Rais Samia atangazie upya suala la Kikokotoo cha Mafao

Huu ni upuuzi, mfanyakazi aruhusiwe kuchukua hadi 80% ya mafao yake kama kiinua mgongo ili akaendelee na uwekezaji ambao utamsaidia kujikwamua badala ya kusubiri pensheni ya kila mwezi ambayo mara nyingi inachelewa............mfanyakazi kafanya kazi ya kulipwa mshahara hadi kastaafu, kwa nini mnalazimisha kumlipa kila mwezi utafikiri bado yupo kazini? wapeni pesa zao zote bhanaa, kama ni ku handle pesa nyingi wana uzoefu mkubwa hadi wamefika umri wa kustaafu. Mnachotakiwa kufanya ni kuwapa elimu ya kuwawezesha kuwa na uwekezaji utakaowapa kipato endelevu..........haya mambo ndo yanafanya watu wanajiondoa kwenye vyama vya wafanyakazi, vinaonekana kama havina msaada wowote.
Tuliamshe tu hakuna namna
 
Wanadai hizo fedha ndizo zinazotekelezea miradi ya ki mkakati. Wasipoifuta sheria hii karma ya Mungu iwe juu ya vichwa vyao na familia zao hadi vizazi vya tatu hadi vya nne.
Kabisa na iwe hivyo maana hii Hata Mungu inamchukiza
 
Wakuu:
✓Ifike mahali tukubaliane kuwa hakuna anayeijua kesho yake.
✓Ifike mahali tukubaliane kuwa kila mtu anazalisha ili ajikwamue kimaisha akiwa bado hai!
✓Ifike mahali tukubaliane vile vile kuwa kuna haja ya kupitia upya suala zima la matumizi ya Kikokotoo kwenye mafao ya wafanyakazi wa nchi hii!
Nashauri lifanyike moja au yote mawili:
1. Mfanyakazi aruhusiwe kuchukua fedha zake kadri itakavyompendeza.
2. Mfanyakazi akopesheke kwenye taasisi za fedha kwa dhamana ya Michango yake kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii.

Wafanyakazi kumbukeni kuwa ajenda hii ni muhimu kwa sasa kuliko mapambio ya kusifu na kuabudu!View attachment 1979524
KIKOKOTOO HICHO KIPYA KIPO KWA AJILI YA KUISAIDIA SERIKALI KUJIKOPESHA KIRAHISI MICHANGO YA MFANYAKAZI HIVYO SIO RAHISI KUKIBADILISHA PIA KUMBUKA MAGUFULI ALIKWISHA SAINI
 
Mimi nilikuwa nina uhakika tangu siku anaapishwa
Hili swala Bulaya na Mdee waliliongelea sana Bungeni lakini mwanasiasa Muhagama alijibu kisiasa zaidi .

Sasa limeibukia tena huku kwa ujumla hali za watu wanaodai zilivyo mbaya walipwe fedha zao mapema wakati wakiwa nguvu za kuwekeza na kuzalisha ili serikali ikusanye kodi zaidi kuliko kukaa madeni ya watu maskini.
Hii inapelekea serikali kuchukiwa bila sababu wanaosababisha chuki ni Nssf wanaoshindwa namna ya kuwahudumia Wateja wao.
 
Mimi kama mimi aldeo nachangia

Nssf wabadilike waje na mtazamo wao kivyao hii itawasaidia kuendesha shirika kwa faida bila changamoto Kama hizi baina ya shirika na NSSF.

Katika kuongelea maslai mapana ya mtanzania huwa linaanza na mtanzania mwenyewe Sasa hili la NSSF wacha tuanzie sie wahanga wa kutokupata pesa zetu bila kujali n kiasi gani na kwa muda gani.

Nimeshajaribu kutafuta namna ya kupata mafao haya nikiwa bado sijafikisha 55yrs lakini imekua ngumu sana nishaenda kuomba kufungua madai ya kulipwa kwa zaid ya mikoa mitatu Yan unazungushwa wee mwishowe wanakwambia andika barua baada ya hapo hutopata jibu kamwe hii ndo tabia ya mameneja Kanda kuanzia Arusha, Kilimanjaro, shinyanga, kinondoni yan wanakupa sababu ambazo n za kitoto sana mfano unaeza ambiwa uende ukafungue madai kwenye tawi lilipokuwa linapokea mchango wako Sasa mwajiri ofisi ipo DSM mwajiriwa kazi n kasulu na hata hajawahi kufika dar sababu HQ ipo dar Basi process zote zinafanyikia dar sasa ukitaka kuchukua pesa zako baada ya kukomeshwa ajira utaanza vizuri mwishoni unaambiwa uende kule ulipokuwa unachangia sasa tangu mwanzo hawakuliona hilo.
Nilishawahi kusafirishwa mikoa miwili tofauti kufuatilia taarifa ya matibabu ya ajali yan wanakuona kabisa unamagongo wanakutuma kama mtoto tena bila huruma alafu Bora hata upate hxo pesa isaidie Ila wap utaambulia kupoteza hata kile ulichokuwa nacho na madeni kipao kwenye hili meneja wa NSSF SHINYANGA mwaka 2020-2021 MUNGU anilipie kwa majibu na dharau ulizonionyeshea akifutiwa na wa Arusha huyu ndo anasimama nje kabisa yan kama umekuja kudai mafao anakurudisha hapo n bora hata akuelekeze uelewe Ila anakufokea kama mtoto huyu ndo alinifanya niende tawi lingine kufungua madai.

SULULISHO LA MADAI BILA SHIRIKA KUTETEREKA

Napendekeza na nilishawaambia baadhi ya watumishi wa NSSF Arusha na shyinyanga kutokana na malalamiko kuwa mengi na msongamano kuwa mkubwa wa maombi pili tunapoelekea watu wengi wanastaafu na kupoteza ajira Basi iwapendeze wake na huu mpango wangu niliouona kuwa n wa kiukombozi na usawa na shirika likawa stable milele kwa hatua hizi mbili.

1. Shirika liendeshwe serious kibiashara kwa maana investment zote walizonazo zifanye kazi kwa lazima na return ya faida ionekane nakila kitega uchumi kioewe target kulingana na Hali halisi ya eneo zaid kibiashara hapa namaanisha. (Majengo ya kibiashara, Viwanda walivyoingia Shea, Nyumba za kuishi wanazojenga na kuuza, hotel walizoingia ubia na baadhi ya miradi au mikopo walifadhili kibiashara ilete +return kwa kila kipindi walichopangiwa.

2. Shirika lipunguze watumishi wasiokuwa na tija utakuta meza moja Kuna watu watatu wote Wana title moja au wanafanya kazi zinazofana hii nimeona NSSF ARUSHA pili wote hao Bora hata upate hata mmoja anachojua kuhusu kazi ya jina lake Yan n zero mfano Kuna dada mmoja yupo ghorofa ya kwanza mwishon wote na bosi wake hawajui formula ya mafao, hawajui benefits za mtu kuwa mwanachama wa hiari Yan wanakuimbia eti utapata matibabu bure na mkopo Sasa nikawauliza mie tayari Nina bima ya afya kutoka jubilee pia ninamausiano mazuri na absa+crdb benki hvyo nakopesheka vizuri kule wakawa hawana majibu wanaanza kupigiana simu eti mie huyu nimemshindwa Yan kifupi NSSF ARUSHA na kwingineko kuna watumishi wanaenda kureport na kusubiri muda wa kazi uishe waende kulala yan hawafanyi chochote na Ni mzigo na hasara kwa shirika.

3. Ofisi zote za NSSF zilizopanga ziondoke maramoja kwani Majengo yao waliojenga yapo wazi. Pia litumie network base ya wateja wake kama mashirika na kampuni kubwa kuwapa nafasi ya kupanga kwani Majengo ya NSSF n mazuri na yanapangishika nashangaa pale Moshi na Arusha Kuna floor zipo wazi.

4. HILI NDO MUHIMU SASA YAANI WATENGEZE VOCHA AMBAZO MWANACHAMA ANAEZA KUUZIA MWANACHAMA MWENZAKE AU MTU MWINGINE KADRI WATAKAVYOONA ITALETA TIJA.

"Hii itaondoa kelele na kuleta tija na ufanisi na kuacha uchumi wa shirika kuwa stable maradufu YAANI mwanachama akiwa anataka kuchukua pesa zake hana haja ya kwenda NSSF kudai pesa yeye anaenda kwenye gulio la hisa za NSSF anauza kwa KADRI ya bei ya soko lilivyo kwakua NSSF tayari inavitega uchumi vingi na vikubwa hvyo wakipatikana watu wenye vichwa vizuri Basi shirika lazima litengeneza faida maradufu kila siku mana zile hisa mfano aldeo michango yake na mafao n 20m na kila hisa moja ya NSSF kiunachama n 50k hvyo nitakuwa na hisa 400 hapa nikiamua kuuza labda hisa 100 au 200 au zote naingia sokoni Yan mnadani huu n mnada wa wanachama ambao wameamua kufanya Biashara ya kuwekeza pesa au kwa mashirika au watu binafsi ambao wanataka kuendelea kuwa na hisa nyingi za SHIRIKA.

Kwaleo naomba niishie hapa Ila kama NSSF mtahitaji zaidi wazo langu nitafuteni niwaongezee ideas pia siku mkiamua kutumia wazo hili msisite kutoa credit kwangu hii itasaidia kuwamotivate wale wenye mawazo chanya kuwa huru kuleta mawazo mazuri ili mnufaike vizuri
Au SAMIA akuteue tu kuwa Mkurugenzi wa NSSF ukanyooshe hili suala.
 
😄😄😅 Anikabidhi shirika kiukweli tuonyeshe kuwa kuna vijana wakiaminiwa nchi inasonga hili mimi nalimudu vizuri sana
Uondoe na mikopo ya bila riba wanayokopeshana wafanyakazi wa mifuko ya jamii na matokeo ni kuwavimbia na kuwaona ndezi wachangiaji.
 
Uondoe na mikopo ya bila riba wanayokopeshana wafanyakazi wa mifuko ya jamii na matokeo ni kuwavimbia na kuwaona ndezi wachangiaji.
Yan shirika linakuwa likijiendesha kibiashara wafanyakazi na wanachama unaweza wapa riba kidogo tofauti na mashirika au Viwanda hvyo ndo itafaa iwe
 
Hili swala Bulaya na Mdee waliliongelea sana Bungeni lakini mwanasiasa Muhagama alijibu kisiasa zaidi .

Sasa limeibukia tena huku kwa ujumla hali za watu wanaodai zilivyo mbaya walipwe fedha zao mapema wakati wakiwa nguvu za kuwekeza na kuzalisha ili serikali ikusanye kodi zaidi kuliko kukaa madeni ya watu maskini.
Hii inapelekea serikali kuchukiwa bila sababu wanaosababisha chuki ni Nssf wanaoshindwa namna ya kuwahudumia Wateja wao.
 
KIKOKOTOO HICHO KIPYA KIPO KWA AJILI YA KUISAIDIA SERIKALI KUJIKOPESHA KIRAHISI MICHANGO YA MFANYAKAZI HIVYO SIO RAHISI KUKIBADILISHA PIA KUMBUKA MAGUFULI ALIKWISHA SAINI
Wafanyakazi wana nguvu sana!
KIKOKOTOO HICHO KIPYA KIPO KWA AJILI YA KUISAIDIA SERIKALI KUJIKOPESHA KIRAHISI MICHANGO YA MFANYAKAZI HIVYO SIO RAHISI KUKIBADILISHA PIA KUMBUKA MAGUFULI ALIKWISHA SAINI
Kwa hoja zako hizo hizo inabidi hili jambo lipambaniwe na kila mfanyakazi.
Haiwezekani watu wakubali kuishi kwa misingi haramu ya hayati!
Wafanyakazi msikubali kuwa wanyonge! Unyonge ni sifa ya wana ccm!

KIKOKOTOO HICHO KIPYA KIPO KWA AJILI YA KUISAIDIA SERIKALI KUJIKOPESHA KIRAHISI MICHANGO YA MFANYAKAZI HIVYO SIO RAHISI KUKIBADILISHA PIA KUMBUKA MAGUFULI ALIKWISHA SAINI
Kusainiwa si hoja!
 
KIKOKOTOO HICHO KIPYA KIPO KWA AJILI YA KUISAIDIA SERIKALI KUJIKOPESHA KIRAHISI MICHANGO YA MFANYAKAZI HIVYO SIO RAHISI KUKIBADILISHA PIA KUMBUKA MAGUFULI ALIKWISHA SAINI
Tozo za Mafuta huwa zinapitishwa na bunge wakati wa bunge la bajeti, kufutwa kwake ni kwa bunge pia wakati wa kupitisha bajeti nyingine, lakini majuzi hapa tumeambiwa Rais amefuta Tozo 8 za mafuta.

Kama ameweza kufuta kiholela (kwa faidaya wengi) kitu asichokuwa na mamlaka nacho, hawezi shindwa kufuta hii kikokotoo (kwa faida ya wengi). Na pia kwa vile kipo kwenye kanuni na sio sheria mama, mtu sahihi wa kukifuta ni JENISTA, kwa kutoa kanuni mpya yenye kikokotoo cha zamani.
 
Ifutwe hii dhambi kubwa
 
Sheria hii wakati inatangazwa aisee nilikuwa Capripoint Mwanza, nadhani saivi panaitwa Caprikona.. Niliumia sana na kutembea kwa uchungu mkubwa sana mpaka Pasiansi..nakufakamia mafenesi cha ajabu nikaonana na jamaa yangu wa utotoni akiwa kwenye Foreter kali akanishtua, aisee nikiwa nimebeba fenesi niliona aibu sana huku akinitambulisha kwa chenchede wake akidai mimi ndo nilikuwa naongoza Darasani enzi hizo huko Wilaya ya Kishap..

Dah! siku hii sheria ikiondolewa nahisi wafanyakazi wengi hasa wa sekta binafsi watafurahi sana!
Mkuu mbona hata mimi nakula sana fenesi barabarani...ila huwa napaka mafuta ya kula mikononi kwanza!
 
Back
Top Bottom