Rais Samia, hii kauli ya kuwaruhusu Mawaziri wajipimie, wasivimbiwe itolee ufafanuzi tena

Kula kwa urefu wa kamba.
 

Attachments

  • VID-20220204-WA0003.mp4
    8.1 MB
What if hao wakurugenzi walikula hadi wakavimbiwa?Kwa sababu msimamo wa Samia ni watu watafune ila mradi wasivimbiwe.Labda wakurugenzi walivimbiwa.
Msimamo wake ungekuwa ni kuruhusu rushwa kama unavyotaka ionekane asingewafukuza kazi, angeruhusu rushwa iendelee. Hili suala ni dogo sana ni la uelewa tu.
 
Kama ninavyotaka?Yaani Samia adai watu wake wajipimie halafu unadai kwamba mimi ndiye nataka Samia aruhusu rushwa?!Samia amesharuhusu rushwa halafu unadai kwruamba mimi ndiye nataka aruhusu rushwa?!
Angekuwa karuhusu rushwa hao wakurugenzi wanne wasingefukuzwa kazi mkuu.
 
Nimeshakuambia kuwa wakurugenzi wanne walivimbiwa ila nashangaa bado unarudia kitu hichohicho.
Unao ushahidi wa kuvimbiwa kwao au ni story za kujifurahisha? , kumbuka rais ni mamlaka ya juu kupita zote nchini anazo taarifa zote zenye kuwahusu wakurugenzi na taasisi nyinginezo za kiserikali.
 
Ushahidi ni kauli ya Rais aliyosema kuwa hataki watendaji wake wavimbiwe bali wajipimie,kwa hiyo kama kuna aliowatumbua maana yake ni kwamba wameenda kinyume na kauli hiyo kwa kuvimbiwa kwa sababu kama wangejipimia maana yake kwa maelezo ya Rais wangekuwa salama.
Kauli ya rais na uelewa wako ni vitu viwili tofauti kabisa.
 
Hakuna Rais duniani ambae anapaswa kuongea kwa mafumbo.Marais wanapaswa kuongea moja kwa moja bila mafumbo ili kila mtu hadi watoto wadogo na watu ambao hawajaenda shule waelewe kauli ya Rais na ndicho alichofanya Samia.
Huyu ni mpaka 2025 kwa hapa TZ Mungu akipenda. Tafuta rais wa kwako kutoka akilini mwako ndio umpangie namna ya kuongoza nchi ya kufikirika.
 
Ushahidi ni kauli ya Rais aliyosema kuwa hataki watendaji wake wavimbiwe bali wajipimie,kwa hiyo kama kuna aliowatumbua maana yake ni kwamba wameenda kinyume na kauli hiyo kwa kuvimbiwa kwa sababu kama wangejipimia maana yake kwa maelezo ya Rais wangekuwa salama.
Na pia hao wakurugenzi wanne walipiga jumla jumla bila hata kupeleka mgao kwa mama. Ndio maana kawatumbua. Yaani walikula, wakala hadi kuvimbiwa na kile ambacho kilitakiwa kimrudie mama nacho wakakipiga. Hatari sana
 
Back
Top Bottom