Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,834
- 18,835
Mahojiano ya jana ya Rais Samia na Gazeti la New York Times alinukuliwa akisema alipata wakati mgumu kufanya kazi na Hayati Magufuli kutokana na msimamo wa Magufuli juu ya Covid-19.
Japokuwa simkubali Magufuli, lakini hii kauli haijakaa sawa, lakini nina uhakika Rais Samia hakudhamiria kusema hivyo, bali aliyekuwa akimhoji ndio alimbana na kulazimisha kusema hivyo.
Kwa wanaoangalia mahojiano ya viongozi na waandishi wa habari wa nchi za 'mbele' wanajua jinsi waandishi hao wanavyokuwa aggressive, mnakumbuka Tundu Lissu mwenyewe alivyobanwa na mwandishi wa BBC hadi kujikuta ametamka atawapa mashoga haki zao...! Baadae akaja kukana hakumaanisha hivyo, ila sikumlaumu maana unabanwa kwelikweli.
Sasa kwa mtu kama Rais ambaye ana wasaidizi wengi smart walitakiwa ku-anticipate maswali ambayo angeulizwa Rais, na Rais angekua namna ya kuyajibu kabla, kuna maswali mengine unaya-dodge tu badala ya kutoa majibu direct ambayo yataleta utata, ndivyo wanasiasa hufanya.
Wasimuache kama anaenda kuhojiwa TBC.
Nadhani hili halitajirudia tena.