DOKEZO Wananchi wa Kondoa wamkataa Mkuu Wilaya, wamtuhumu kutumia polisi kuwapiga raia wakiwa uchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Wananchi wa kijiji cha Hurui, kata ya Kikore wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, wamelalamikia kitendo cha askari polisi wilayani humo, kuwakamata na kuwapiga wakiwa uchi wa mnyama usiku wa manane kwa amri ya mkuu wa wilaya hiyo, Dkt. Hamis Mkanachi, kwa madai kwamba wanashiriki kuchochea mgogoro wa ardhi kijijini hapo.

Aidha, hali hiyo imesababisha kijiji hicho kukosa uongozi baada ya viongozi kadhaa na vijana wengi kuyakimbia makazi yao na wengine kulala porini kuhofia kukamatwa na kubambikwa kesi mbalimbali kituo cha polisi wilayani humo.

Wakiongea kwa jazba katika mkutano wa hadhara wa kijiji hicho, wananchi hao wametishia kutoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mapema Oktoba mwaka huu, wakishinikiza Rais Samia Suluhu Hassan kumwondoa mkuu huyo wa wilaya baada ya kushoshwa na vitendo vya udhalilishaji.

Aidha, wamemtuhumu mkuu huyo wa wilaya kuamuru viongozi 10 wa serikali ya kijiji hicho kupiga magoti na waite mvua baada ya kufika eneo la mgogoro na viongozi hao, pia akiwa ameambatana na askari polisi alipoenda kutembelea eneo hilo na kutoa maamuzi ya kibabe kulikabidhi kwa wananchi watatu wa kijiji cha jirani kinyume na utaratibu na viongozi hao kuonesha kutoridhika na maamuzi yake.

Wakiongea kwenye mkutano huo, baadhi ya wananchi hao, Tembea Ama Senge, Maico Matei, na Joachim Manaha, walisema wananchi wa kijiji hicho wamejaa hofu kiasi kwamba vijana na viongozi wao wameyakimbia makazi yao kwa hofu ya kukamatwa na kumwomba Rais Samia kuingilia kati mgogoro huo huku wakitishia kutoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

Akiongelea kiini cha mgogoro huo, mjumbe wa serikali ya kijiji hicho ambaye alionja joto la DC la kupiga magoti, Fatuma Kinkuri, alisema eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 500 ni mali ya kijiji na walikabidhiwa na serikali tangu mwaka 1974 kama eneo la malisho, lakini baadhi ya viongozi wao mwaka 2009 walimega eneo lenye ukubwa wa ekari 54 na kuliuza kwa wananchi watatu wa kijiji jirani.

"Baadaye wananchi walibaini ardhi yao imeuzwa kinyamela, ndipo walipokuja juu na kuzuia ardhi yao isichukuliwe, na mwaka 2017 alikuja aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba na Mbunge wetu Ashantu Kijaji na kuamuru eneo hilo libaki kuwa mali ya wananchi kwa ajili ya malisho na sio vinginevyo."

Aidha, aliongeza kuwa watu watatu walionunua ardhi yao ambao ni Issa Kibaura, Omari Bashiri, na Iddy Lungu wamekuwa wakimtumia diwani wao ambaye amekuwa akimrubuni mkuu wa wilaya hiyo kuwagandamiza na kupuuza barua ya Mwigulu Nchemba aliyeamuru eneo hilo kibakie mikononi mwa wananchi wa kijijini hicho.

Akifungua mkutano huo, kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho, Abuu Hussein Gela, alisema kikao hicho kililenga kujadili mustakabari wa viongozi wao waliokimbia makazi yao na namna polisi wanavyovamia usiku wa manane bila hata kuwashirikisha watendaji wa serikali na kuvunja milango na kukamata wananchi kinyume cha sheria.

"Hivi sasa kuna wananchi wasiopungua kumi wamekamatwa usiku tena wakiwa uchi na kupigwa na miongoni mwao ni pamoja na mjumbe wa serikali ya kijiji, Mohamedi Bakari, na mwenyekiti wa kitongoji, Athumani Bakari, ambao wapo kituo cha polisi kwa zaidi ya wiki tatu wanashikiliwa na tumesikia wamepewa kesi ya kulawiti, kubaka, na unyang'anyi."

Naye Mwenyekiti wa CCM wa kijiji hicho, Vicent Matei, alisema Chama cha Mapinduzi kimesikitishwa na hali inayoendelea kijijini hapo na kudai kwamba wanahofu iwapo wananchi watashiriki uchaguzi wa serikali za mtaa. "Tunamwomba Rais Samia kuingilia kati suala hili ili kurejesha amani iliyopotea kijijini hapa kwani watu wengi wameyakimbia makazi yao."

Akijibu hoja hizo, mkuu wa wilaya ya Kondoa, Dkt. Hamis Mkanachi, alidai kutofahamu hatua ya wananchi kukamatwa na polisi na kuyakimbia makazi yao akisisitiza kuwa yeye kama mwenyekiti wa usalama hajapata taarifa hizo.

Dkt. Mkanachi alikiri kutembelea eneo lenye mgogoro ila alisema hakuwapigisha magoti viongozi wa kijiji hicho ila alichokifanya ni kwenda kumaliza mgogoro huo kwa kukabidhi eneo lenye mgogoro kwa wananchi walionunua kihalali baada ya uongozi wa kijiji hicho kushindwa kuwafidia.

"Usichukue maneno ukayaamini bila ushahidi tulitembea hadi site kwenye mgogoro, hakuna aliyekamatwa wala kupigishwa magoti na mimi nilienda kuwakabidhi wanunuzi haki yao."

"Hivi karibuni nilipigiwa simu na Mbunge Ashatu Kijaji akaniambia kuna mwenyekiti wa kijiji cha Hurui amekamatwa, nilifuatilia polisi kwa OCD akaniambia ni kweli yupo anakesi ya unyang'anyi sasa nimeshindwa kuelewa amemnyang'anya nani bado nafuatilia."

Mkuu huyo wa wilaya ameahidi kufuatilia kituo cha polisi ili kujiridhisha na tuhuma walizoshtakiwa viongozi wa kijiji hicho kama zina ukweli, alisisitiza kuwa asilimia 80 ya tuhuma hizo hazina ukweli.
 
Yani wanakijiji zaidi ya 15000,wote wawe wazushi?
🤣🤣🤣🤣Madaraka ya kulevya.
 
Acha wayakomeshe hayo mabushister.
Ndo yanaying'sng'ania ccm majinga hayo.
Yanyoosheni Tena Sana pigeni kabisa hayo mapumbavu mpaka akili iyakae sawa.hats kama mdingi wangu Yuko huko pigeni kabisa.

Ndo wanasababisha shida,dhiki Nchi hii kutokuisha Kwa ujinga wao.Pigeni kabisa.
 
Back
Top Bottom