Rais Samia awaapisha Wakuu wa Mikoa. Afanya mabadiliko madogo, Kafulila apelekwa Simiyu, Mongella aletwa Arusha

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
665
1,000

Dkt. Mpango: Wakuu wa Mikoa wasiwe walevi na wazinzi
Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, amewataka Wakuu wa Mikoa walioapishwa Mei 19, 2021 wafanye kazi kwa weledi Asema Kiongozi mzuri ni yule mwenye busara na bidii ya kazi

Jaji Mkuu: DPP ni chujio la kwanza la haki
Prof. Ibrahim Juma amesema, "DPP hawezi kuingiliwa na mtu yeyote, hata Jaji Mkuu hana mamlaka ya kuingilia kazi yake" Asema Mkurugenzi wa Mashtaka amepewa wajibu wa kuangalia maslahi ya Taifa

Spika Ndugai: Wakuu wa Mikoa msijione Marais
“Wapo Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanaamini kule waliko wao ni Marais, utasikia Mimi Rais wa Mkoa huu au Wilaya hii nani kasema?, Rais wa Nchi hii ni mmoja tu, Samia Suluhu Hassan, ukijivisha koti ambalo si lako matokeo yake unaweza kufanya mambo ukidhania wewe Rais”

Rais Samia afanya Mabadiliko teuzi za Wakuu wa Mikoa Arusha na Simiyu
John Mongella aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha

David Kafulila ambaye awali aliteuliwa kuwa RC Arusha atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

“Kuna mabadiliko madogo nimefanya, Kafulila nilimteua kuwa RC Arusha na Mongella RC Simiyu, nimeamua Mongella kwasababu ulikuwa unaongoza Mkoa mkubwa basi ukawe RC Arusha na Kafulila kwasababu ndio anaanza alikuwa RAS basi akawe RC Simiyu” Rais Samia

“Baada ya shughuli hizi za kuapishana na kupiga picha Wakuu wa Mikoa na Wateuliwa wengine mtarudi hapa na tutakuwa na kikao cha kazi kwahiyo kwasababu nina mambo mengi ya kuongea na nyinyi leo tuishie hapa tutakutana kwenye kikao cha kazi”

“Wote mlioapa na mlioteuliwa hongereni sana, nasema hongereni kwasababu Tanzania kuna Watu wengi na 15% wangefaa kuteuliwa lakini mmeteuliwa nyinyi, naamini mnapokwenda kufanya kazi zenu mtasimama na Mungu”
1621436034861.png
1621436048199.png
 

Fatma-Zehra

Senior Member
Oct 18, 2020
148
1,000
Sijafurahia reason ya kubadilisha wakuu wa mikoa. Mongela anapelekwa Arusha kwa sababu ni "mzoefu" na majiji na Kafulila ni mpya. This is not a reason for sure kwa sababu yule David, although ni "mpya" ni mbunifu sana kuliko Mongela (kwa mtazamo wangu).

Kama kweli hayo ndiyo majukumu ya mkuu wa mkoa as per VP Phillip, wakuu wa mikoa wanaoweza kufanya kazi hiyo popote pale ni Kafulila, Mtaka, and Queen.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,264
2,000
Mama anajitahidi sana kuwaamisha wapinzani wake yw kwamba hicho kiti alicho kikalia kimemzidi nguvu! Haiwezekani haya mambo yaendelee kujirudia!

Alijichanganya kwa yule Dogo wa Uvccm kule TPDC! Na leo anajichanganya tena kwa Kafulila.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom