Rais Samia atuma salamu za pole kufuatia kifo cha mzee Kassum

..Al Noor Kassum, akiwa waziri, kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa wizara [jina nimelisahau], waliwezesha vijana wetu kwenda kusoma Uhandisi wa Maji India, kwa udhamini wa nchi moja ya Skandinavia.

..Kuna nchi moja ya Skandinavia ilitoa msaada wa fedha kusomesha wahandisi wa maji wa Tanzania.

..Al Noor Kassum na Katibu Mkuu wakaona fedha hizo zingeweza kusomesha vijana wengi zaidi kama wangekwenda India badala ya Skandinavia.

..Kwa hiyo wakaweza kuwashawishi wafadhili wa Kiskandinavia wadhamini vijana wetu kwenda kusoma India na hilo liliwezesha wahandisi wengi wa maji kupata elimu ya chuo kikuu India.

..Kama unamfahamu Engineer wa Maji aliyehitimu India miaka ya 1980 basi uwezekano mkubwa alidhaminiwa kwa mpango uliowezeshwa na Waziri Al Noor Kassum na Katibu Mkuu wake.
Kama ni ivo Basi alijitahidi Mimi ni mmoja wa wanufaika chuo kinaitwa IIT Roorkee.
 
Kama ni ivo Basi alijitahidi Mimi ni mmoja wa wanufaika chuo kinaitwa IIT Roorkee.

..hongera.

..Roorkee ni moja ya vyuo vikuu vinavyoheshimika sana India.

..kuna jamaa nawafahamu walisomea Engineering Roorkee Univ miaka ya 80.

..nadhani miaka hiyo Roorkee ilikuwa bado haijawa IIT.
 
Back
Top Bottom