Rais Samia, hii kauli ya kuwaruhusu Mawaziri wajipimie, wasivimbiwe itolee ufafanuzi tena

Hapo Hagaya atasema video wame edit hakusema hayo maneno.
Siku hizi kwenye ofisi za serikali hata hospitalini na mahakama huduma imesharudi hali ya zamani hawajali mtu
 
Is This A Compromise Or What !!?? If So Such Behaviours Won't End.
 
Kuleni sana lakini msivimbiwe. Na kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake na muelewane, najua mnakula sana lakini kuleni taratibu.

Kweli mkuu kuna uzanzibari hapa ambao sisi wabongo hatujui kitu??

Hatarii sana aisee. Acha walio juu waendelee kuneemeka mpaka 2025 tuwape tena hadi 2030 na kuendelea na kuendelea
Mkuu umeandika kinyonge sana..😑😑
 
Maana yangu ni kuwa, kama Rais hayo maneno ya kuonyesha kuwa kupiga marufuku, na kuzuia upigaji sio kipau mbele kwake hakupaswa kuyatamka.
 
Mkisikia ^kula^ tu mnajua ni ufisadi? Najua fika kwamba utawala huu ni ponga katika suala la matumizi ya mali za umma na udhibiti wa pesa, kuliko ile ya JPM, lakini hapa Bi Mikopo anamaanisha matumizi ya mamlaka. Watendaji wake ""wasiingiliane na kugombana katika kutekeleza majukumu ya ^sirikali.^

Don't be so closed-minded. Anyweiz, politics inatendensi ya kukapitolaizi kwenye mambo tata na seemingly negative.
... huo ni mtazamo wako usilamishe kila mtu aelewe ulivyoelewa wewe! Rais alikuwa very clear, nanukuu,

" ... sio kwamba hampati; mnapata lakini jipimieni; jipimie! Kwa mfano kuna lile nililolisema la ujenzi wa meli; kuna kijiajenti huko pembeni kinalipwa milioni 2 dola kwa kila meli. Hiyo sio sawa, sio sawa! Sijui kuna ujenzi wa barabara, fedha itagawiwa kwanza weee barabara ikijengwa inakuwa compromised, viwango vinakuwa compromised ..."

... kwa nukuu hiyo unataka tusiwe "closed-minded" tuone kwamba hajazungumzia ufisadi. Hiyo USD 2 m Rais anayong'aka sio sawa kulipwa kwa "kijiajenti" ni hela ya mboga sio? Na hiyo ya fedha za barabara kugawiwa kwa kiwango cha ku-compromise ubora?

Rais alitakiwa akemee vitendo hivyo in strongest terms possible na sio kuviongelea kwa soft language - 'JIPIMIENI MSIVIMBIWE' maneno ambayo ameya-connect moja kwa moja na fedha za miradi tena kwa mifano. Kinyume chake wewe unataka tuamini alimaanisha "wasiingiliane na kugombana katika kutekeleza majukumu ya sirikali"; you must be joking.
 
Acha kujipa upofu na kujilazimisha kuwa mpumbavu.

Samia ametoa mifano mingi jinsi miradi inavyokuwa haikamiliki kutokana na ufisadi uliopitiliza(Kula hadi kuvimbiwa) na ametoa mifano ya miradi ya meli pamoja na barabara.Halafu unadai kuwa hazungumzii ufisadi?!

Unavyojilazimisha kuwa mpumbavu unapata faida gani?
View attachment 2081340
... watu wengine kwa kujitoa ufahamu hawaoni tatizo! Kauli ile inatakiwa iombewe msamaha na mhusika mwenyewe aliyeitoa; na sio wapambe kujifanya kuitolea "ufafanuzi".
 
... watu wengine kwa kujitoa ufahamu hawaoni tatizo! Kauli ile inatakiwa iombewe msamaha na mhusika mwenyewe aliyeitoa; na sio wapambe kujifanya kuitolea "ufafanuzi".
Mkuu ile kauli haiwezekani mhusika aiombee msamaha kwa sababu ukiangalia hii hotuba yake hapo mwanzoni kabisa anadai kuwa ni mara ya pili anatoa ule msimamo/kauli.Hii maana yake ni kwamba alichokisema ndiyo msimamo wa serikali yake.

Wewe kudai kuwa mhusika aombe msamaha kitu ambacho ni msimamo wa serikali yake unajaribu kupaka ufisadi mafuta kwa mgongo wa chupa kitu ambacho kinakufanya kuwa kama hawa jamaa ambao ni mazezeta.
 
Lilikuwa ni onyo la tabia za kifisadi zilizoshamiri tangu 2010 to 2020 ambazo hazijawahi kuachwa. 2015 to 2020 hazikuzungumzwa tu ila zilikuwepo za kibabe.

Hata hivyo ametoa onyo very weak, ukisha amua kuweka udhaifu wa mtendaji wazi ni umemshtaki kwa jamii basi unatakiwa umuwajibishe, kinyume na hapo muite faragha muonye. Sasa hapa tunajua kuwa kuna mawaziri walafi ila wanatakiwa wajipime wenyewe.

Tunahitaji mpango mkakati bora wa kudhibiti utendaji wa serikali.
Iko wazi waibe lakini wasizidishe!! Disgusting what a leader!!??
 
Rais Samia, jana akiongea na mawaziri aliwaambia wajipimie ila wasivimbiwe tena mbele ya TV ya umma. Nilipigwa na butwaa ila nikahisi mambo yafuatayo.

1. Rais hajui kwamba mali anazowaambia mawaziri wajipimie ni za wananchi wanao msikiliza na kwamba wananchi wanataka alinde mali zetu kama kiapo kinavyomtaka?

2. Rais anajua hawezi shitakiwa hata kama atafanya lolote; hivyo kalewa madaraka.

Ushauri kwa rais; Hii kauli itolee ufafanuzi, huku mtaani kishanuka mno.

Hata hivyo mawaziri wapiga deal wanajulikana.

VEDIO HII HAPA
Kama niliwahi kuonesha japo chembe ya imani kwa SSH; naomba nikiri nilikosa mimi na nilikosea sana. Naomba mnisamee!
Performance ya urais wa SSH utakuwa juu kidogo ya A.H Mwinyi na chini ya JM Kikwete!
Na hivi upinzani nao bado wanajitafuta;
Hakika,
Tumepigwa!
 
Hii kauli inauma sana.
Wajipimie kiasi gani?
100Mil.
600Mil.
1Bil.
100Bil.
200Bil.
..........?
Halafu mwenye kamba ndefu zaidi(Rais)
atakula sh.ngapi?.
Tunampenda sana Mheshimiwa Samia,Ila kwa kauli hii ni vyema akaomba msamaha.
 
Hii kauli inauma sana.
Wajipimie kiasi gani?
100Mil.
600Mil.
1Bil.
100Bil.
200Bil.
..........?
Halafu mwenye kamba ndefu zaidi(Rais)
atakula sh.ngapi?.
Tunampenda sana Mheshimiwa Samia,Ila kwa kauli hii ni vyema akaomba msamaha.
Hata akiomba msamaha ndo kaongea ya moyoni
 
Kula kwa urefu wa kamba yako, hapo unahitaji ufafanuzi upi. Akili za kuambiwa changanya na zako...Tunaongozwa na mfalme juha.
 
Rais Samia, jana akiongea na mawaziri aliwaambia wajipimie ila wasivimbiwe tena mbele ya TV ya umma. Nilipigwa na butwaa ila nikahisi mambo yafuatayo.

1. Rais hajui kwamba mali anazowaambia mawaziri wajipimie ni za wananchi wanao msikiliza na kwamba wananchi wanataka alinde mali zetu kama kiapo kinavyomtaka?

2. Rais anajua hawezi shitakiwa hata kama atafanya lolote; hivyo kalewa madaraka.

Ushauri kwa rais; Hii kauli itolee ufafanuzi, huku mtaani kishanuka mno.

Hata hivyo mawaziri wapiga deal wanajulikana.

VEDIO HII HAPA
History ina tabia ya kujirudia. Mzee Mwinyi alitoa RUKSA sasa SSH naye ametoa RUKSA. Nadhani hii itazua yafuatayo:-

1. Power struggle
Wengi wataanza kupambana hata kwa kuhonga kutafuta madaraka badala ya kudeliver. Utekelezaji wa ilani utazorota.

2. Security of property.
Wenye mashamba na viwanja wajipange kuhakikisha usalama wake. Uporaji wa mali za watu wasio na madaraka na ukwasi utashamiri. Mwenye nacho ataongezewa asiye nacho atanyang'anywa hata kile kidogo alicho nacho. Hati juu ya hati. Wawekezaji wanaochukuwa kwa kificho ardhi yenye ukubwa hata wa Wilaya nzima. Vita ya wakulima na wafugaji.

3. Institutional failure.
PCCB, Land Court/Judiciary, Police, Ethics Commission zitapotezewa nguvu zao na hiyo high profile decree (kula mle lkn msivimbiwe na msigombane bali kila mtu kwa urefu wa kamba yake)

4. Proliferation of Mega & Giga Corruption.
Public finances at major risk, thus donours demoralized.

5. Unajuwa mimi ni nani?


Naunga mkono mada ufafanuzi upya ufanyike maana huku mitaani tafsiri ziko nyingi na mzuka unapanda.

NB.
Nadhani kazi ya urais inawafaa sana watu wa bara (kanda ya ziwa) kuliko wa mwambao.
 
Acha kujipa upofu na kujilazimisha kuwa mpumbavu.

Samia ametoa mifano mingi jinsi miradi inavyokuwa haikamiliki kutokana na ufisadi uliopitiliza(Kula hadi kuvimbiwa) na ametoa mifano ya miradi ya meli pamoja na barabara.Halafu unadai kuwa hazungumzii ufisadi?!

Unavyojilazimisha kuwa mpumbavu unapata faida gani?
View attachment 2081340
Wamefukuzwa kazi wakurugenzi wanne wa halmashauri nne. Nadhani unaitafsiri vibaya maana ya hiyo video, au unafanya kisiasa zaidi ukiwa humpendi SSH.
 
Kauli iko clear kwamba watu wajipimie,wale kwa urefu wa kamba zao yaani wawe na kiasi.Ukizidi tuu urefu wa kamba yako tunakula kichwa na kizimbani unapandishwa.
 
Back
Top Bottom