Rais Samia aongoza kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu ya Dar es salaam

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,714
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge ameongoza kikao cha Baraza la mawaziri ikulu ya Dar hii leo jumapili.

Habari hiyo iliyopambwa na picha ya wajumbe wa baraza la mawaziri ambao ni mawaziri imesambaa na kuonekana katika mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo imeonekana kugusa na kuteka hisia za watu mbalimbali ,ambao wameonyesha kufurahishwa na uchapa kazi wa Mheshimiwa Rais. Maana wengine walitegemea pengine kumuona akiwa kapunzika kama siku ya mapumziko na wanavyo pumzika watumishi wengine.

Lakini wameshangaa na kufurahishwa kuona Rais wao kipenzi akiendelea na kazi bila kujali leo ni siku gani.hii inamaanisha kuwa Rais wetu muda wote yupo kazini kwa ajili ya kuwatumikia watanzania na kuweka mipango na sera nzuri za kuwakwamua kiuchumi Watanzania.maana yake ni kuwa kero za wananchi zinasikilizwa na kupatiwa majibu muda wote bila kujali siku wala muda.

Kwa hakika Rais Samia ni mfano wa kuigwa na alama ya uchapa kazi na uongozi uliotukuka wenye kugusa maisha ya watu.Rais Samia anatoa somo kwa viongozi wa chini kufanya kazi kwa kujituma na muda wote katika kuwahudumia watanzania.ametoa soma kuwa ukiwa kiongozi kazi yako na maisha yako ni kwa ajili ya kuleta matumaini na nuru kwa maisha ya watu na siyo kubweteka tu na kujikalia tu utafikiri kocha ambaye timu yake imeshinda uwanjani na tayari imetangaza ubingwa.

Rais Samia muda wote anawatafutia ushindi wa maisha na uchumi watanzania.ndio maana anaonekana akiwa mchaka mchaka katika kukimbizana na muda wa kukamilisha miradi mbalimbali pamoja na mipango mbalimbali yenye maslahi kwa Taifa na ustawi wa watanzania.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Unasikilizia uteuzi?
Hapana bali najiona fahari sana kuongozwa na kuwa sehemu ya historia ya kuongozwa na Rais Samia.maana nitakuwa na mengi sana ya kusimulia kwa vizazi vijavyo panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu. Nitawaleeza watu uchapa kazi ,uzalendo na upendo mkubwa alionao Rais Samia Katika Taifa letu na namna alivyolipaisha kimaendeleo kama ndege vita.
 
Back
Top Bottom