Rais Samia atuma salamu za pole kufuatia kifo cha mzee Kassum

Alnoor Khasum hajawahi kuwa waziri wa fedha. Aliyekua waziri wa fedha Ni Amir Jamal.
Alnoor alikua maji na nishati wakati huo lile jengo karibu na posta ya zamani likiwa Ni Kati ya majengo marefu sana Dar. Huyu mzee alikua anaendesha gari mwenyewe kuja kazini gari yake naikumbuka ilikua Peugeot 505.
Wakati hoja kuhusiana na Wizara yake ya Maji na Nishati zikipamba moto alikua anaongea Kiingereza mwanzo mwisho Bungeni
 
Alnoor Khasum hajawahi kuwa waziri wa fedha. Aliyekua waziri wa fedha Ni Amir Jamal.
Alnoor alikua maji na nishati wakati huo lile jengo karibu na posta ya zamani likiwa Ni Kati ya majengo marefu sana Dar. Huyu mzee alikua anaendesha gari mwenyewe kuja kazini gari yake naikumbuka ilikua Peugeot 505.
Shikamoo babu
 
Al Noor Kassum was a Tanzanian politician. Educated in Tanzania and the United Kingdom, where he was called to the Bar at the Inns of Court in London, Al Noor Kassum was a prominent figure in Tanzanian politics and the Ismaili Muslim community after the country's independence.
Born: 11 January 1924, Dar es Salaam, Tanzania
Died: 18 November 2021
Party: Chama Cha Mapinduzi
Books: Africa's Winds of Change: Memoirs of an International Tanzanian
Duh! Kwahiyo 97 yiaz oldi

Ndomaana simjui huyo

Wengine tutasikia tu hata hamsini sikuhizi kufika ni ishu

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
RIP Mzee Al-noor Kassum. Huyo kwenye Wizara ya Nishati na Madini ndio legend, hasa ukiongelea miradi kama Umeme wa bwawa la Mtera.
 
Sijui ni waziri gani wa sasa ambaye unaweza kumlinganisha na huyu waziri. Huyu alikuwa ni waziri hasa, kuanzia maadili ya uongozi hadi weledi.

Ni waziri pekee mwenye asili ya kihindi aliyeaminika sana na Mwalimu Nyerere. Wakati wote alishika wizara mama.

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya watu kama hawa kwa Taifa letu maana faida zao kwa watanzania wote, hazihesabiki wala kupimika.

Baba yetu uliye muweza wa yote, tunaomba umjalie pumziko la amani furaha mzee wetu huyu maana maisha yake ya hapa Duniani ameyapa thamani kubwa. Mema yake yalipie mapungufu yake. Amina.
Wako 2 waliaminiwa sana huyu na Marehemu Ameir Jamal ....no best mno mno Mwl alimfuata Canada siku zake mwisho akamuomba PM Canada ampe matibabu....sababu alikuwa raia wa Tanzania.....inabidi awe raia Canada kupata 1st classt treatment inabidi apewe uraia......ili atibiwe bahati mbaya alifariki.....kabla matibabu kuanza alikuwa akiwa masikini kabisa....
 
Alnoor Khasum hajawahi kuwa waziri wa fedha. Aliyekua waziri wa fedha Ni Amir Jamal.
Alnoor alikua maji na nishati wakati huo lile jengo karibu na posta ya zamani likiwa Ni Kati ya majengo marefu sana Dar. Huyu mzee alikua anaendesha gari mwenyewe kuja kazini gari yake naikumbuka ilikua Peugeot 505.
Zaidi ya kuendesha gari mwenyewe Mzee Alnoor hotuba zake mjengoni zilikuwa lugha ya Malkia (English).Kuna mijitu kama ingekuwa bungeni kipindi chake sijui kama wangeeelwa tukianza na Musukuma na yule Bwege wa Mtera.
 
Ndio kwa miaka 60 tumefika hapa kwa weledi wake na sifa zote.
Ukitaka kujua kama hatua imepigwa au la kitaalamu unachukua baseline data yaani pale ulipoanza kuendelea hali ilikuwaje na sasa ikoje. Maendeleo hayapimwi subjectively.

Al noor Kassum kama nawaziri wote wa awamu ya kwanza walikuwa waadilifu na wa.meifanyia nchi makubwa sana .

Fikiria katika wizara hiyo ya nishati hakufanya ufisadi wowote lakini huyo jamaa wa msoga aliposhika tu wizara hiyo hiyo tena kwa muda mfupi tukapigwa na ufisadi wa IPTL kwa mkataba wa miaka ishirini. Ulipoisha tu tukapigwa tena pesa za escrow; na sasa kupitia mtoto wa rafikiye tunapigwa US Dollar miliion 30.
 
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa pole Watanzania, wanafamilia kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye Serikali ya awamu ya kwanza na pili, Al noor Kassum.

“Rais Mheshimiwa Samia amenituma niwape pole ndugu, familia na wote walioguswa na kifo cha Mzee Al noor Kassum. Mzee Kassum amefanya mambo makubwa sana kwenye nchi hii. Ametumikia Taifa kwa weledi, uaminifu na uadilifu mkubwa, Watanzania hatuwezi kumsahau.

Salamu hizo za pole zimetolewa leo (Jumamosi, Novemba 20, 2021) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia katika kuaga mwili wa Marehemu Kassum kwenye viwanja vya Karimjee mkoani Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa watumishi wa umma kuyaendeleza yote mazuri aliyoyafanya wakati wa utumishi wake ili Taifa liendelee kushamiri kwa maendeleo na amani. “Tuliokuwepo kwenye madaraka tuendeleze utawala unaojali wananchi kama alivyokuwa akifanya marehemu.”

Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania kila mmoja kwa imani yake waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu Mzee Al noor Kassum.

Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema marehemu Mzee Kassum alimfundisha namna ya kufanyakazi na kuishi vizuri kati ya Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Waziri. Alimpokea wizarani alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati, Maji na Madini wakati huo Mzee Kassum akiwa Waziri wa Wizara hiyo.
Enzi hizo wizara zikiongozwa na mawaziri sio siku hizi unachukua Kibaka mwigulu anakabidhiwa wizara nyeti ya fedha kisha utegemee kukua kwa uchumi!
 
Ndio mhindi mtanzanzia Kama wewe ulivyo mndengereko mtanzania
Iko haja wahindi watanzania wakumbukwe Ajira serikalini na wizara kupewa uwaziri vyeo vya kisiasa nk Kama zamani tumewasahau sana

Ubaguzi umetamalaki sana nchini
Yaani kuanzia mzawa Msomali kosa
Mzawa mwarabu kosa


Serikali ndio huwa zinaleta ubaguzi kwani wananchi hufuata amri tu zilizowekwa

Priti Patel ni Waziri wa mambo ya ndani na Rishi Sunak akiwa wa fedha, huku Sadiq Khan akiwa Mayor wa jiji la London
Yote haya ni kwa sababu ya serikali inalazimisha hivyo na ubaguzi mwiko

Una uwezo unapata kazi
Huwezi kukuta bunge letu la Tz linaongelea ubaguzi hata siku moja you know why? Wao ndio wanataka hivyo
 
Alnoor Khasum hajawahi kuwa waziri wa fedha. Aliyekua waziri wa fedha Ni Amir Jamal.
Alnoor alikua maji na nishati wakati huo lile jengo karibu na posta ya zamani likiwa Ni Kati ya majengo marefu sana Dar. Huyu mzee alikua anaendesha gari mwenyewe kuja kazini gari yake naikumbuka ilikua Peugeot 505.
Peugeot 504 bwana!
 
..Al Noor Kassum, akiwa waziri, kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa wizara [jina nimelisahau], waliwezesha vijana wetu kwenda kusoma Uhandisi wa Maji India, kwa udhamini wa nchi moja ya Skandinavia.

..Kuna nchi moja ya Skandinavia ilitoa msaada wa fedha kusomesha wahandisi wa maji wa Tanzania.

..Al Noor Kassum na Katibu Mkuu wakaona fedha hizo zingeweza kusomesha vijana wengi zaidi kama wangekwenda India badala ya Skandinavia.

..Kwa hiyo wakaweza kuwashawishi wafadhili wa Kiskandinavia wadhamini vijana wetu kwenda kusoma India na hilo liliwezesha wahandisi wengi wa maji kupata elimu ya chuo kikuu India.

..Kama unamfahamu Engineer wa Maji aliyehitimu India miaka ya 1980 basi uwezekano mkubwa alidhaminiwa kwa mpango uliowezeshwa na Waziri Al Noor Kassum na Katibu Mkuu wake.
 
Back
Top Bottom