DED na DC wa Wilaya ya Mtwara Waliohamisha Mradi Hawafai Kukaa Ofisini: Rais Dkt. Samia Amechukua Hatua Sahihi kwa muda sahihi

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,328
8,246
Nakupongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kufanya uamuzi wa kuwatimua kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya (DED) na Mkuu wa Wilaya (DC) wa Wilaya ya Mtwara, kufuatia maamuzi yao ya kuhamisha mradi kutoka kata moja kwenda kata nyingine kutokana na madai kuwa wakazi wa kata iliyopoteza mradi wengi wao ni wapinzani wa chama tawala na sio wanaounga mkono serikali.

Kila mwananchi anayo haki ya kupata huduma bora na fursa za maendeleo bila kujali itikadi za kisiasa au mwelekeo wa kisiasa. Serikali inapaswa kuwa wakala wa maendeleo kwa kila raia, bila kujali chama chake cha siasa au mitazamo yake ya kisiasa.

Uhamishaji wa miradi na huduma unapaswa kufanyika kwa misingi ya kujenga na kuimarisha maendeleo na ustawi wa jamii. Kuchukua hatua za kubadilisha mipango kwa sababu tu ya mwelekeo wa kisiasa wa wakazi wa eneo fulani ni kinyume na dhana ya uwajibikaji wa kiuongozi. Badala yake, viongozi wanapaswa kuhamasisha ushirikiano na kujenga daraja kati ya wananchi wa pande zote za kisiasa ili kufanikisha malengo ya maendeleo.

Hivyo uamuzi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuwatimua kazi DED na DC wa Wilaya ya Mtwara ni hatua ya kuimarisha uwajibikaji. Kuchukua hatua kwa kujibu madai ya ubaguzi wa kisiasa katika utoaji wa huduma ni ishara ya uongozi unaowajibika na wa haki.

Kwa kuongezea katika jamii inayojali misingi ya haki, usawa, na maendeleo, uamuzi wa Rais wa kuwatimua kazi DED na DC wa Wilaya ya Mtwara ni hatua sahihi ya kusimamia uadilifu na usawa katika utoaji wa huduma za umma. Serikali inapaswa kuwa chombo cha kuwahudumia wananchi wake bila upendeleo wa kisiasa, na hatua hii inaleta matumaini ya kuona maendeleo endelevu yanayojengwa juu ya ushirikiano na maono ya pamoja.
 
🤣🤣🤣🤣🤣 kama DED au DC wake, majina yao ni... A B C .

Baada ya Mwezi Mmoja, Wahuni watamletea majina hayo ila Kwa Staili ya C B A.

Sasa kwakua Mbumbumbu Huwa ni msahaulifu na anayeogopa Kusoma , atawateua Tena !!
 
Ni Mradi Gani umebadilishwa? Kutoka Kata gani na kwenda kata gani?
Unafahamu hata Jina la DED huyo?
Unamfahamu DC wa Mtwara DC na wa Manispaa?
Kiufupi naona unakurupuka kutoa pongezi kwa mambo usiyoyajua....
Dalili ya Uchawa na roho mbaya
 
Kwahiyo kuhamisha mradi hadi umfukuze kazi? Kama waziri au RC tu wangetoa amri mradi kukaa mahali pake wangepinga?

Lipi kubwa kuuza lango la nchi na kuhamisha mradi kutoka kata moja kwenda nyingine?

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app

Sasa kama mawazo ya hao viongozi ni ya kibaguzi na kugawa wananchi kwa mlengo wa kisiasa, hao sio viongozi wakutufikisha nchi ya ahadi.
Kama na wew unasema mawaziri waache kufanya mambo yao ili kuwasimamia hao viongozi wanatumia ofisi zao kwa kukiuka majukumu yao kwa makusudi basi unamatatizo kichwani mwako.
Mda wa kuendelea na wajinga wajinga umepitwa na wakati kwani uvccm wengi tu wapo mtaani wanasubiri hizo nafasi.
 
Kuna mabaya mangapi yanafanywa naye kuonyesha ubora wa zanzibar na kuidunisha Tanganyika?

Juzi tu tanesco wanasamehe deni la umeme la zanzibar, lakini bara gharama za umeme zimekaza mbaya. Ametumia hekima gani kama kweli ana hekima?

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Nakupongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kufanya uamuzi wa kuwatimua kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya (DED) na Mkuu wa Wilaya (DC) wa Wilaya ya Mtwara, kufuatia
Moshi Arusha Ni wapinzani Sana Ila maendeleo yamepelekwa kwa Kasi ya 5 g
 
🤣🤣🤣🤣🤣 kama DED au DC wake, majina yao ni... A B C .

Baada ya Mwezi Mmoja, Wahuni watamletea majina hayo ila Kwa Staili ya C B A.

Sasa kwakua Mbumbumbu Huwa ni msahaulifu na anayeogopa Kusoma , atawateua Tena !!
Hakika hili pia linawezekana
 
Ni Mradi Gani umebadilishwa? Kutoka Kata gani na kwenda kata gani?
Unafahamu hata Jina la DED huyo?
Unamfahamu DC wa Mtwara DC na wa Manispaa?
Kiufupi naona unakurupuka kutoa pongezi kwa mambo usiyoyajua....
Dalili ya Uchawa na roho mbaya
Yaan ikikuingia roho ya kutafuta ukuu wa wilaya ushoga haukai mbali unajiropokea tu.hata hawajui hao waliotumbuliwq
 
🤣🤣🤣🤣🤣 kama DED au DC wake, majina yao ni... A B C .

Baada ya Mwezi Mmoja, Wahuni watamletea majina hayo ila Kwa Staili ya C B A.

Sasa kwakua Mbumbumbu Huwa ni msahaulifu na anayeogopa Kusoma , atawateua Tena !!
Mla mla leo, mla kesho kala nini?
 
Niliandika kuwauliza walipoleta kiuzi chao cha umbeya, mnafahamu zilizopelekea hao kutumbuliwa, wakakaa kimya.

Nikawawekea na video kamili, siyo kipande cha ushuzi wao walioweka kule.

Mama Samia hawezi kumuonea mtu hata siku moja, na hapendi raia zake waonewe, awe wa chama chocote kile. CCM haipo madarakani kujitumikia yenyewe, ipo madarakani kutumikia wote.
 
Yaan ikikuingia roho ya kutafuta ukuu wa wilaya ushoga haukai mbali unajiropokea tu.hata hawajui hao waliotumbuliwq
Mkuu umeshindwa kuchangia hoja yenye mantiki mpaka unaamua kutumia lugha ya matusi. Badirika boss sisi wengine hatujakulia matusi.
 
kama DED au DC wake, majina yao ni... A B C .

Baada ya Mwezi Mmoja, Wahuni watamletea majina hayo ila Kwa Staili ya C B A.

Sasa kwakua Mbumbumbu Huwa ni msahaulifu na anayeogopa Kusoma , atawateua Tena !!
Mbu mbu mbu ana wekewaga makaratasi mezani ana sign uku ana rembua macho
 
kama DED au DC wake, majina yao ni... A B C .

Baada ya Mwezi Mmoja, Wahuni watamletea majina hayo ila Kwa Staili ya C B A.

Sasa kwakua Mbumbumbu Huwa ni msahaulifu na anayeogopa Kusoma , atawateua Tena !!
Mbumbumbu kukushinda wewe M.D usijejitambua na roporopo ?!!!

#DoNotDoHarm
 
Back
Top Bottom