Polepole: Nilitegemea kuona kuna Mawaziri watajitokeza na kulaani ile kauli ya kula kwa urefu wa kamba

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
20220130_040726.jpg

"Wapo watu wanakula urefu wa Kamba na wanavimbiwa, hivi hawa watu wana uhalali wa kutuambia sisi tuishi maisha ya uadilifu? na mimi nitakuwa nauliza na wewe unakula kwa urefu wa kamba? kama ndio basi usiongee na mimi". Polepole

"Mimi nilitegemea kuona kuna Mawaziri watajitokeza na kulaani ile kauli ya kula kwa urefu wa kamba kwamba kuna wenzetu wanakula kwa urefu wa kamba na kauli hii haikubaliki, mimi nilidhani watu watatoka, lakini wapi ni kwa sababu ni wanafiki" Polepole

Pia, soma: Thread 'Rais Samia: Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, lakini mbona mnakula sana mnavimbiwa? Si kweli kama hampati kwenye maeneo yenu. Jipimieni...' Rais Samia: Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, lakini mbona mnakula sana mnavimbiwa? Si kweli kama hampati kwenye maeneo yenu. Jipimieni...
 
Tatizo la politicians wetu they always get their voice back wanapokua nje ya system why?

Mr. Polepole kipindi chako wakati kamba yako haijakatika hukuyasema haya kwa UHURU; kupotea kwa Saanane, kupigwa risasi na kuuliwa kwa Akwilina, kuvunjwa kwa haki za binadamu, kubinywa kwa demokrasi nchini etc etc; hukusimama na kunyosha kidole kuyasemea ika sasa upo nje ya system unaongea.

Huu ni unafiki
 
Angekuwa kiongozi ni bwana yule aliyeenda ndy amezungumza hayo maneno, hakuna Shaka kuwa yeye na mawaziri wa enzi zake wasingeongea chochote, wangekaa kimya km hao anaowashutumu wamekaa kimya sasa hivi

CCM ikibadilisha viongozi tu na wanafiki wanabadilika majina, ila unafiki uko palepale
 
Tatizo la politicians wetu they always get their voice back wanapokua nje ya system why?Mr. Polepole kipindi chako wakati kamba yako haijakatika hukuyasema haya kwa UHURU;kupotea kwa Saanane,kupigwa risasi na kuuliwa kwa Akwilina,kuvunjwa kwa haki za binadamu,kubinywa kwa demokrasi nchini etc etc ;hukusimama na kunyosha kidole kuyasemea ika sasa upo nje ya system unaongea....huu ni unafiki
Mbona chadema waliwahi kumshambulia Lowassa ni fisadi na pia wakasema wanaushahidi na ufisadi wake lakini hao hao wakampokea kwenye chama chao na wakamkabidhi kuwa mgombea wa Uraisi pamoja na unafiki Huu walionyesha lakini bado wengine wanawaamini wanapotoa hoja zao inakuaje kwa Mhe PolePole iwe nongwa?
 
Mbona chadema waliwahi kumshambulia Lowassa ni fisadi na pia wakasema wanaushahidi na ufisadi wake lakini hao hao wakampokea kwenye chama chao na wakamkabidhi kuwa mgombea wa Uraisi pamoja na unafiki Huu walionyesha lakini bado wengine wanawaamini wanapotoa hoja zao inakuaje kwa Mhe PolePole iwe nongwa?
Acheni rais apingwe akifanya makosa, ataruhusuje mawaziri wafanye ufisadi eti sababu ni wakati wao halafu chadema wafurahi na kumbeza polepole kisa katoka hadharani na kulaani ile ruhusa? Chadema msipende kupinga Kila kitu kisa Polepole ni CCM.
 
Angekuwa kiongozi ni bwana Yule aliyeenda ndy amezungumza hayo maneno,hakuna Shaka kuwa yeye na mawaziri wa enzi zake wasingeongea chochote..wangekaa kimya km hao anaowashutumu wamekaa kimya sasa hivi

CCM ikibadilisha viongozi tu na wanafiki wanabadilika majina,ila unafiki uko palepale
Magufuli hawezi kuongea huo ujinga wa kula kwa urefu wa kamba! Waacheni wale kwa urefu wa kambana kufanya birthday!
 
Tatizo la politicians wetu they always get their voice back wanapokua nje ya system why? Mr. Polepole kipindi chako wakati kamba yako haijakatika hukuyasema haya kwa UHURU; kupotea kwa Saanane,kupigwa risasi na kuuliwa kwa Akwilina, kuvunjwa kwa haki za binadamu,kubinywa kwa demokrasi nchini etc etc; hukusimama na kunyosha kidole kuyasemea ika sasa upo nje ya system unaongea. Huu ni unafiki
Eti mawaziri wajitokeze kulaan, hivi unaweza kulaani mzazi wako?? huyu polepole kichwa chake hakiko sawa.
 
Back
Top Bottom