Rais Samia, hii kauli ya kuwaruhusu Mawaziri wajipimie, wasivimbiwe itolee ufafanuzi tena

Kama alilenga kutoa onyo basi sidhani kama ilitoka moyoni. nilioona mimi Rais anajua kabisa mawaziri na manaibu ni wapigaji, sasa anachowaambia wasipige sana, na yeye hana shida na hilo kama watapiga ila wasizidishe na kuvimbiwa. Maneno ambayo naona kama Rais wetu mpendwa alikosea kuyatamka.
Amekosea vipi kuyatamka wakati kwenye ile hotuba amesema kuwa ile ni mara ya pili anasema maneno yale?
 
Je unadhani Watanzania wote ni la Saba C???
Miaka 60 hakuna maji wala umeme, huduma za afya ni kwa msaada wa wafadhili, barabara tumejengewa kwa msaada au mikopo, niliwahi sikia hata nyumba kuu pale Dom ni kwa msaada wa mchina.
Hata uwe na proposal nzuri kiasi gani au hata aje nayo mmarekani; bila ya 10% hakuna kigogo anayetia sahihi.
Kuna mtu aliwahi sema kuwa CCM ni sawa na ukoo wa panya.
Mama ametukumbusha ukweli kuwa ukiona mradi unasusua jua w
akubwa wajipimia zote.
Kwa hili hata mimi ni shahidi, nimetuma proposal kibao, maoni mpaka nimekatatamaa...Hakuna mwenye kujali raia kila mtu anatengeneza fellowship yake ya kumaliza matatizo yake binafsi, nchi ni second to personal interets....Acha ni nukuu neno la Mungu kwa wale ambao wanakaribia kukata tamaa kama mimi.

Methali 28:1-25 BHN​


Mungu hajawahi kudhihakiwa, si kiziwi hata asisikie na wala si kipofu hata asiweze kuona machozi ya wanyonge ambao wameachwa kama yatima
 
Rais Samia, jana akiongea na mawaziri aliwaambia wajipimie ila wasivimbiwe tena mbele ya TV ya umma. Nilipigwa na butwaa ila nikahisi mambo yafuatayo.

1. Rais hajui kwamba mali anazowaambia mawaziri wajipimie ni za wananchi wanao msikiliza na kwamba wananchi wanataka alinde mali zetu kama kiapo kinavyomtaka?

2. Rais anajua hawezi shitakiwa hata kama atafanya lolote; hivyo kalewa madaraka.

Ushauri kwa rais; Hii kauli itolee ufafanuzi, huku mtaani kishanuka mno.

Hata hivyo mawaziri wapiga deal wanajulikana.

VEDIO HII HAPA
Samia ni jipu kuuuuubwa ambalo lisipotumbuliwa mapema, litakuja kutuletea maafa makubwa sana hapa Wilayani Kivu ya Mashariki.
 
Yes...Let me prophesy:
Rest in the LORD , and wait patiently for him: Fret not thyself because of him who prospereth in his way, because of the man who bringeth wicked devices to pass. For evildoers shall be cut off: But those that wait upon the LORD , they shall inherit the earth. For yet a little while, and the wicked shall not be: Yea, thou shalt diligently consider his place, and it shall not be. But the meek shall inherit the earth; And shall delight themselves in the abundance of peace.
Psalm 37:7‭, ‬9‭-‬11 KJV
 
Serikali inaongozwa na MWANADAMU na si MUNGU......


Mwanadamu huyo anawakumbusha WATENDAJI KUSIMAMIA VIAPO VYAO vifuatavyo........

1)Kutoingiliana katika majukumu ya mipaka ya kazi zao....kazi yoyote ina maslahi binafsi na Yale makuu zaidi(kutoa huduma kwa jamii)

2)Kutochafuana ,kubagazana na kufitiniana kwa kiongozi mkuu(kwenda kusema kwa mama)

Mh.SSH amefafanua vyema tu ila baadhi yetu tumeamua kufanya UPOTOSHAJI WA MAKUSUDI.....

#Siempre JMT🙏
Upuuzi wakiwango cha Utopolo
Kawadanganye Wajinga sio Sie
Tanzania Ilisha patwa
 
Wana polisi, wana jeshi, usalama wa taifa. Huwezi kuiondoa CCM kwa kura za uchaguzi. Ingekuwa kura zinaondoa CCM ingekuwa chama pinzani miaka mingi
 

Attachments

  • 20210191812.mp4
    980.3 KB
Rais Samia, jana akiongea na mawaziri aliwaambia wajipimie ila wasivimbiwe tena mbele ya TV ya umma. Nilipigwa na butwaa ila nikahisi mambo yafuatayo.

1. Rais hajui kwamba mali anazowaambia mawaziri wajipimie ni za wananchi wanao msikiliza na kwamba wananchi wanataka alinde mali zetu kama kiapo kinavyomtaka?

2. Rais anajua hawezi shitakiwa hata kama atafanya lolote; hivyo kalewa madaraka.

Ushauri kwa rais; Hii kauli itolee ufafanuzi, huku mtaani kishanuka mno.

Hata hivyo mawaziri wapiga deal wanajulikana.

VEDIO HII HAPA
Kumtetea Rais Samia ni kazi sana...
Em ngoja tuone mwisho wake.

Damn this country.
 
Mods wameondoa ile video ya mpendwa wetu rais SSH akihimiza tujisevie kadri ya urefu wa kamba zetu aniwekee hapa!
 
mimi naona ana struggle for acceptance kutaka kumplease kila mtu ndio matokeo yake hayo unaongea utumbo
Mkuu upo sahihi asilimia mia moja.Anauza nchi in expense ya yeye kutokujiamini katika uongozi wake.

Siyo tu kwamba anaongea utumbo bali utumbo alioongea unaenda kutekelezwa na waliopo chini yake kwa speed ya mwanga.
16402654753460.jpg
 
Hapa kuna mawili....

1. Huenda Mama anaongea kauli tata kwa kumaanisha hivyo hastahili samehewa kwa vile anakijua kiswahili fasaha vizuri.
2. Mama ni mzanzibari na kama tunavyowajua wazanzibar wanafunguka mno ktk lugha, yaani wako 'too explicit'. Huku bara huenda tusiwaelewe ila kule visiwani ni Kiswahili mujaarab. Na huenda mpaka sasa wanatushangaa sana.

MY BASIC ARGUMENT...

Tujitahidi kumzoea Mama. Tunaweza mjaji vibaya kumbe waaalaa mtoto wa kiUnguja ana nia njema kabisa.

'kujipimia' huenda kwa maadili ya ki ISLAM ni norm..accepted.

Thread posted.
 
Back
Top Bottom