CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 4,984
- 4,083
#Ntwara kuchweree,
Haya ndio matokea ya ziara ya Mhe Rais Dkt SAMIA Suluhu Hassan huko Kusini na neno langu kwa wateule wote ukiona mwenzako ananyolewa wewe tia maji.
Taarifa toka kwa Msemaji Mkuu Ikulu Bi Zuhra Yunus imesema kuwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewafukuza kazi baadhi ya wateule wake mkoani Mtwara kuanzia RAS,DC,DED mpaka DAS huku akiwaonya wateule wake wanaofanya kazi kwa mazoea,kushindwa kuwasikiliza na kuwajali Wananchi.
Niukweli usiopingika Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameacha kilio na simanzi kwa wateule wake huku akipeleka vicheko na furaha kwa Wananchi wa Mtwara ambao wameonyesha kutokuridhishwa na utendaji kazi wa wateule hao,
Baada ya hayo,Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Ndugu Abdallah Mohamed Malela, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara.
Hata hivyo amemteua Bi. Bahati Ibrahim Geuzye kuwa katibu Tawala Mkoa wa Mtwara.
Kabla ya uteuzi huu, Bi Bahati alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
Rais Mhe Dkt Samia Suluhu hakuishia kwa kumsukuma nje RAS pekee ametengua pia uteuzi wa Ndugu Hanafi Msabaha, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini,
Na sasa amemteua Bi. Mwanahamisi Mkunda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini. Kabla ya uteuzi huo Bi. Mkunda aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke
Vilevile Mhe Rais amemteua Dkt. Stephen Isaac Mwakajumilo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.
Naaliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bi Mariam Chaurembo amesukumwa nje.
Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hakuishia kwenye wakuu wa wilaya tu amesukuma nje pia wakurugenzi kadhaa,
Mhe rais amemteua Ndugu Hassan Bakari Nyange kuwa Mkurugenzi (DED) mpya wa Mtwara TC.
Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Nyange alikuwa DAS Wilaya ya Namtumbo.
Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi (DED) wa Wilaya ya Mtwara TC, Kanali Emmanuel Mwaigobeko atapangiwa kazi nyingine kama itaonekana inafaa,
Aidha Mhe Rais ametengua uteuzi wa Bi. Tatu Said Issike, Mkurugenzi wa Mtwara DC na kumteua Ndugu Abeid Abeid Kafunda kuwa Mkurugenzi (DED) wa Mtwara DC.
Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Kafunda alikuwa Mwanasheria katika Ofisi ya mkemia Mkuu wa Serikali.
Vilevile Mhe Rais amemteua Ndugu Reuben Sixbert Jichabu kuwa Mkurugenzi (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Aidha, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndugu Erica Yegella atapangiwa kazi nyingine.
Hakuishia hapo tu Mhe Rais amekula kichwa cha Katibu Tawala wa Wilaya ambapo amemteuar Fancis George Mgoloka kuwa Katibu Tawala wa Wilaya
(DAS) ya Namtumbo.
Kabla ya uteuzi huo Ndugu Mgoloka alikuwa Katibu Tarafa Mswaki - Kilindi Handeni.
Salamu hizi ziwafikie wateule wote wa Rais "mnaozungusha sketi" badala ya kuchapa kazi na kulinda kila rasilimali ya mwananchi pamoja na mwananchi mwenyewe kwani kama chama tunahitaji "kushinda kabla ya kushinda" Chaguzi zote zilizombele yetu.
#MAMAHAKAMATIKI
#Wekend Njema,
======