Rais Samia amtimua Hanafi Hassan Msabaha, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara kisa wananchi kurudisha Kadi za CCM

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,312
10,494
Hii nimeiona ITV habari. Mama kakasirika mkuu wa wilaya kufanya uzembe kwa wananchi kurudisha kadi za chama kisa Mtwara wengi ni upinzani.

My Take: Tuendelee kupambana!

=========

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kumuondoa kazini Hanafi Hassan Msabaha wakati akifunga mafunzo ya uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika Shule ya Uongozi Kibaha

Akieleza sababu zilizopelekea uamuzi huo Rais Samia amesema Mkuu huyo wa Wilaya amekuwa akipokea hongo na kuhamisha Miradi inapotakiwa kwenda na kuipelekea sehemu isiyohitajika, kitendo kilichofanya Wananchi kukerwa na kurudisha Kadi za Chama

Amesema hawezi kustahimili kuona Kadi za Chama zinarudishwa wakati Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wapo na walipoulizwa, Wakuu hao walijibu kuwa eneo hilo lina Wapinzani wengi

Zikiwa zimepita siku nne tangu baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Kijiji cha Lyowa Wilaya ya Mtwara warudishe kadi zao za chama kushinikiza Serikali kumaliza shule ya sekondari kijijini kwao, hatimaye Rais Samia Suluhu Hassan amesema atawafuta kazi Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa eneo hilo kwa kushindwa kusikiliza kero za wananchi.

Rais Samia ametangaza dhamira hiyo mkoani Pwani leo, Jumapili Agosti 27, 2023 alipohutubia hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa, yaliyofanyika katika Taasisi ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha mkoani humo. “Mkuu wa Wilaya anahongwa, mradi anaacha kwenda unakotakiwa anapeleka usipotakiwa, kiasi kwamba wananchi wanafika kurudisha kadi za chama, sisi huku tuna haja kubwa mmetuacha fedha mmepeleka kule na kadi zenu hizo. ALSO READ Rais Samia kuwafuta kazi DC, DED Mtwara

Kitaifa 30 min ago Rais Samia kuwafuta kazi DC, DED Mtwara

Kitaifa 30 min ago “Sina imani na Mkuu wa Wilaya anayesababisha kadi zirudishwe, Mtwara, Mkuu wa Wilaya yako sijui Hanafi (Msabaha) namtimua leo siwezi kustahimili kadi za chama zinarudishwa, nini Mkuu wa Wilaya yupo DED yupo yeye na DED wake,” amesema. Chanzo Wakati Rais Samia akiyasema hayo leo, Mwananchi Digital ilifika katika Kijiji cha Lyowo Jumatano Agosti 23, 2023 na kufanya mahojiano na wananchi hao kujua sababu za kurudisha kadi hizo.

Ally Mtambulwa mkazi wa kijiji hicho amesema wamerudisha kadi hizo kutokana na kutoridhishwa na maamuzi ya Serikali juu ya umaliziaji wa shule kijijini kwao huku akidai fedha zilizoletwa na Serikali kwaajili ya ujenzi wa shule ya kata zikipelekwa katika kijiji jirani kwa ajili ya ujenzi wa shule nyingine. “Hizi kadi tunazirudisha kwa Mkuu wa Mkoa, hatuko tayari kuona fedha zinakuja za shule lakini zinapelekwa kijiji kingine wakati sisi tumejenga kwa nguvu hatujapewa hata shilingi kumi kwanini tusisaidiwe?,”alihoji.

“Tumeshindwa na siasa kadi tunazo mfukoni tunazirudisha leo tena kwa Mkuu wa Mkoa, tumefunga ofisi ya mtendaji kwakuwa tuliishirikisha Serikali kwa kila hatua kwa nini ilituacha tumejenga sekondari madarasa matano, choo na ofisi ya walimu na walipopata fedha za ujenzi wakazipeleka kwingine ambako kuna madarasa mawili tu kwanini hawaji tukamalizia ujenzi wa shule hii?,” aliuliza Mtambulwa. Naye Asha Issa mkazi wa kijiji cha Lyowa amesema kuwa awali walianza ujenzi kwa kujitolea na walifikia hatua nzuri ambapo imebakia sehemu ndogo iweze kukamilika hivyo kuhitaji msaada wa serikali. “Sisi hatuna maneno mengi watoto wetu hawataenda shule wala kazi hazitafanyika tunahitaji mpaka tujue sekondari yetu inakalimikaje na kwanini sekondari ya kata isijengwe hapa?,”alihoji Asha.

Majibu ya Serikali Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Hassan Mmunda ambaye alisema ana siku tatu tangu wananchi wakatae kuongozwa nae huku akiiomba viongozi wa juu wafike kwa ajili ya usuluhishi wa jambo hilo. “Mimi nimetenguliwa siku tatu sasa (saba sasa) nawaomba viongozi wa Serikali waje tukae tuongee naona maendeleeo yamefanyika shule imejengwa lakini sasa shughuli za kiserikali zimesimama hii inaumiza hata watoto wetu wapo nyumbani hawaendi shule na ofisi zimefungwa,”alisema Mmunda

Mwananchi Jumatano Agosti 23, 2023 ilipomtafuta Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Hanafi Msabaha alisema Sh500 milioni walizopokea zitaenda kujenga shule mpya katika Kata ya Muungano na baada ya hapo wataimalizia ya Kijiji cha Lyowa. “Suala la shule kila sehemu walitaka shule ijengwe kwenye kijiji chao hivyo nikatumia busara ya kawaida baada ya kutembelea shule ya sekondari Lyowa ina eneo zuri kubwa limenyooka lakini tayari walikuwa na makubaliano waliyokaa katika vikao na kupitisha ujenzi wa shule ya kata katika kijiji cha Muungano,” alisema Msabaha.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema anamfuta kazi Mkuu wa Wilaya ya Mtwara vijijini, Hanafi Msabaha kutokana na kushindwa kusikiliza kero za wananchi hadi kupelekea wananchi hao kurudisha kadi za chama cha Mapinduzi (CCM).

Samia ameyasema hayo leo Jumapili Agosti 27, 2023 akifunga mafunzo ya uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika Shule ya Uongozi Kibaha, mkoani Pwani.

"Mnapopuuza kero zao sijui mtaenda kujibu nini kwa Mungu…..Mkuu wa Wilaya anahongwa, mradi unapelekwa usikotakiwa kiasi kwamba wananchi wanarudisha kadi za chama, Sina Imani na mkuu wa Wilaya anayesababisha kadi zirudishwe, Mkuu wa Wilaya Mtwara vijijini, namtimua Leo, siwezi kustahimili kadi zinarudishwa,”amesema Rais Samia.
 
Hii nimeiona ITV habari. Mama kakasirika mkuu wa wilaya kufanya uzembe kwa wananchi kurudisha kadi za chama kisa Mtwara wengi ni upinzani.

My Take: Tuendelee kupambana!

=========

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kumuondoa kazini Hanafi Hassan Msabaha wakati akifunga mafunzo ya uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika Shule ya Uongozi Kibaha

Akieleza sababu zilizopelekea uamuzi huo Rais Samia amesema Mkuu huyo wa Wilaya amekuwa akipokea hongo na kuhamisha Miradi inapotakiwa kwenda na kuipelekea sehemu isiyohitajika, kitendo kilichofanya Wananchi kukerwa na kurudisha Kadi za Chama

Amesema hawezi kustahimili kuona Kadi za Chama zinarudishwa wakati Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wapo na walipoulizwa, Wakuu hao walijibu kuwa eneo hilo lina Wapinzani wengi

View attachment 2730252
Kwahiyo kazi ya DED & DC ni kufanya kazi za chama na sio za serikali daaaa
 
Umewaza kama mimi. Au hajui kama kuna wanachama wameacha kushiriki mambo ya kichama kwasababu yake?
Huyu mama angekuwa anafanya haki angejifukuza mwenyewe....
Tangu aliposababisha spika kujiuzulu, tangu aliporudisha watendaji wabovu kwenye wizara (akina mwigulu, makamba na nnauye), tangu aliposaini makubaliano/mikataba yenye utata; kuna watu hawana imani kabisa.
Na huo ndio ukweli jamani wala sio chuki kama chawa wake wanavyotafsiri!
 
Amfukuze na yule waziri wa nishat ukiwa na sera nzuri ahadi za kweli utaongeza wanachama
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema anamfuta kazi Mkuu wa Wilaya ya Mtwara vijijini, Hanafi Msabaha kutokana na kushindwa kusikiliza kero za wananchi hadi kupelekea wananchi hao kurudisha kadi za chama cha Mapinduzi (CCM).

Samia ameyasema hayo leo Jumapili Agosti 27, 2023 akifunga mafunzo ya uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika Shule ya Uongozi Kibaha, mkoani Pwani.

"Mnapopuuza kero zao sijui mtaenda kujibu nini kwa Mungu…..Mkuu wa Wilaya anahongwa, mradi unapelekwa usikotakiwa kiasi kwamba wananchi wanarudisha kadi za chama, Sina Imani na mkuu wa Wilaya anayesababisha kadi zirudishwe, Mkuu wa Wilaya Mtwara vijijini, namtimua Leo, siwezi kustahimili kadi zinarudishwa,”amesema Rais Samia.

View: https://www.instagram.com/p/CwcbU1FN79K/

JE, YEYE ANASIKILIZA KWELI KERO ZA WATANZANIA? Amemwonea bure labda kama ana shida nyingine huyo aliyemfuta kazi.
 
kwan serikali imepatikanaje?rais anapataje watendaj wake cndo kupitia ccm?au nakosea?muhm katiba ibadilishwe
Hayo alitakiwa ayaongee ndani ya vikao vya chama.

Issue hapo angeongelea kutatua kero, kurudisha kadi au kuandikisha kadi ni KAZI ya kiongozi wa chama, hata mkuu wa wilaya au Mkoa hahusiki.

Tusichanganye mambo.
 
Mama hajui kua mtu anaweza akawa na kadi ya CCM,halafu akaipigia kura CHADEMA,halafu yule asiye na kadi,akaipigia kura CCM?
Ashauriwe vema,mama yetu.Pole mkuu wa wilaya,ukute ni zengwe tu umetengenezewa,na chawa wa mama,kwasababu kuna mambo hujawakubalia.
 
Hayo alitakiwa ayaongee ndani ya vikao vya chama.

Issue hapo angeongelea kutatua kero, kurudisha kadi au kuandikisha kadi ni KAZI ya kiongozi wa chama, hata mkuu wa wilaya au Mkoa hahusiki.

Tusichanganye mambo.
CCM ni Chama Dola usisahau hilo!
 
Hii nimeiona ITV habari. Mama kakasirika mkuu wa wilaya kufanya uzembe kwa wananchi kurudisha kadi za chama kisa Mtwara wengi ni upinzani.

My Take: Tuendelee kupambana!

=========

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kumuondoa kazini Hanafi Hassan Msabaha wakati akifunga mafunzo ya uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika Shule ya Uongozi Kibaha

Akieleza sababu zilizopelekea uamuzi huo Rais Samia amesema Mkuu huyo wa Wilaya amekuwa akipokea hongo na kuhamisha Miradi inapotakiwa kwenda na kuipelekea sehemu isiyohitajika, kitendo kilichofanya Wananchi kukerwa na kurudisha Kadi za Chama

Amesema hawezi kustahimili kuona Kadi za Chama zinarudishwa wakati Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wapo na walipoulizwa, Wakuu hao walijibu kuwa eneo hilo lina Wapinzani wengi

View attachment 2730252
Na bado
869bd07e67e29c35d24b6d4892fd3015.jpg
 
Kashindwa kusikiliza kero za wananchi basi na yeye aondoke kwakua hana analofanya kama rais. Kiufupi hana jipya
 
Back
Top Bottom