Kikokotoo cha Mafao bado ni kilio kwa Askari Polisi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
Nini hatima ya kilio cha askari wa Jeshi la Polisi kuhusu kikokotoo? Hili ndilo swali linaloumiza vichwa vya askari polisi wengi hususan wale wanaotarajia kustaafu kuanzia mwakani.

Kikokotoo kwa askari na watumishi wengine wa umma inaonekana kuwa kaa la moto popote kunapokuwa na mikusanyiko ya wafanyakazi, huku wadau wakija na mapendekezo ya kutibu kilio hicho.

Pia kuna dalili kuwa suala la kikokotoo huenda likaibuka wiki ijayo Jijini Mwanza katika maandhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), ambacho wanachama wake pia ni waathirika wa kikokotoo.

Askari waliohojiwa wakiwemo wanaojiandaa kustaafu mwakani, wamehoji busara iliyotumika kuwaondoa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa nini haikutumika kwa askari wa Jeshi la Polisi na Magereza.

Baadhi ya askari waliliitaka Bunge litafakari upya sheria zinazogusa maslahi ya wafanyakazi huku wenye taaluma ya sheria wakisema sheria hizo zina viashiria vya ubaguzi kwa watumishi kwa kuwaweka katika matabaka katika suala la mafao.

Ibara ya 13(2) ya Katiba ya 1977 inasomeka “Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yeyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.

Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi juu ya malalamiko hayo ya askari na wastaafu wa jeshi hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillius Wambura alisema atafutwe, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Misime kwa ufafanuzi.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu, Misime alisema suala la kikokotoo kwa wastaafu lilishatolewa jibu kuwa linafanyiwa kazi na viongozi wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kabla ya kumuuliza IGP Wambura, Mwananchi lilimtafuta, Kamishna wa Polisi wa Kamisheni ya Utawala na Manejimenti ya Rasilimali Watu, Suzan Kaganda aliyesema suala hilo aulizwe msemaji wa jeshi hilo.

Wanachokisema askari Polisi

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, askari Polisi kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mara, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa na Ruvuma, walisema wanatamani kumsikia Rais Samia akisema kitu juu ya kikokotoo kabla ya mwaka mpya 2024.

“Tuko askari nafikiri zaidi ya 1,000 ila sina hakika na idadi, ambao tutastaafu 2024. Sasa wanasema ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji. Tumeona wenzetu waliostaafu walicholipwa. Hakilingani na uzalendo wetu,” alidai askari ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Askari huyo mwenye cheo cha Stesheni Sajini anayefanya kazi Moshi mkoani Kilimanjaro, alisema haikuwa sawa kuweka ubaguzi kwa majeshi katika kikokotoo kati ya Polisi, Magereza, JWTZ na JKT.

“Wenzetu wakistaafu wanalipwa fedha yao yote, sisi tunalipwa asilimia 33 ya michango halafu unaambiwa hizo nyingine wanakutunzia then (halafu) wanakupa pensheni ya kila mwezi ambayo kwa kweli ni ndogo,” alidai askari huyo.

Askari mwingine mwenye cheo cha Inspekta msaidizi mkoani Mara, alisema kikokotoo kinavunja morali ya askari wengi jeshini, lakini kutokana na uendeshaji wa jeshi ulivyo wa amri, hawawezi kugoma au kuandamana.

“Tunaumia moyoni. Tunajiuliza kwa nini Serikali inatufanyia hivi? Kwa mfano askari polisi mwenye cheo cha inspekta aliyehudumu miaka 30 akistaafu analipwa Sh27 milioni kwa mkupuo,” alieleza.

Askari huyo alisema kiwango hicho ni asilimia 33 ya michango yake yote na kiwango kinachobaki hupewa kama pensheni ya kila mwezi ya Sh370,000, kiwango alichodai ni kidogo hasa ukilinganisha na hali ya maisha ya sasa.

“Ukiwa na cheo cha stesheni sajenti kwa muda huo huo kazini ukistaafu unalipwa Sh21 milioni na pensheni ya Sh300,000 kwa mwezi na sajenti Sh18 milioni na pensheni ya Sh260,000 na koplo ni Sh17 milioni na pensheni Sh200,000.”

“Wenzetu JWTZ hawapo katika janga hili. Sasa katiba yetu ya Tanzania ukiisoma ile ibara ya 13 inakataza ubaguzi. Hili linatuumiza na kutuletea msongo wa mawazo,” alisema.

Ofisa wa jeshi hilo mwenye cheo cha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Jijini Dodoma ambaye pia hakutaka kutajwa jina lake alipoulizwa alisema hilo linawagusa hata askari wa vyeo vya juu, ila nidhamu inawazuia kuzungumza.

“Askari wanalia kwa kuumia hata sisi wakubwa tulitakiwa kulia, ila kwa sababu ya viapo vyetu hatuwezi. Ingekuwa kwa ile kanuni ya zamani sajenti angechukua mafao ya Sh40 milioni, lakini sasa analipwa Sh17 milioni nyingine anaacha,”alisema.

“Mifuko ya mafao inabaki na fedha zetu nyingi, halafu wanakuongezea Sh20,000 kwenye pesa yako. Yaani kwa mwezi pesa yangu inazalisha Sh20,000 tu hivi kweli? Ningenunua hati fungani au kuweka fixed deposit ningepata ngapi?”alihoji.

“Naambiwa mwenye cheo cha ACP (Kamishina Msaidizi wa Polisi) ambaye kwa kanuni ya zamani alikuwa anaondoka na kati ya Sh180 milioni na Sh190 milioni sasa anafyekwa analipwa kama Sh90 milioni na pensheni yake Sh1.2 milioni,” alisema.

Ahadi ya Rais Samia

Kilio cha polisi kimeibuka miezi mitatu tangu askari hao wakiwasilishe kwa Rais Suluhu kwa njia ya sanaa ya kibati, alipofungua kikao kazi cha maofisa waandamizi wa Polisi Septemba 4, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni na Inspekta Jenerali wa Polisi, mwimbaji kiongozi wa kikundi cha ngoma alimweleza Rais kabla kikundi chao hakijatoka kuburudisha ana ujumbe mahsusi.

“Mama kikokotoo kiangalie akika kitatuua. Maana wastaafu wengi huko nje wanalia. Hakika uamuzi wako ni wa busara, tunangoja huruma yako utusaidie,” alisema mwimbaji katika hafla iliyofanyika Oysterbay.

Akijibu suala hilo, Rais Samia alisema wanalifanyia kazi.

“Tuko tunakifanyia kazi kuona jinsi ambayo tutaweza kwenda vizuri kwa sababu masuala ya kikokotoo haya si tu matakwa ya Serikali kuja na kikokotoo, ni hali ya uchumi na hali ya mifuko yenu ilivyo,”alisema Rais Samia.

Alisema kwa kuwa kimepigiwa kelele sana, si tu na Jeshi la Polisi, bali na watumishi wengine, wataangalia kwa kuwa siku zote Serikali ni sikivu.

Ripoti ya Tume ya Haki Jinai aliyoiunda chini ya Jaji mkuu mstaafu Othuman Chande ilieleza eneo ambalo limelalamikiwa sana na Polisi na Magereza ni kikokotoo hususan kwa askari wa vyeo vya chini.

Ripoti hiyi ilieleza msingi wa malalamiko hayo ni utaratibu mpya wa kukokotoa mafao ya mkupuo, umeathiri kwa kiasi kikubwa kiwango cha malipo hayo kutokana na malipo yao kuhusisha posho nyingi na umri wa kustaafu kuwa mdogo.

Wanasheria, wadau wafunguka

John Heche, mbunge wa zamani wa Musoma Vijijini alisema ni vizuri kurudi mezani na kuliangalia upya suala hilo, ili liende sambamba na kuwatumia wataalamu sahihi wa masuala ya hifadhi ya jamii hasa wataalamu wa tathmini ya afya ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

Heche alipendekeza kuwepo mafao ya aina mbili, ili kutoa nafasi ya kuchagua kati ya mafao ya mkupuo makubwa au pensheni ya kila mwezi kubwa.

Miezi miwili iliyopita, Mbunge wa Arusha mjini (CCM), Mrisho Gambo alisema moja ya mambo ambayo hayajawahi kueleweka na hayaeleweki ni kikokotoo na kuhoji mwanachama anapata nini mifuko inapokopesha fedha.

“Unajiuliza pesa ni ya kwangu sio ya kwako. Hata ukiniambia unanihifadhia kiasi gani lazima tukubaliane. Yaani huwezi tu kuamua kuwa wewe bwana ukistaafu utachukua asilimia 33 na zingine utaniwekea,” alisema.

Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Bob Wangwe alisema ili mifuko ya hifadhi ya jamii itekeleze majukumu yake, lazima kufanyike marekebisho ya sheria ili kuiondoa Serikali kutumia fedha za mifuko.

Wakili Peter Mshikilwa alisema lawama za kikokotoo zinapaswa kupelekwa kwa Bunge na Serikali kwa kuwa kinachofanyika sasa ni utekelezaji wa kanuni zilizopitishwa.
 
Public relation kati ya police na raia wa kawaida ni very poor, sio rahisi population kutetea jeshi la police, ata wakisema wasipewe mafao yao yote, hamna raia atakae andamana kwa uonevu huo.....why?
 
Pia kuna dalili kuwa suala la kikokotoo huenda likaibuka wiki ijayo Jijini Mwanza katika maandhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), ambacho wanachama wake pia ni waathirika wa kikokotoo.
Mkuu niko Nje ya mada kidogo.

CWT ima miaka 100 yaani Chama cha walimu Tanzania kina Miaka 100?

Miaka ambayo hata Tanzania yenyewe haijafikiisha..
Tanzania Iliundwa mwaka 1964
Ambapo kwa hesabu za Haraka ina miaka 59
Then hiyo miaka 41 ilikuwaje.....

Ningekubaliana na Watu kama Tanganyika Medical Council (MCT), Tanganyika Law Society (TLS)...
Kama wangesema Kuwa wao wana miaka zaidi ya 100 ila kwa CWT nahitaji mtu kunishawishi vizuri
 
Sasa matatizo ni yale yale, hao watumishi una wa ona ni wasomi lakini ni wajinga kupitiliza, wakipewa pesa kunywa pombe kuoa vitoto vidogo kununua gari za kutembelea sio biashara, ni kero kwa jamii.
Mkuu Utajisikiaje kama wewe serving yako siku umeenda kuchukua pale NBC,CRDB,NMB Au benki yoyote wakwambie kwamba..
"Tunakupa kiasi hiki tu kingine tunakutunzia"
"Na utaruhusiwa kuchukua kiasi hiki tu kila mwezi "

Mkuu sidhani kama tumefikia hatua ya kuingilia Uhuru wa Matumizi ya pesa ya Mtu...

As far as katiba Inavyosema..

23.- (1) Kila Mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na kiasi na sifa za kazi wanazozifanya.

(2) Kila Mtu anayefanya kazi anastahili kupata malipo ya haki.

24.-(1) Kila Mtu anayo haki ya kumiliki mali, na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya
(1), ni marufuku kwa mtu yeyote kunyang’anywa mali yake kwa madhumuni ya kuitaifisha au madhumuni mengineyo bila ya idhini ya sheria ambayo inaweka masharti ya kutoa fidia inayostahili.
 
Inauma sana, sawa ila hao watu hawana ushirikiano na jamii zingine hasa kutatua kero za wananchi hasa wakipata hizo kazi za ummah wana ona wemewin maisha kumbe wakistaafu wanakufa kama masikini, ukiwakuta makazini ofisi za ummah wanaringa sanaa hawaheshimu muda wetu, ebu wateseke tu mbwa hizo .
 
Nini hatima ya kilio cha askari wa Jeshi la Polisi kuhusu kikokotoo? Hili ndilo swali linaloumiza vichwa vya askari polisi wengi hususan wale wanaotarajia kustaafu kuanzia mwakani.

Kikokotoo kwa askari na watumishi wengine wa umma inaonekana kuwa kaa la moto popote kunapokuwa na mikusanyiko ya wafanyakazi, huku wadau wakija na mapendekezo ya kutibu kilio hicho.

Pia kuna dalili kuwa suala la kikokotoo huenda likaibuka wiki ijayo Jijini Mwanza katika maandhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), ambacho wanachama wake pia ni waathirika wa kikokotoo.

Askari waliohojiwa wakiwemo wanaojiandaa kustaafu mwakani, wamehoji busara iliyotumika kuwaondoa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa nini haikutumika kwa askari wa Jeshi la Polisi na Magereza.

Baadhi ya askari waliliitaka Bunge litafakari upya sheria zinazogusa maslahi ya wafanyakazi huku wenye taaluma ya sheria wakisema sheria hizo zina viashiria vya ubaguzi kwa watumishi kwa kuwaweka katika matabaka katika suala la mafao.

Ibara ya 13(2) ya Katiba ya 1977 inasomeka “Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yeyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.

Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi juu ya malalamiko hayo ya askari na wastaafu wa jeshi hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillius Wambura alisema atafutwe, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Misime kwa ufafanuzi.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu, Misime alisema suala la kikokotoo kwa wastaafu lilishatolewa jibu kuwa linafanyiwa kazi na viongozi wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kabla ya kumuuliza IGP Wambura, Mwananchi lilimtafuta, Kamishna wa Polisi wa Kamisheni ya Utawala na Manejimenti ya Rasilimali Watu, Suzan Kaganda aliyesema suala hilo aulizwe msemaji wa jeshi hilo.

Wanachokisema askari Polisi

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, askari Polisi kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Mara, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa na Ruvuma, walisema wanatamani kumsikia Rais Samia akisema kitu juu ya kikokotoo kabla ya mwaka mpya 2024.

“Tuko askari nafikiri zaidi ya 1,000 ila sina hakika na idadi, ambao tutastaafu 2024. Sasa wanasema ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji. Tumeona wenzetu waliostaafu walicholipwa. Hakilingani na uzalendo wetu,” alidai askari ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Askari huyo mwenye cheo cha Stesheni Sajini anayefanya kazi Moshi mkoani Kilimanjaro, alisema haikuwa sawa kuweka ubaguzi kwa majeshi katika kikokotoo kati ya Polisi, Magereza, JWTZ na JKT.

“Wenzetu wakistaafu wanalipwa fedha yao yote, sisi tunalipwa asilimia 33 ya michango halafu unaambiwa hizo nyingine wanakutunzia then (halafu) wanakupa pensheni ya kila mwezi ambayo kwa kweli ni ndogo,” alidai askari huyo.

Askari mwingine mwenye cheo cha Inspekta msaidizi mkoani Mara, alisema kikokotoo kinavunja morali ya askari wengi jeshini, lakini kutokana na uendeshaji wa jeshi ulivyo wa amri, hawawezi kugoma au kuandamana.

“Tunaumia moyoni. Tunajiuliza kwa nini Serikali inatufanyia hivi? Kwa mfano askari polisi mwenye cheo cha inspekta aliyehudumu miaka 30 akistaafu analipwa Sh27 milioni kwa mkupuo,” alieleza.

Askari huyo alisema kiwango hicho ni asilimia 33 ya michango yake yote na kiwango kinachobaki hupewa kama pensheni ya kila mwezi ya Sh370,000, kiwango alichodai ni kidogo hasa ukilinganisha na hali ya maisha ya sasa.

“Ukiwa na cheo cha stesheni sajenti kwa muda huo huo kazini ukistaafu unalipwa Sh21 milioni na pensheni ya Sh300,000 kwa mwezi na sajenti Sh18 milioni na pensheni ya Sh260,000 na koplo ni Sh17 milioni na pensheni Sh200,000.”

“Wenzetu JWTZ hawapo katika janga hili. Sasa katiba yetu ya Tanzania ukiisoma ile ibara ya 13 inakataza ubaguzi. Hili linatuumiza na kutuletea msongo wa mawazo,” alisema.

Ofisa wa jeshi hilo mwenye cheo cha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Jijini Dodoma ambaye pia hakutaka kutajwa jina lake alipoulizwa alisema hilo linawagusa hata askari wa vyeo vya juu, ila nidhamu inawazuia kuzungumza.

“Askari wanalia kwa kuumia hata sisi wakubwa tulitakiwa kulia, ila kwa sababu ya viapo vyetu hatuwezi. Ingekuwa kwa ile kanuni ya zamani sajenti angechukua mafao ya Sh40 milioni, lakini sasa analipwa Sh17 milioni nyingine anaacha,”alisema.

“Mifuko ya mafao inabaki na fedha zetu nyingi, halafu wanakuongezea Sh20,000 kwenye pesa yako. Yaani kwa mwezi pesa yangu inazalisha Sh20,000 tu hivi kweli? Ningenunua hati fungani au kuweka fixed deposit ningepata ngapi?”alihoji.

“Naambiwa mwenye cheo cha ACP (Kamishina Msaidizi wa Polisi) ambaye kwa kanuni ya zamani alikuwa anaondoka na kati ya Sh180 milioni na Sh190 milioni sasa anafyekwa analipwa kama Sh90 milioni na pensheni yake Sh1.2 milioni,” alisema.

Ahadi ya Rais Samia

Kilio cha polisi kimeibuka miezi mitatu tangu askari hao wakiwasilishe kwa Rais Suluhu kwa njia ya sanaa ya kibati, alipofungua kikao kazi cha maofisa waandamizi wa Polisi Septemba 4, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni na Inspekta Jenerali wa Polisi, mwimbaji kiongozi wa kikundi cha ngoma alimweleza Rais kabla kikundi chao hakijatoka kuburudisha ana ujumbe mahsusi.

“Mama kikokotoo kiangalie akika kitatuua. Maana wastaafu wengi huko nje wanalia. Hakika uamuzi wako ni wa busara, tunangoja huruma yako utusaidie,” alisema mwimbaji katika hafla iliyofanyika Oysterbay.

Akijibu suala hilo, Rais Samia alisema wanalifanyia kazi.

“Tuko tunakifanyia kazi kuona jinsi ambayo tutaweza kwenda vizuri kwa sababu masuala ya kikokotoo haya si tu matakwa ya Serikali kuja na kikokotoo, ni hali ya uchumi na hali ya mifuko yenu ilivyo,”alisema Rais Samia.

Alisema kwa kuwa kimepigiwa kelele sana, si tu na Jeshi la Polisi, bali na watumishi wengine, wataangalia kwa kuwa siku zote Serikali ni sikivu.

Ripoti ya Tume ya Haki Jinai aliyoiunda chini ya Jaji mkuu mstaafu Othuman Chande ilieleza eneo ambalo limelalamikiwa sana na Polisi na Magereza ni kikokotoo hususan kwa askari wa vyeo vya chini.

Ripoti hiyi ilieleza msingi wa malalamiko hayo ni utaratibu mpya wa kukokotoa mafao ya mkupuo, umeathiri kwa kiasi kikubwa kiwango cha malipo hayo kutokana na malipo yao kuhusisha posho nyingi na umri wa kustaafu kuwa mdogo.

Wanasheria, wadau wafunguka

John Heche, mbunge wa zamani wa Musoma Vijijini alisema ni vizuri kurudi mezani na kuliangalia upya suala hilo, ili liende sambamba na kuwatumia wataalamu sahihi wa masuala ya hifadhi ya jamii hasa wataalamu wa tathmini ya afya ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

Heche alipendekeza kuwepo mafao ya aina mbili, ili kutoa nafasi ya kuchagua kati ya mafao ya mkupuo makubwa au pensheni ya kila mwezi kubwa.

Miezi miwili iliyopita, Mbunge wa Arusha mjini (CCM), Mrisho Gambo alisema moja ya mambo ambayo hayajawahi kueleweka na hayaeleweki ni kikokotoo na kuhoji mwanachama anapata nini mifuko inapokopesha fedha.

“Unajiuliza pesa ni ya kwangu sio ya kwako. Hata ukiniambia unanihifadhia kiasi gani lazima tukubaliane. Yaani huwezi tu kuamua kuwa wewe bwana ukistaafu utachukua asilimia 33 na zingine utaniwekea,” alisema.

Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Bob Wangwe alisema ili mifuko ya hifadhi ya jamii itekeleze majukumu yake, lazima kufanyike marekebisho ya sheria ili kuiondoa Serikali kutumia fedha za mifuko.

Wakili Peter Mshikilwa alisema lawama za kikokotoo zinapaswa kupelekwa kwa Bunge na Serikali kwa kuwa kinachofanyika sasa ni utekelezaji wa kanuni zilizopitishwa.
Hao hawana haja ya pensheni, wanaila barabarani, wanadhulumu haki , wanakula rushwa kama haki yao. Kimsingi hawatakiwi kupewa ata shilingi kumi.
 
Mkuu niko Nje ya mada kidogo...
CWT ima miaka 100 yaani Chama cha walimu Tanzania kina Miaka 100...?

Miaka ambayo hata Tanzania yenyewe haijafikiisha..
Tanzania Iliundwa mwaka 1964
Ambapo kwa hesabu za Haraka ina miaka 59..
Then hiyo miaka 41 ilikuwaje.....

Ningekubaliana na Watu kama Tanganyika Medical Council (MCT), Tanganyika Law Society (TLS)...
Kama wangesema Kuwa wao wana miaka zaidi ya 100 ila kwa CWT nahitaji mtu kunishawishi vizuri
Cwt imeanzishwa 1993 ina miaka 30 P
 
Back
Top Bottom