Mbunge Kainja: Bilioni 182 tu Kati ya Bilioni 732 Wizara ya Afya, Fedha Hazipelekwi kwa Wakati

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

MBUNGE JACQUELINE KAINJA: BILIONI 182 TU ZIMETOLEWA KATI YA BILIONI 732 WIZARA YA AFYA, FEDHA HAZIPELEKWI KWA WAKATI

"Nampongeza sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha Wizara ya Afya na sekta inafanya kazi kwa ufasaha kwa maslahi mapana ya wananchi wa Tanzania hususani wananchi wa pembezoni na Vijijini" - Mhe. Jacqueline Kainja Andrew, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora

"Taarifa ya Kamati imeonyesha kuna changamoto ya fedha za bajeti zilizotengwa kwa mwaka wa fedha 2023-2024. Sasa ni mwezi wa saba kwa Serikali, fedha zilizotengwa ni Bilioni 732, kiasi kilichokwenda ni Bilioni 187 sawa na asilimia 26, asilimia 74 tutazikamilsha kwa muda gani? Napata ukakasi sana juu ya sekta ya Afya" - Mhe. Jacqueline Kainja Andrew, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora

"Niombe Serikali, fedha tulizopitisha kwenye Bunge ziwe zinatoka kwa wakati ili Mipango ambayo tumesomewa na tukaweza kuipitisha ziwe zinatolewa kwa wakati, vinginevyo hatuna sababu ya kupitisha Bilioni 732 wakati uwezo huo hatuna" - Mhe. Jacqueline Kainja Andrew, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora

"Wananchi wana changamoto, tumekuwa na majengo mazuri, Zahanati nzuri, Vituo vya Afya vimejengwa kwa wingi lakini bado tuna changamoto sana upande wa huduma za afya lakini Changamoto kubwa ni hii ya fedha haziendi kwa wakati" - Mhe. Jacqueline Kainja Andrew, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora

"Medical Store Department (MSD) ni kitovu na kiini cha Wizara ya Afya na sekta ya Afya kwa ujumla lakini bado wana changamoto, uwezo wao ni mdogo sana kuweza kukidhi haja ya huduma ya Afya hususani kwa Serikali na Mashirika binafsi (Hospitali binafsi)" - Mhe. Jacqueline Kainja Andrew, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora

"MSD wakiwa na Bilioni 561 wana uwezo wa kujiendesha vizuri. MSD tumeipa jukumu la kuwa na viwanda vya kuzalisha vifaa tiba. Ili MSD iweze kusambaza dawa na vifaa tiba kuanzia Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya, Mikoa, Kanda na Taifa tunahitaji kuweka nguvu" - Mhe. Jacqueline Kainja Andrew, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora

WhatsApp Image 2024-02-14 at 11.34.32(1).jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom