Dr Mpango: Lowassa alikuwa mchapakazi na Mpenda Maendeleo, nitafikisha salamu za Rais Samia kwa mama Lowassa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,992
142,008
Makamu wa Rais Dr. Mpango amesema anajua Mchango mkubwa uliotolewa na Mzee Lowassa kwenye Maendeleo ya Arusha.

Lowasa alikuwa mchapakazi na Mpenda Maendeleo hivyo nikitua DSM nitakwenda Moja kwa Moja nyumbani kwa familia ya marehemu na nitazifikisha salamu zenu, amesema Dr. Mpango.

Dr. Mpango amesema kwa sasa Rais Samia yuko nje ya Nchi na amemtuma yeye kumwakilisha hapo Arusha kwenye Ibada ya Uaskofu.

Dr. Mpango ameandamana na Makamu Mwenyekiti wa CCM na mbunge wa zamani wa Arusha Komredi Kinana.

Credit: Upendo TV
 
Sunday, Feb 11, 2024​

Rais Samia Hassan ziarani VATICAN na Norway kuanzia Feb 11 hadi 14, 2024​

Waziri Makamba leo tarehe 21 January 2024 kupitia blog ya wizara ya mambo ya nje ametoa taarifa kwa umma kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia pia kufanya Ziara ya Kitaifa Vatican tarehe 11 – 12 Februari, 2024 kufuatia mwaliko wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Papa Francis.

Tarehe 12 February 2024 mheshimiwa Rais Samia Hassan katika msafara wake pia ameamua ataongozana na makundi ya umoja wa Wanawake Wa Katoliki WAWATA, umoja wa Vijana Wakatoliki na Halmashauri ya Walei katika mazungumzo hayo na Papa Francis, ameeleza mheshimiwa waziri January Makamba.

Waziri Makamba ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa Vatican, atakuwa na mazungumzo na Baba Mtakatifu Papa Francis pamoja na Katibu wa Vatican, Mhe. Pietro Parolin.

Uhusiano kati ya Tanzania na Vatican ulianza miaka ya 1960 wakati ambapo Vatican ilianzisha Ubalozi wake hapa nchini.
Tangu wakati huo Vatican kupitia Kanisa Katoliki imekuwa mstari wa mbele katika kujishughulisha na masuala ya kiroho, amani, elimu na program za afya. Kwenye ziara hiyo Mhe. Rais Samia ataongozana na wawakilishi watano wa waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania kutoka kwenye jumuiya mbalimbali za kanisa hilo.

Amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya Kitaifa nchini Norway, tarehe 13-14 Februari 2024 kufuatia mwaliko kutoka kwa Mfalme Herald wa Norway na Malkia Sonja.

Ameongeza kuwa ziara hiyo inafanyika ikiwa ni miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway.
“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atakuwa na mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Norway akiwemo Mfalme Herald. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Rais pia atashiriki Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Norway pamoja na Kongamano la Nishati la Oslo,” alisema Waziri Makamba

Tanzania na Norway zinashirikiana kupitia sekta mbalimbali zikiwemo biashara, uwekezaji, nishati kama mafuta na gesi, elimu na masuala ya kodi na utawala bora.
Kuanzia mwaka 2010, Serikali ya Norway imekua ikishirikiana na Tanzania kwenye programu mbalimbali za maendeleo zilizo gharimu takribani TZS. 300 bilioni. Programu hizo zimesaidia na kuimarisha sekta muhimu za kiuchumi ikiwa ni pamoja na Sekta ya Nishati; Sekta ya Elimu; Sekta ya Mafuta na Gesi; Mpango wa Usimamizi wa Fedha za Umma; programu za Mabadiliko ya Tabianchi; na programu za Usimamizi wa Misitu.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anaandika historia kupitia ziara hii nchini humo kwani mara ya mwisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea nchi hiyo kwa Ziara ya Kitaifa ilikua mwaka 1976

View: https://m.youtube.com/watch?v=RZQVsph0pOU
Source : tovuti: mfatanzania.blogspot.com/2024/01/diplomasia-ya-tanzania-yazidi-kungara.html?m=1
 
Dah acha tanesco watambe tu bila kuwasahau DAWASA!!!

Kwa hiyo atakuwa nje ya nchi mpaka 17 Feb?toka lini hiyo haituhusu ila huko ni nini anasimamia?nimewaza labda yupo kwenye kamati ya kusitisha vita hapo Mashariki ya Kati.
 
Makamu wa Rais Dr Mpango amesema anajua Mchango mkubwa uliotolewa na Mzee Lowassa kwenye Maendeleo ya Arusha

Lowasa alikuwa mchapakazi na Mpenda Maendeleo hivyo nikitua DSM nitakwenda Moja kwa Moja nyumbani kwa familia ya marehemu na nitazifikisha salamu zenu, amesema Dr Mpango

Dr Mpango amesema kwa sasa Rais Samia yuko nje ya Nchi na amemtuma yeye kumwakilisha hapo Arusha kwenye Ibada ya Uaskofu

Dr Mpango ameandamana na Makamu Mwenyekiti wa CCM na mbunge wa zamani wa Arusha Komredi Kinana

Credit: Upendo TV
R.I.P Laigwanan EL
 
Sunday, Feb 11, 2024​

Rais Samia Hassan ziarani VATICAN na Norway kuanzia Feb 11 hadi 14, 2024​

Waziri Makamba leo tarehe 21 January 2024 kupitia blog ya wizara ya mambo ya nje ametoa taarifa kwa umma kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia pia kufanya Ziara ya Kitaifa Vatican tarehe 11 – 12 Februari, 2024 kufuatia mwaliko wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Papa Francis.

Waziri Makamba ameeleza kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa Vatican, atakuwa na mazungumzo na Baba Mtakatifu Papa Francis pamoja na Katibu wa Vatican, Mhe. Pietro Parolin.

Uhusiano kati ya Tanzania na Vatican ulianza miaka ya 1960 wakati ambapo Vatican ilianzisha Ubalozi wake hapa nchini.
Tangu wakati huo Vatican kupitia Kanisa Katoliki imekuwa mstari wa mbele katika kujishughulisha na masuala ya kiroho, amani, elimu na program za afya. Kwenye ziara hiyo Mhe. Rais Samia ataongozana na wawakilishi watano wa waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania kutoka kwenye jumuiya mbalimbali za kanisa hilo.

Amesema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya Kitaifa nchini Norway, tarehe 13-14 Februari 2024 kufuatia mwaliko kutoka kwa Mfalme Herald wa Norway na Malkia Sonja.

Ameongeza kuwa ziara hiyo inafanyika ikiwa ni miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway.
“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atakuwa na mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Norway akiwemo Mfalme Herald. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Rais pia atashiriki Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Norway pamoja na Kongamano la Nishati la Oslo,” alisema Waziri Makamba

Tanzania na Norway zinashirikiana kupitia sekta mbalimbali zikiwemo biashara, uwekezaji, nishati kama mafuta na gesi, elimu na masuala ya kodi na utawala bora.
Kuanzia mwaka 2010, Serikali ya Norway imekua ikishirikiana na Tanzania kwenye programu mbalimbali za maendeleo zilizo gharimu takribani TZS. 300 bilioni. Programu hizo zimesaidia na kuimarisha sekta muhimu za kiuchumi ikiwa ni pamoja na Sekta ya Nishati; Sekta ya Elimu; Sekta ya Mafuta na Gesi; Mpango wa Usimamizi wa Fedha za Umma; programu za Mabadiliko ya Tabianchi; na programu za Usimamizi wa Misitu.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anaandika historia kupitia ziara hii nchini humo kwani mara ya mwisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea nchi hiyo kwa Ziara ya Kitaifa ilikua mwaka 1976
Ni jambo jema
 
Back
Top Bottom