Rais Samia awarejesha kazini Watumishi zaidi ya elfu nne (4,000+) walioondolewa kipindi cha Magufuli kwa madai ya kugushi vyeti

Uanapotosha makusudi magufuli wakati anahutubia watumishi kule bandarini aliwaambia kama wee ni lasaba ni umejaza lasaba hamna mwenye shida naye ila mtu la saba anafoji ni form four uki mwambia alete cheti cha form anaruka ruka
Ni kweli waliondolewa la Saba kimakosa ndo hao walisharuhusiwa kurudi na wengi walikuwa kwenye kustaafu hivyo walirudi Ili kuchukua mafao yao.
 
Kwahiyo kughushi cheti si kosa kisheria au sijaelewa vzr.

Kutoboa Mwafrika haitakaa itokee.

Kwamba umeghushi umekatwa halafu serikali inakupongeza.

Sasa yule aliyekuwa anatibu watu isivyo kiutaratibu yeye ana mkosi.

Ni kama tunaenda na pweza wa utabiri
Tz hakuna sheria hata Machinga waachwe watakavyo, kuwatoa ni uonevu tu maana hakuna sheria inayoongoza nchi ni Siasa tu za kijingajinga
 
Kweli! Huyu kama aliingia kwa kufoji lazima alikua ashtakiwe na afungwe jela.
Enzi za nyerere kununua jina na kurudia darasa la saba kwa jina la mtu ilikuwa kawaida kwani mfumo ulikuwa hauruhusu mtu kujiendeleza kivingine iwapo utafeli darasa la saba,, ilikua either uwe mwalimu wa UPE au uapply kwenda polisi, sasa kwa mtu mwenye ndoto kubwa, labda kuwa doctor, injinia, meneja, mkurugenzi, etc, walipofeli la saba, option iliyobaki ilikuwa kununua jina na kurudia shule,, hapakuwa na shule nyingi za private eti mtu angeweza kujiunga na kuendelea na masomo ya sekondari,
Tatizo lilikuwa la kimfumo zaidi,, miaka ya sasa mtu hawezi kutumia jina la mtu, wakati kuna options nyingi mno,,
So SSH kuamua hao warudi kazini ni Reasonable na ubinaadamu pia,,
 
Magufuli angekuwa hai angekuuliza utamlipaje stahiki mtu aliyeidanganya serikali na kujipatia ajira na mshahara kiudanganyifu?

Kama unataka kutekeleza sheria basi inabidi uwe bandidu kotekote yaani, hakuna mafao wala kurudishwa kazini.

Ila wewe ukiona bora alipwe mafao tu, mwingine ansona bora arudi kazini tu

Ni mtizamo tu wa kila mmoja
Kuna watu wengi mfano bashite, bagaile, etc hii amri haikuwagusa,, huwezi ku cherry pick hivi vitu
 
Utadhani hakuwa kwenye hiyo serikali.

Ipo siku Rais mwingine anaetokana na CCM, atakuja kumuomba radhi Mbowe kwa kesi ya kusingiziwa, na pengine kumlipa fidia, na CCM hawa hawa wanafurahia Mbowe kuwekwa ndani, watampongeza huyo Rais.

Kuwaelewa CCM na akili zao, ni vigumu kama ilivyo vigumu kujua Mungu alitoka wapi au kati ya yai na kuku, kipi kilianza.

Anyway, awalipe fidia na wale waliobomolewa nyumba zao maeneo ya Kimara wakati wa Mwendazake.
Kumbe Salary Slip HUJUI kati ya kuku na yai kipi kilianza? FYI Mungu hakuumba yai bali kuku. Kuku ndiye aliyeanza na yai ni mchakato tu wa kiendeleza kizazi cha kuku!
Usishangae tena eti kipi kilianza.
 
Ni wazi kabisa mtu akifoji kitu official huyu ni mualifu na adhabu yake inaweza kuwa kifungo mpaka miaka7.

Hamna kitu kinasikitisha kama mtu unahangaike kusoma kwa bidii pamoja na changamoto zote unakomaa, halafu ajira aje kupewa mtu ambaye kaamua kutumia shortcut ya kufoji vyeti, hii haiko sawa.

Nilitegemea Hawa watu wawe mfano wa onyo la kughushi vyeti lakini ndio kwanza wanarudishwa kazini, ni sawa na mtu aliefungiwa account yake benki alipokamatwa akingiza noti feki ila sasa anasamehewa na zile noti feki zinahesabiwa kuwa orijino.

Vijana kibao wapo mitaani wamesoma kwa shida ili kumaliza degree / masters, kiukweli hawatendewi haki hawa vijana, Binafsi sikuwa fan wa magufuli lakini kuna mambo machache sana aliyoyafanya nilikuwa upande wake likiwemo hili swala la kuchomoa wanao ghushi vyeti,

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora imetangaza kuwarejesha kazini Wafanyakazi zaidi ya elfu nne (4000+) ambao waliondolewa kazini kutokana na kugushi vyeti katika maeneo mbalimbali lakini sasa kwa huruma ya Rais Samia watarejeshwa kazini kwa sharti la kuwa wawe wamejiendeleza kielimu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Mohamed Mchengerwa amesema "wale walioweza kujiendeleza ambao ni zaidi ya 4100 tayari wamerejeshwa kazini, pia tunao Watumishi 1150 ambao hawakufanikiwa kujiendeleza maana yake hawana sifa za kutosha kuendelea kuitumikia Serikali japo walikua ni Watendaji wazuri”

Rais Samia alishatuagiza kwamba hawa 1150 kutokana na utendaji wao uliotukuka Watumishi hao wote walipwe haki zao na stahiki zao kama vile wapo kazini kwahiyo watalipwa"
Vizuri. Cheti cha form IV hakumuondolei mtu ujuzi alioupata akiwa chuoni plus uzoefu.
 
Hii nchi KWA Sasa inapoelekea ni shimoni kabisa, hata hyo elimu ambayo ni nguzo ya nchi KWA Sasa inadharaulika na itaendelea kudharaulika Zaidi. Hivi mtu akifoji kitu official si ni mualifu na adhabu yake inaweza kua kifungo mpaka miaka7?


Nilitegemea Hawa watu kua jela Kwa Sasa, lakini ndo kwanza wanarudishwa kihuni huni tu.


Yaani nchi KWA Sasa haina Dira
Hao watu kabla ya kutolewa kazini walikuwa wanafanya kazi Serikalini mbona nchi haikuwa Shimoni? Fine, kabla na baada ya the so called vyeti feki kutoka nchi ilipiga hatua gani?
 
Enzi za nyerere kununua jina na kurudia darasa la saba kwa jina la mtu ilikuwa kawaida kwani mfumo ulikuwa hauruhusu mtu kujiendeleza kivingine iwapo utafeli darasa la saba,, ilikua either uwe mwalimu wa UPE au uapply kwenda polisi, sasa kwa mtu mwenye ndoto kubwa, labda kuwa doctor, injinia, meneja, mkurugenzi, etc, walipofeli la saba, option iliyobaki ilikuwa kununua jina na kurudia shule,, hapakuwa na shule nyingi za private eti mtu angeweza kujiunga na kuendelea na masomo ya sekondari,
Tatizo lilikuwa la kimfumo zaidi,, miaka ya sasa mtu hawezi kutumia jina la mtu, wakati kuna options nyingi mno,,
So SSH kuamua hao warudi kazini ni Reasonable na ubinaadamu pia,,
Hakuna jema hapa kwetu, kila analofanya mtu wengine watalalamika
 
Vizuri. Cheti cha form IV hakumuondolei mtu ujuzi alioupata akiwa chuoni plus uzoefu.
Hao watu kabla ya kutolewa kazini walikuwa wanafanya kazi Serikalini mbona nchi haikuwa Shimoni? Fine, kabla na baada ya the so called vyeti feki kutoka nchi ilipiga hatua gani?
Acheni kutete ujinga aisee, mtu kaghushi cheti huyo hana utofauti na jambazi kisheria
 
Nimeipenda, mtu hawezi kufanya kazi miaka 10 halafu unamtoa kirahisi tu...
Mwizi wa cheti au mtumia cheti cha kugushi ni mhalifu anatakiwa kufikishwa mahakamani. Serikali ihalalishe kugushi na kutumia vyeti vya watu wengine.
 
Back
Top Bottom