilo hilo linalojiita la wanannchi linakaa kimya bila kumuadabisha huyu Abdul simply because mama yake ni Rais!
Ni jukumu la JWTZ kuhakikisha kuwa watu binafsi hawaundi majeshi yao humu nchini ama sivyo kazi yao itakuja kuwa ngumu sana huko mbele.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuepuka mashikizo ya kisisa akieleza kuwa kuwa mshikamano kati ya uongozi wa kisiasa na uongozi wa kijeshi ni nguzo muhimu ya usalama wa Taifa, hata hivyo amesisitiza kuwa JWTZ ni jeshi la wananchi na linapaswa kubaki huru na siasa za vyama, likiwa na utii kwa Serikali HALALI iliyopo madarakani.

Rais Samia ameyasema hayo akizungumza na Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi na Makamanda wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kabla ya kufungua mkutano wa 9 wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Makamanda uliofanyika katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA) mkoani Tanga tarehe 15 Desemba 2025.

Zingatia neno "HALALI"
 
Back
Top Bottom