Rais Samia anachukua sifa ya kuwa Rais bora wa mudawote katika uwekezaji wa Afya

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Mnyonge mnyongeni ila sifa yake muachieni.

Sisi waswahilli tunatumia msemo huu kumsemea asiyependa kujikweza.

Kabla ya kuingia katika madaraka ya Urais mhe.Samia Suluhu Hassan amekuwa ni muumini wa kuigwa na kutajwa kama mfano kati ya Viongozi wachache nchini waliotoa kipaumbele kwa vitendo kwa sekta ya Afya.
Ukiongelea kimahsusi Rais Samia amefanya mengi katika sekta ya Afya hususani afya ya uzazi ,wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

Kipekee kama mdau wa afya nitaje machache na muhimu aliyoweza kuyatolea maamuzi na msisitizo.

1-Kampeni ya kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga...Jiongeze tuwavushe salama.

2-Hamasa na ufuatiliaji katika suala la lishe

3-Maamuzi Magumu yatakayorejewa ya kuanzisha tozo iliyojenga vituo vya afya katika kila tarafa na kata zenye jografia ya kimkakati.

4-Maamuzi kuntu ya kupeleka fedha za uviko 19 katika sekta ya afya na maji kwa minajili ya afya kinga na tiba.

5-Sambamba na namba 4 hapo juu ni ujenzi wa miundombinu ya huduma za dharura na mahututi (EMDs na ICUs)katika hospitali za mikoa na wilaya.

6-Ajira ya watumishi wengi wa afya kuliko mtangulizi yoyote kabla yake.

7-Ununuzi wa vifaa tiba muhimu na vya kipekee katika hospitali ngazi ya afya ya msingi na hospitali za rufaa

8-Uboreshaji wa utendaji kazi wa MSD uliombatana na upelekaji wa fedha za dawa /vifaa tiba kwa wakati MSD

9-JARIBIO MAHSUSI LA KUTAKA KUWA NA SERA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE(Japo wizara na wabunge hawakulitendea haki).

10-Kutumia diplomasia na weledi wake wa NGOs kuhakikisha uwezeshaji katika sekta ya afya unakuwa mkubwa na rahisi.

Nimetaja machache na ya kipekee ili umma ujionee na kuweka kumbukumbu.

MAONI NA OMBI
-Bado Wizara zinazohusika na Afya hazijajipanga ipasavyo katika kutafsiri dhamira ya mhe. Rais...yaani bado zipo kwenye mvutano usio kuwa na tija kwa jamii.

Hapa kuna uhitaji wa kuwaweka sawa wizara mtambuka zinazogusa afya ili kuona tija ya maamuzi ya Mhe.Rais.
-Asichoke kuwekeza kwenye Afya kwani bado ni adui miongoni mwa maadui watatu wa Taifa.

-Mhe.Rais aitishe wasaidizi wake wote ikiwemo wale waliopo katika ngazi za chini wampe strategies za kuboresha Maswala ya Afya hususani kwa jamii iliyoko chini kabisa kiuchumi ,kielimu,kiutawala na kiujitaji.

MWISHO
Pongezi nyingi kwako Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa hili na Mungu atakulipa.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
 
Shida huwa mnampa sifa ambazo siyo uhalisia, afya si majengo pekee, hakuna staff wala vifaa tiba, dawa ndiyo usiseme kabisa, labda wewe unatibiwa Muhimbili mwenzetu, nenda pembezoni hali ni mbaya haswa kuliko unavyodhani.
 
Kama hayo unayoyasema ni kweli viongozi wote wakiumwa hakuna kutibiwa nje, au serikali ifute vibali vya matibabu nje ya nchi
 
Kwenye siasa huwa hivi

IMG_20231028_215416.png
 
Umewahi kunisoma kwenye threads zangu marangapi??



Huwa si-comment kama chawa...nifuatilie
Ulipotea sana mjini... naona majeraha yanapona nyoka mnaanza kutoka mapangoni... usifanye mchezo na njaa. Kukamilisha draft muweke Samia kwa Avatar kabisa.
 
Shida huwa mnampa sifa ambazo siyo uhalisia, afya si majengo pekee, hakuna staff wala vifaa tiba, dawa ndiyo usiseme kabisa, labda wewe unatibiwa Muhimbili mwenzetu, nenda pembezoni hali ni mbaya haswa kuliko unavyodhani.
Mbona yote nimeyasema hapo juu? Umesoma?
 
Ulipotea sana mjini... naona majeraha yanapona nyoka mnaanza kutoka mapangoni... usifanye mchezo na njaa. Kukamilisha draft muweke Samia kwa Avatar kabisa.
Ni majukumu tu...na ugumu wa access ya JF kama ninavyotaka .
 
Haya mweke Bi Hangaya kwa Avatar! Huyo marehemu kwa sasa ni irrelevant si umeona mwenyewe jasho la meno lilivyo chungu? Msisuse tena mende hawezi ishi mbali na choo.
Kwani aliyemfanya kuwa mgombea mwenza ,makamu na hatimaye Jemedari sio huyu aliopo kwenye avatar??
 
kwani aliyemfanya kuwa mgombea mwenza ,makamu na hatimaye Jemedari sio huyu aliopo kwenye avatar??
Sawa ila ndo hivyo hana relevance kwa maisha ya sasa hata wewe unalijua hilo. Si umeonja joto ya jiwe umejionea? Mlileta kiburi mwanzo ila njaa imewaumbua...chawa hawezi ishi mbali. Na jalala au uchafu!
 
Back
Top Bottom