Rais Samia atuma salamu za pole kufuatia kifo cha mzee Kassum

Anna Nkya

Member
Oct 21, 2021
69
341
RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa pole Watanzania, wanafamilia kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye Serikali ya awamu ya kwanza na pili, Al noor Kassum.

“Rais Mheshimiwa Samia amenituma niwape pole ndugu, familia na wote walioguswa na kifo cha Mzee Al noor Kassum. Mzee Kassum amefanya mambo makubwa sana kwenye nchi hii. Ametumikia Taifa kwa weledi, uaminifu na uadilifu mkubwa, Watanzania hatuwezi kumsahau.

Salamu hizo za pole zimetolewa leo (Jumamosi, Novemba 20, 2021) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia katika kuaga mwili wa Marehemu Kassum kwenye viwanja vya Karimjee mkoani Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa watumishi wa umma kuyaendeleza yote mazuri aliyoyafanya wakati wa utumishi wake ili Taifa liendelee kushamiri kwa maendeleo na amani. “Tuliokuwepo kwenye madaraka tuendeleze utawala unaojali wananchi kama alivyokuwa akifanya marehemu.”

Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania kila mmoja kwa imani yake waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu Mzee Al noor Kassum.

Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema marehemu Mzee Kassum alimfundisha namna ya kufanyakazi na kuishi vizuri kati ya Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Waziri. Alimpokea wizarani alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati, Maji na Madini wakati huo Mzee Kassum akiwa Waziri wa Wizara hiyo.
 
Alnoor Khasum hajawahi kuwa waziri wa fedha. Aliyekua waziri wa fedha Ni Amir Jamal.
Alnoor alikua maji na nishati wakati huo lile jengo karibu na posta ya zamani likiwa Ni Kati ya majengo marefu sana Dar. Huyu mzee alikua anaendesha gari mwenyewe kuja kazini gari yake naikumbuka ilikua Peugeot 505.
 
Dah, sikujuwa kuwa Alnoor Kassum alikuwa bado yu hai!

Ukisikia mawaziri, hao ndio walikuwa mawaziri kwelikweli na wanaonekana na kutenda na kujibeba kama mawaziri. Akisimama kusema jambo watu wanasikiliza. Akiiwakilisha nchi anabeba heshima ya nchi popote anapokuwa.
 
Sijui ni waziri gani wa sasa ambaye unaweza kumlinganisha na huyu waziri. Huyu alikuwa ni waziri hasa, kuanzia maadili ya uongozi hadi weledi.

Ni waziri pekee mwenye asili ya kihindi aliyeaminika sana na Mwalimu Nyerere. Wakati wote alishika wizara mama.

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya watu kama hawa kwa Taifa letu maana faida zao kwa watanzania wote, hazihesabiki wala kupimika.

Baba yetu uliye muweza wa yote, tunaomba umjalie pumziko la amani furaha mzee wetu huyu maana maisha yake ya hapa Duniani ameyapa thamani kubwa. Mema yake yalipie mapungufu yake. Amina.
 
Amir Jamal,alikuwa mhindi,na alikuwa waziri wa fedha,kwa kweli Nyerere,hakuwa mbaguzi wa dini,kabila wala rangi.Nyerere aliwasaidia wapalestina,katika kujikomboa kwa kuwapa mpaka nyumba za kukaa wapalestina,Dar es Salaam.
 
Alnoor Khasum hajawahi kuwa waziri wa fedha. Aliyekua waziri wa fedha Ni Amir Jamal.
Alnoor alikua maji na nishati wakati huo lile jengo karibu na posta ya zamani likiwa Ni Kati ya majengo marefu sana Dar. Huyu mzee alikua anaendesha gari mwenyewe kuja kazini gari yake naikumbuka ilikua Peugeot 505.
alikuwa waziri wa fedha na utawala wa jumuiya ya afrika mashariki.
 
Huyo marehemu ndio namsikia Leo,
Hata Mbowe watajitokeza wengi kuja kumwekezea alivyokuwa mvumilivu kushitakiwa kwa HISIA.

..kama umesoma post ya kwanza Al Noor Kassum alikuwa waziri wa maji nishati na madini.

..akiwa ktk nafasi hiyo Raisi Mwinyi alimteua Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Naibu waziri ktk wizara hiyo.

..Baada ya muda Jakaya Kikwete aliteuliwa kuwa waziri kamili wa wizara ya maji nishati na madini.

..Baada ya hapo Kikwete aliteuliwa waziri wa fedha, waziri wa mambo ya nje, na baadae akawa Raisi.
 
Back
Top Bottom