Rais Samia awatumbua Mkuu wa Wilaya Morogoro Bakari Msulwa na Mkurugenzi Morogoro Sheilla Lukuba Kwa Mgambo Kuwapiga Wamachinga

Kwahio alingoja kuwatumbua leo wakati kosa lilifanyika lini ? (au alikuwa bado anafanya upelelezi kuhusu makosa na jibu alipata dakika chache kabla ya utumbuzi)?

Nilidhani hizi zama zimekwisha....
 
Rais Samia kawatumbua kwa kuwashambulia Machinga mtaani mkoani Morogoro.

Aliyetumbuliwa ni Bakari Msulwa Mkuu wa wa Wilaya ya Morogoro na Sheilla Lukuba Mkurugenzi Morogoro. NI kutokana na Mgambo kuwapiga Machinga.

Pia amesisitiza ajira zote zinazokuja za Ma-DC zijazo zitakuwa za vijana.

Anataka kutuletea akina Sabaya tena?
 
Namuombea paskali kwa mungu safari hii awe DC na mama atanifurahisha akimtumbua DC wa arusha maana hana tofauti na sabaya
 
Usilazimishe wafanane

1. Samia hateki watu
2. Samia hafokei watu
3. Samia anatambua Corona ipo
4. Samia anajipendekeza kwenye uhusiano wa kimataifa
5. Samia hapendi sifa za kupakwa mafuta kwa mgongo wa chuma (Ref: SABAYA)
6. Samia sio mshamba wa kujiona yeye ana akili kuliko watu wote eti kwa sababu tu ni Rais
7. Samia hana strategies za kuua upinzani


Usimfananishe kabisa na yule "MWANAKWENDAZAKE NA AENDE"
Umesahau mama yetu samia haui watu
 
Mwenyezi Mungu awape subira!

Labda kama kuwe na makosa au tuhuma nyingine mbali na hiyo kadhia ya machinga lakini kama sababu ni hiyo tu kwa kweli mmh !
 
Rais Samia kawatumbua kwa kuwashambulia Machinga mtaani mkoani Morogoro.

Aliyetumbuliwa ni Bakari Msulwa Mkuu wa wa Wilaya ya Morogoro na Sheilla Lukuba Mkurugenzi Morogoro. NI kutokana na Mgambo kuwapiga Machinga.

Pia amesisitiza ajira zote zinazokuja za Ma-DC zijazo zitakuwa za vijana.
View attachment 1819504


Busara ilitakiwa kutumika, hawa sio majambazi kama sabaya, kuwasikiliza kwanza, maybe they have a sensible defense. Mimi sio muumini wa huu upuuzi.
 
Sasa kuna sababu gani ya kutumbua mtu wakati unakaribia kufanya mabadiliko nchi nzima.
Sijui kama amejiridhisha bila shaka, kuwa viongozi hao, ndio waliwatuma mgambo kufanya hayo, ama unakuta ni viongozi walio chini yao tu waliamua 'kujimwambafy wenyewe' dizaini ya jamaa yetu wa Hai.... kaaazi kwelikweli. Na kweli kazi iendelee.
 
Back
Top Bottom