RC Makonda: Rais Samia ameipendelea Arusha, amemtoa mwanae wa pekee na kumleta Arusha

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,104
Nafahamu Arusha ni mji wa kitalii, Dkt. Samia Suluhu Hassan (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ameamua kwa makusudi kuipendelea Arusha hata akamtoa mwanaye wa pekee (Paul Makonda) ili aje aungane nanyi, angeweza kuniacha nikafanya kazi ya Uenezi na amesema mwenyewe nimeifanya vizuri lakini kwa kuwapendeni wakazi wa Arusha akasema Makonda nenda kaanzie pale alipoishia kaka yako Mongela (John Mongela, aliyekuwa Mkuu wa mkoa Arusha, ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara)

"Na katika utalii tuna maeneo matatu (3), utalii wa kwanza ambao Dkt. Samia ameufanya ni kufanya 'Royal Tour' na alivyotoka Marekani kituo chake cha kwanza katika nchi yetu Tanzania alitua KIA (uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro) kuja kusema nanyi katika uzinduzi wa 'Royal Tour', alitaka kila kijana, kila mama, kila muuza mchicha amletee mtu mwenye pesa ili maisha yake yaende, na ndio maana leo hii utalii umevunja record"

"Katika eneo hilo (la utalii) ameniagiza nishirikiane na ndugu zetu wa uwekezaji (TIC) kuhakikisha tunaongeza Hoteli za kutosha Arusha, tukiongeza Hoteli maana yake tumeongeza ajira, tukiongeza ajira tunakuwa tumeongeza kipato kwa wakulima na hivyo tutaboresha maisha ya wananchi"

Paul Makonda ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Arusha amezungumza hayo wakati akizungumza na wananchi wa Arusha waliojitokeza kumpokea kwenye viunga vya ofisi ya Mkuu wa mkoa huo leo, Jumatatu Aprili 08.2024

Chanzo: Jambo TV

=======

Uteuzi kuwa Mkuu wa Mkoa Arusha
Matukio baada ya Uteuzi
 
Back
Top Bottom