Rais Samia atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo 18 vya abiria wa basi la Alfa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
IMG_8832.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kufuatia vifo vya watu 18 vilivyotokea katika ajali ya gari.

Ajali hiyo imetokea leo saa 5 asubuhi katika kata ya Uchama, tarafa ya Nyasa wilaya ya Nzega mkoani humo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora CP Richard Abwao waliopoteza maisha ni wanaume 14 akiwemo mtoto mmoja na wanawake 4.

Majeruhi ni 60 ambapo majeruhi 51 wanatibiwa Hospitali ya Wilaya ya Nzega, 19 wako Hospitali ya Rufaa ya Nkinga, 1 anatibuwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando na 9 wametibiwa na kuruhusiwa.

CP Abwao amesema ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Alfa lililokuwa likisafiri kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam ambalo liligongana na Lori la mafuta lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza.

Rais Samia anawapa pole majeruhi wa ajali hiyo pamoja na wafiwa wote na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema Peponi. Amina.

Pia soma: 18 wafariki ajalini Nzega baada ya basi kugongana na lori
 
CP Abwao amesema ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Alfa lililokuwa likisafiri kutoka Mwanza kwenda Dares Salaam ambalo liligongana na Lori la mafuta lililokuwa likitoka Dares Salaam kuelekea Mwanza.

Rais Samia anawapa pole majeruhi wa ajali hiyo pamoja na wafiwa wote na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema Peponi. Amina.​

WhatsApp Image 2023-10-21 at 20.35.05.jpeg
 
Hizi ajali mpaka zitumalize tu.
Pole kwa familia zilizofiwa na ndugu zao, na pole kwa majeruhi pia.
 
Kwa sasa, uwapo barabarani, upo kwenye mazingira hatarishi sana.

Kutokana na kuzaliana kwa kasi kwa Watanzania, ili kukidhi mahitaji ya watu, kumekuwa na ongezeko kubwa sana la malori makubwa barabarani, na kwa vyovyote, yatazidi kuongezeka. SGR hata kama itakamilika, , kutokana na uwezo mdogo wa watumishi wa umma katika mambo ya biashara, bado watu wengi wataendelea kutumia malori. TAZARA inapitia Mbeya na Makambako, kwenye mikoa inayozalisha chakula na mbao kwa wingi sana, lakini vyote vinasafirishwa na malori, licha ya kwamba TAZARA ipo. Kama huko tumeshindwa, kwa nini tutarajie SGR ya kwenda kanda ya Ziwa itavutia watu wengi kuitumia katika usafirishaji mizigo?

Ni vema tukatambua kuwa mrundikano wa malori makubwa utaendelea kuongezeka kwenye barabara zetu. Ni vema kuanza kujenga lanes maalum za malori. Mathalani, tunakuwa na highways zenye lanes nne, mbili za malori, mbili za magari mengine. Na lanes hizi zitenganishwe kwa umbali angalao wa mita 50 mpaka mita 100.

La sivyo, kuna wakati utafika, barabara zitakuwa hazipitiki. Madereva wataendelea kulazimisha ili wawahi kufika wanakoenda, na hapo ajali zitaongezeka mara dufu.
 
We jmaa Yan Malori yapite njia yake mara nchi nzima ....we uliskia wapi, bajeti .
 
Na tutazidi kuishaaa na maajali
Waache waZidi kuwaendekeza maderevA wazembe na vichaaa

Ukiwaongezea na matrafik wala rushwa...
Watu watakufa na kufa sanaa tu,mtatoa pole sanaaa

Ova
 
Madereva wengi wa mabasi na pia wale wa malori, wana mchango mkubwa sana kwenye hizi ajali kutokana tu na uendeshaji wao wa kizembe barabarani.
 
Kwa sasa, uwapo barabarani, upo kwenye mazingira hatarishi sana.

Kutokana na kuzaliana kwa kasi kwa Watanzania, ili kukidhi mahitaji ya watu, kumekuwa na ongezeko kubwa sana la malori makubwa barabarani, na kwa vyovyote, yatazidi kuongezeka. SGR hata kama itakamilika, , kutokana na uwezo mdogo wa watumishi wa umma katika mambo ya biashara, bado watu wengi wataendelea kutumia malori. TAZARA inapitia Mbeya na Makambako, kwenye mikoa inayozalisha chakula na mbao kwa wingi sana, lakini vyote vinasafirishwa na malori, licha ya kwamba TAZARA ipo. Kama huko tumeshindwa, kwa nini tutarajie SGR ya kwenda kanda ya Ziwa itavutia watu wengi kuitumia katika usafirishaji mizigo?

Ni vema tukatambua kuwa mrundikano wa malori makubwa utaendelea kuongezeka kwenye barabara zetu. Ni vema kuanza kujenga lanes maalum za malori. Mathalani, tunakuwa na highways zenye lanes nne, mbili za malori, mbili za magari mengine. Na lanes hizi zitenganishwe kwa umbali angalao wa mita 50 mpaka mita 100.

La sivyo, kuna wakati utafika, barabara zitakuwa hazipitiki. Madereva wataendelea kulazimisha ili wawahi kufika wanakoenda, na hapo ajali zitaongezeka mara dufu.
Sikubishii nakusoma unajua
 
Hela za kutengeneza barabara kubwa zenye viwango hazipo Ila hela za magoli ya simba na yanga zipo.
Hata kama situmii mabasi kwenye safar zangu lakini ndugu zangu wanatumia ,daah hii itatisha.
 
View attachment 2788512Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kufuatia vifo vya watu 18 vilivyotokea katika ajali ya gari.

Ajali hiyo imetokea leo saa 5 asubuhi katika kata ya Uchama, tarafa ya Nyasa wilaya ya Nzega mkoani humo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora CP Richard Abwao waliopoteza maisha ni wanaume 14 akiwemo mtoto mmoja na wanawake 4.

Majeruhi ni 60 ambapo majeruhi 51 wanatibiwa Hospitali ya Wilaya ya Nzega, 19 wako Hospitali ya Rufaa ya Nkinga, 1 anatibuwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando na 9 wametibiwa na kuruhusiwa.

CP Abwao amesema ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Alfa lililokuwa likisafiri kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam ambalo liligongana na Lori la mafuta lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza.

Rais Samia anawapa pole majeruhi wa ajali hiyo pamoja na wafiwa wote na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema Peponi. Amina.

Pia soma: 18 wafariki ajalini Nzega baada ya basi kugongana na lori
Evidence: Wanaume tuna muda mfupi sana wakuishi duniani

"Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora CP Richard Abwao waliopoteza maisha ni WANAUME 14 akiwemo mtoto mmoja na wanawake 4."
 
Madereva wa Siku Hizi ni Watoto wadogo wadogo
Siyo watoto wadogo tu lakini kwa wastani ukimtazama dereva aliyenyuma ya usukani wa lori, basi au pikipiki huoni kama anajali kuhusu thamani ya uhai wake au wa wengine. Waajiri hawafanyi usaili? Watetezi wetu wa thamani ya uhai wetu wao wanaona jukumu lao kuu ni kutoa rambirambi za nguvu! Hakuna wa kuwajibika wala kuwajibishwa! Mwenyezi Mungu Aweke mkono wake Tanzania ipate uongozi wa dhati unaostahili ili ajali za kweli tu na siyo za uzembe ndiyo zitusibu!
 
Back
Top Bottom