Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi,

Kwa Maslahi ya Taifa kwenye Nipashe ya leo 5/02/2023

Screen Shot 2023-02-05 at 5.01.56 PM.png
Screen Shot 2023-02-05 at 5.02.21 PM.png

Makala ya leo, ni kuhusu haki za binaadamu, na kwa wale wenye kumbukumbu mzuri ya safu hii, makala za mwanzo kabisa zilikuwa ni makala mfullulizo za “Kilio Cha Haki” ambazo nilizungumzia sana haki jinai.
  1. Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?. Hoja hii imejibiwa kwa vitendo na matokeo yameonekana msikilize Rais Samia akizungumzia matokeo hayo
  2. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  3. Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…
  4. Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?
  5. Pongezi kwa DPP Mpya. Kama itampendeza, aanze kwa kutumia Nolle, kusafisha Uchafu wote wa mtangulizi wake...

Mtu unapozungumzia haki jinai namna hii, kisha ukasikia Rais ameunda timu kuangalia haki jinai, iwe makala zako zilichangia au hazikuchangia, haijalishi, lakini kitendo cha kukizungumza kitu kisha kikafanyiwa kazi ni faraja tosha kwako mwandishi.
  1. Rais Samia ana nia njema na ya dhati kwa kauli thabiti na matendo, Watanzania wapate haki, ila imetokea Watanzania hawajui haki zao!. Je tumsaidie Rais Samia na kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au tuwaachie wenyewe?.
  2. Katiba japo ni kakitabu kadogo ka kurasa 143 tuu, lakini kukaelewa ni shughuli nzito!, ili Watanzania waielelewe katiba, kunatakiwa kufanyika kazi kweli kweli ya uelimishaji umma kuhusu Katiba, sheria na haki.
  3. Tanzania japo tuna wanasheria wengi ambao ni manguli wabobezi na wabobevu wa sheria, lakini wengi hawaijui katiba!.
  4. Serikali tunawasheria wengi manguli wabobezi na wabobevu wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa serikali ambao walipaswa kuijua katiba vilivyo lakini wengi wao, hawaijui katiba, ndio maana serikali inaweza kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba.
  5. Bunge letu nalo ambalo limeshehenezwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, lakini wametunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, hivyo Bunge letu na wabunge wetu nao hawaijui katiba kikamilifu.
  6. Mahakama ndio mhimili pekee ambao angalau angalau unaijua Katiba na kuliambia Bunge na Serikali kuwa sheria fulani ni batili kwasababu iko kinyume cha katiba, ila very unfortunately Mahakama haina meno, badala ya kubatilisha sheria batili, ndio kwanza inayarudishia yale yale majinga yaliyotunga sheria batili ndio yaibadilishe!. Hivyo mahakama kwenye kuitekeleza katiba nayo inashikwa na kigugumizi!.
  7. Lakini huku mitaani kuna wanasheshia wa kawaida tuu na taasisi za kisheria, wanaweza kabisa kusaidia kuelimisha umma elimu ya katiba sheria na haki, ili kumuwezesha Rais Samia kutimiza azma yake ya kutaka Watanzania kutendewa haki ni lazima kwanza hawa Watanzania wazijue haki zao.
  8. Hivyo hizi kauli dhabiti za Rais Rais Samia katika utoaji haki, nimeanza kuzifuatilia kwa muda mrefu, na wiki hii amezitoa tena katika matukio makubwa mawili, tukio la kwanza ni siku ya uzinduzi wa Tume ya Haki Jinai jijini Dodoma siku ya Jumatatu iliyopita ya tarehe 30 January na kesho yake tarehe mosi February kwenye Siku ya Sheria jijini Dodoma.
  9. Kwenye utetezi wa haki nchini Tanzania, tukubali tukatae, Rais Samia ana nia njema na ya dhati ya kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki kwenye vyombo vya utoaji haki, na moja ya udhaifu mkubwa katika utoaji haki Tanzania, ni Watanzania, hawazijui haki zao!.
  10. Haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki ni stahili na stahiki inayopaswa kutolewa bila wewe kuiomba, na ikitokea haki haikutolewa au haikutendeka, haki haiombwi, bali inapaswa kudaiwa, sasa ukiwa mtu hujui haki yako, huwezi kudai kitu usichokijua!
  11. Hiki kitu cha Watanzania kutokujua haki zao, nimesikia tena wiki hii, Rais Samia, akirudia kulisema jambo hili, kwenye kilele cha siku ya sheria iliyoadhimishwa kitaifa uwanja wa Chinangali, jijini Dodoma.
  12. Rais Samia, alisema mambo mengi makubwa mazuri katika utoaji haki nchini Tanzania, kubwa nililo ondoka nalo mimi leo katika makala hii ni hili la Watanzania hawajui haki zao!.
  13. Kwenye hili, Rais Samia amesema, na naomba nimnukuu “Wanasema, kuna msemo maarufu kwamba haki hupewi mkononi, lazima uitafute, lakini katika kutafuta haki kuna ujuzi, wananchi wetu wengi hawana ujuzi wa kutafuta haki zao kwa hiyo tuwasaidie kutafuta au kupata haki zao” mwisho wa kunukuu.
  14. Hii sii mara ya kwanza kwa Rais Samia kuzungumzia changamoto ya haki kwa Watanzania wengi wasiojua haki zao, mwaka jana siku maadhimisho ya miaka 10 ya taasisi ya mtandao wa watetezi wa haki za binaadam, THRDC inayoongozwa na mwanasheria, Onesmo Ole Ngurumwa.
  15. Rais Samia alisema, “Mtetezi mkubwa wa haki za binaadamu ndani ya Tanzania ni katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo serikali ndiyo inaitekeleza, ndio sheria mama ambayo haki zote za binadamu wanaoishi Tanzania”.
  16. Rais Samia anaendelea, “swala langu kwenu ni “jee hawa wanadamu tunao watetea, wanaijua hiyo katiba?, na nataka niache kazi kwenu katika eneo la elimu kwa umma, muifanye kazi hii ya kuwaelekeza watu waijue katiba yao, kwasababu wanapodai haki, lazima wajue na wajibu wao, haki ziko kwenye katiba na wajibu uko kwenye katiba wakielekezwa vizuri wataujua na wajibu wao nini kikatiba”, mwisho wa kunukuu. Msikilize Rais Samia mwenyewe
  17. Hivyo hiki ambacho makala hizi zinafanya, kuwaelimisha Watanzania kuhusu haki zao na katiba yao, ni kuwasaidia Watanzania, kulisaidia taifa, na kumsaidia Samia kutimiza nia Njema yake.
  18. Hivyo natoa wito kwa wanasheria kote nchini, haijalishi wewe ni nani kuanzia JM, majaji, mahakimu, mawakili na wasaidizi wa sheria, na bila kujali uko wapi ni mahakamani, serikalini, taasisi za umma, mashirika au wanasheria binafsi, tukiwemo sisi mawakili, sote tumuunge mkono Rais Samia katika kutimiza azma njema ya Rais Samia, kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki.
  19. Tume hiyo ya haki jinai inayoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande, akisaidiawa na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, ameipa tume hii miezi 4 kuangalia mifumo ya utendaji wa taasisi zote za utoaji haki na kuahidi kuyafanyia kazi matokea ya Tume hiyo,
  20. Yakiwemo lile “zumari” fulani ambalo Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma, alilizungumzia kuhusu zumari hilo lililopigwa kutokea Zanzibar, mlio wake ufike na huku bara,
  21. Rais Samia amesisitiza, kwa vile na yeye ametokea Zanzibar, “Lile zumari litalia, na mimi ni Mpemba, najua sana kupuliza zumari, kwa lile zumari litapulizwa, nitakapo pokea taarifa ya tume, na kusema ndio, mama puliza zumari, nitakwenda kufanya hivyo”,
  22. Hivyo sasa taasisi za haki serikali, pingeni kongole sana kwa Rais Samia, kusikia kilio chenu kilichowasilishwa kwa Rais Samia, na Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, sasa kaeni mkao wa kula!.
  23. Kauli za vingozi wa kisiasa zinazotolewa kwenye hotuba, ziko za aina mbili, kwanza kiongozi anaandikiwa hotuba, kisha anapewa kuipitia, katika kuipitia huko, huongeza yale yak wake ya moyoni ambayo hakuandikiwa, na pili inawezekana hayo aliyoandikiwa, akakubaliana nayo na kuyangiza mayoni kwake hivyo akihutubia yanakuwa ni ya kwake.
  24. Sisi wasikilizaji wa hotuba za viongozi, pia tuko wa aina mbalimbali, kuna baadhi yetu tumejaaliwa uwezo wa ziada, unaposikiliza hotuba ya kiongozi, unakuwa na jicho la rohoni na sikio la ndani, ambapo kiongozi akisoma hotuba aliyoandikiwa, lakini anayoyasoma hayatoki moyoni kwake, baadhi yetu tunajua!.
  25. Kiongozi anayesoma hotuba aliyoandikiwa, huku hayo anayoyasema, hayatoki moyoni, bali yanatoka mdomoni tuu, wenzetu wazungu wanaita kwa Kiingereza, “paying lip services”, kuna wanasiasa wengi wanatoa hotuba za kuandikiwa, au hata bila kuandikiwa, bali wanasema kile kitu watu wanachotaka kusikia, lakini hakitoki moyoni mwao!.
  26. Ndio maana kwenye mikutano mingi ya kampeni, wanasiasa, wanaahidi vitu vingi, vingine ni vya uongo, au hata vya kweli lakini havitekelezwi!.
  27. Mimi nikimuangalia Rais Samia, na kusikiliza kauli za Rais Samia katika hili la haki, kusema la ukweli kabisa, Rais Samia, ana nia ya dhati kutoka moyoni mwake kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki.
  28. Kauli za Rais Samia kuhusu haki sio paying lip services, anamaanisha kabisa hicho anachoongea.
  29. Na kuna msemo “haki huinuia taifa”, hivi hiki anachokifanya Rais Samia kwenye utoaji wa haki Tanzania, Rais Samia ataliinua sana Taifa la Tanzania, hivyo atabarikiwa sana, na Tanzania itabarikiwa sana!.

Mungu Mbariki Rais wetu Samia

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Update
Hatimaye usaidizi huu, unakwenda kufanyika, kupitia kipindi cha TV kwenye kituo cha Channel Ten, kila siku za Jumapili Saa 3:00 usiku na marudio kila Jumatano saa 9:30 Alasiri.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=IXfA8sZkNPxpaeZn
Usikose kuangalia!.
P
 
Wanabodi,
Kwa Maslahi ya Taifa kwenye Nipashe ya leo 5/02/2023

Makala ya leo, ni kuhusu haki za binaadamu, na kwa wale wenye kumbukumbu mzuri ya safu hii, makala za mwanzo kabisa zilikuwa ni makala mfullulizo za “Kilio Cha Haki” ambazo nilizungumzia sana haki jinai. Mtu unapozungumzia haki jinai namna hii, kisha ukasikia Rais ameunda timu kuangalia haki jinai, iwe makala zako zilichangia au hazikuchangia, haijalishi, lakini kitendo cha kukizungumza kitu kisha kikafanyiwa kazi ni faraja tosha kwako mwandishi.

Mkuu ninadhani nimekusoma vyema.

Ni bahati mbaya kuwa hii nchi imefikishwa huku tuliko na wanasheria kwa kuendekeza njaa za matumbo yao. Wangapi wanaaminika? Wenyewe kwa wenyewe hawaangushani. Wapi uwakute wakizodoana?

Zingatia, Kabudi wa mchakato wa katiba mpya siyo yule wa awamu ya 5. Mwakyembe wa UDSM siyo huyo wa baada ya kuonja asali. Ni kina Shivji, Siyami, Tiganga, Kidando au yule wa plea bargain au Msando? Listi ni ndefu.

"Wanasheria walio wengi wamekuwa unprincipled" -- na huo ndiyo ulio ukweli.

Nikimrejea rais Samia, ninadhani huyu ni master wa ile art ya kudanganyana. Hayuko tofauti sana na mwamba wa msoga. Ndani moyoni ninadhani ana malengo yake ambayo ni tofauti na yetu. Nisingependa kusema ana nia njema.

Ninadhani Samia ana nia ya kupunguza mashinikizo (pressure) tu Kwa kiasi anachoweza, ila bottom line yeye ni kutaka kubakia madarakani baada ya 2025.

Niliwahi kuandika uzi huu:

Hayupo mwenye kuridhia Katiba Mpya kwenye Mitano yake ya Mwanzo

"Kwa hakika hapa kwetu hayupo mwenye kukubali katiba mpya kwenye awamu yake ya kwanza."

Kulikoni ajiweke kwenye hati hati ya kutorejea kwenye kulamba asali?

Tunayoyaona sasa ni jitihada zake kwa maoni yangu za kupunguza shinikizo tu na kututoa kwenye reli. Habari ya mjini ni Katiba mpya. Huku anakotupeleka ni kujaribu kututoa tu kwenye katiba mpya.

Yote haya anayoongelea ya haki mzizi wake mzima ulikuwa kutokea huko kwenye katiba. Kwanini tusiwekeze nguvu zetu zote kwenye katiba uliko mzizi wote wa fitina, kama nia yake ilikuwa ni njema?

Kwanini tusiende kwenye suluhisho kamili la matatizo yetu badala ya hizi nusu shari?

Tusipokuwa makini atatuweka busy hadi baada ya 2025.

Izingatiwe kwa katiba iliyopo urais kwake post 2025 ni guaranteed.

Habari ndiyo hiyo.
 
Mkuu ninadhani nimekusoma vyema.

Ni bahati mbaya kuwa hii nchi imefikishwa huku tuliko na wanasheria kwa kuendekeza njaa za matumbo yao. Wangapi wanaaminika? Wenyewe kwa wenyewe hawaangushani. Wapi uwakute wakizodoana?

Zingatia, Kabudi wa mchakato wa katiba mpya siyo yule wa awamu ya 5. Mwakyembe wa UDSM siyo huyo wa baada ya kuonja asali. Ni kina Shivji, Siyami, Tiganga, Kidando au yule wa plea bargain au listi ni ndefu.

"Wanasheria walio wengi wamekuwa unprincipled" -- na huo ndiyo ulio ukweli.

Nikimrejea rais Samia, ninadhani huyu ni master wa ile art ya kudanganyana. Hayuko tofauti sana na mwamba wa msoga. Ndani moyoni ninadhani ana malengo yake ambayo ni tofauti na yetu. Nisingependa kusema ana nia njema.

Ninadhani Samia ana nia ya kupunguza mashinikizo (pressure) tu Kwa kiasi anachoweza, ila bottom line yeye ni kutaka kubakia madarakani baada ya 2025.

Niliwahi kuandika uzi huu:

Hayupo mwenye kuridhia Katiba Mpya kwenye Mitano yake ya Mwanzo

"Kwa hakika hapa kwetu hayupo mwenye kukubali katiba mpya kwenye awamu yake ya kwanza."

Kulikoni ajiweke kwenye hati hati ya kutorejea kwenye kulamba asali?

Tunayoyaona sasa ni jitihada zake kwa maoni yangu za kupunguza shinikizo tu na kututoa kwenye reli. Habari ya mjini ni Katiba mpya. Huku anakotupeleka ni kujaribu kututoa tu kwenye katiba mpya.

Yote haya anayoongelea ya haki mzizi wake mzima ulikuwa kutokea huko kwenye katiba. Kwanini tusiwekeze nguvu zetu zote kwenye katiba uliko na mzizi wote wa fitina, kama nia yake ilikuwa ni njema?

Kwanini tusiende kwenye suluhisho kamili la matatizo yetu badala ya hizi nusu shari?

Tusipokuwa makini atatuweka busy hadi baada ya 2025.

Izingatiwe kwa katiba iliyopo urais kwake post 2025 ni guaranteed.

Habari ndiyo hiyo.

Pascal Mayala mwenyewe ni mwanasheria
Tena wakili msomi.
Unavowaponda hao maana yake nae ni “inclusive “
 
Wee mayalla una moyo aisee! Pamoja na kukejeliwa kote Kila siku ..but huchoki!
Wala sio moyo, ni ngozi ngumu tuu!. Licha ya kuandika na kutangaza ndio kazi yangu, I do this for passion just for the love of it, and thanks God sasa pia nimeajiriwa as an official of the court, hivyo kwa mwaka huu sitaishia kuandika tuu na kutangaza tuu, kama nilivyoeleza kwenye salaam zangu za mwaka mpya Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
P
 
Bandiko UCHWARA hili. Kuna haki gani inayoweza kupatikana kupitia katiba ya hovyo namna hii tuliyo nayo? Ninyi CHAWA wake jielekezeni kumkumbusha umuhimu wa kupatikana KATIBA MPYA, ili abakie kwenye historia kama MAMA WA TAIFA
 
Bandiko UCHWARA hili.
Kwa vile humu JF kuna mabadiliko mengi, my advice to you, ni next time ukikutana na bandiko uchwara, save your precious time, don't waste time na uchara jump to mabandiko ya maana kwako!.
Kuna haki gani inayoweza kupatikana kupitia katiba ya hovyo namna hii tuliyo nayo?
Dini zote zinatufunza kuwa na shukrani kwa madogo ili tuweze kupatiwa makubwa!. Ni Katiba hii hii ndio umetupatia kila kitu kilichopo leo ina miaka 46!, tushukuru kwa hiki kidogo kilichopo mkononi ambacho tumekishika halafu ndipo tutafute kikubwa zaidi kizuri zaidi!. Moja shika sii kumi nenda rudi!.
Ninyi CHAWA wake
Mkuu Rashidi Jololo , heshima kitu cha bure, heshimu wote wakubwa na wadogo, sio kila anayempongeza Mama ni chawa!. Japo the dividing line between pongezi za kweli na pongezi za machawa is very thin, tofauti pekee ni kwenye pongezi bonafide genuine mpongezaji atapongeza only pale panapostahili pongezi, na siku mpongezwa huyu huyu akichemsha, anakosolewa!. Machawa kazi yao ni kusifu tuu!. Mimi sio chawa!.
jielekezeni kumkumbusha umuhimu wa kupatikana KATIBA MPYA, ili abakie kwenye historia kama MAMA WA TAIFA
Karibu pande hizi
  1. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  2. Ijue Katiba ya JMT-1: Katiba ni Nini, ya Nani, ya Kazi Gani?. Msemo "Katiba Ndio Kila Kitu" Una Maana Gani?. Katiba Ina Umuhimu Gani?
  3. Katiba ni Sheria Mama. Sheria Yoyote Kinyume na Katiba ni Batili!. Wanasheria Wetu, Waliwezaje Kufanya Madudu Haya Kuchomeka Batili Ndani ya Katiba?!
  4. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
  5. Ajabu Hii ya Haki Iliyotolewa na Ibara Moja ya Katiba, Kuporwa na Ibara Nyingine, Ilifanyika Vipi Huku Tuna Washeria Manguli, Wabobezi na Wabobevu?
  6. Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
  7. Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
  8. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
  9. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  10. Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
Rais Mama Samia anakwenda kutupatia katiba mpya
P
 
Wanabodi,

Kwa Maslahi ya Taifa kwenye Nipashe ya leo 5/02/2023

View attachment 2507414View attachment 2507416
Makala ya leo, ni kuhusu haki za binaadamu, na kwa wale wenye kumbukumbu mzuri ya safu hii, makala za mwanzo kabisa zilikuwa ni makala mfullulizo za “Kilio Cha Haki” ambazo nilizungumzia sana haki jinai.
  1. Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?
  2. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  3. Kumbe DPP kutenda haki kunawezekana! Hongera sana, kazi umeianza vizuri. Sasa haki sio tu inatendeka, inaonekana! Kazi Iendelee…
  4. Ushauri kwa DPP: Kutekeleza nia njema ya Rais Samia, kuona Haki ikitendeka; je, tumchagize DPP kutumia Nolle kufuta kesi zote zinazosuasua?
  5. Pongezi kwa DPP Mpya. Kama itampendeza, aanze kwa kutumia Nolle, kusafisha Uchafu wote wa mtangulizi wake...
Mtu unapozungumzia haki jinai namna hii, kisha ukasikia Rais ameunda timu kuangalia haki jinai, iwe makala zako zilichangia au hazikuchangia, haijalishi, lakini kitendo cha kukizungumza kitu kisha kikafanyiwa kazi ni faraja tosha kwako mwandishi.
  1. Rais Samia ana nia njema na ya dhati kwa kauli thabiti na matendo, Watanzania wapate haki, ila imetokea Watanzania hawajui haki zao!. Je tumsaidie Rais Samia na kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au tuwaachie wenyewe?.
  2. Katiba japo ni kakitabu kadogo ka kurasa 43 tuu, lakini kukaelewa ni shughuli nzito!, ili Watanzania waielelewe katiba, kunatakiwa kufanyika kazi kweli kweli ya uelimishaji umma kuhusu Katiba, sheria na haki.
  3. Tanzania japo tuna wanasheria wengi ambao ni manguli wabobezi na wabobevu wa sheria, lakini wengi hawaijui katiba!.
  4. Serikali tunawasheria wengi manguli wabobezi na wabobevu wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa serikali ambao walipaswa kuijua katiba vilivyo lakini wengi wao, hawaijui katiba, ndio maana serikali inaweza kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba.
  5. Bunge letu nalo ambalo limeshehenezwa na wanasheria manguli wabobezi na wabobevu, lakini wametunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, hivyo Bunge letu na wabunge wetu nao hawaijui katiba kikamilifu.
  6. Mahakama ndio mhimili pekee ambao angalau angalau unaijua Katiba na kuliambia Bunge na Serikali kuwa sheria fulani ni batili kwasababu iko kinyume cha katiba, ila very unfortunately Mahakama haina meno, badala ya kubatilisha sheria batili, ndio kwanza inayarudishia yale yale majinga yaliyotunga sheria batili ndio yaibadilishe!. Hivyo mahakama kwenye kuitekeleza katiba nayo inashikwa na kigugumizi!.
  7. Lakini huku mitaani kuna wanasheshia wa kawaida tuu na taasisi za kisheria, wanaweza kabisa kusaidia kuelimisha umma elimu ya katiba sheria na haki, ili kumuwezesha Rais Samia kutimiza azma yake ya kutaka Watanzania kutendewa haki ni lazima kwanza hawa Watanzania wazijue haki zao.
  8. Hivyo hizi kauli dhabiti za Rais Rais Samia katika utoaji haki, nimeanza kuzifuatilia kwa muda mrefu, na wiki hii amezitoa tena katika matukio makubwa mawili, tukio la kwanza ni siku ya uzinduzi wa Tume ya Haki Jinai jijini Dodoma siku ya Jumatatu iliyopita ya tarehe 30 January na kesho yake tarehe mosi February kwenye Siku ya Sheria jijini Dodoma.
  9. Kwenye utetezi wa haki nchini Tanzania, tukubali tukatae, Rais Samia ana nia njema na ya dhati ya kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki kwenye vyombo vya utoaji haki, na moja ya udhaifu mkubwa katika utoaji haki Tanzania, ni Watanzania, hawazijui haki zao!.
  10. Haki hailetwi kwenye kisahani cha chai, haki ni stahili na stahiki inayopaswa kutolewa bila wewe kuiomba, na ikitokea haki haikutolewa au haikutendeka, haki haiombwi, bali inapaswa kudaiwa, sasa ukiwa mtu hujui haki yako, huwezi kudai kitu usichokijua!
  11. Hiki kitu cha Watanzania kutokujua haki zao, nimesikia tena wiki hii, Rais Samia, akirudia kulisema jambo hili, kwenye kilele cha siku ya sheria iliyoadhimishwa kitaifa uwanja wa Chinangali, jijini Dodoma.
  12. Rais Samia, alisema mambo mengi makubwa mazuri katika utoaji haki nchini Tanzania, kubwa nililo ondoka nalo mimi leo katika makala hii ni hili la Watanzania hawajui haki zao!.
  13. Kwenye hili, Rais Samia amesema, na naomba nimnukuu “Wanasema, kuna msemo maarufu kwamba haki hupewi mkononi, lazima uitafute, lakini katika kutafuta haki kuna ujuzi, wananchi wetu wengi hawana ujuzi wa kutafuta haki zao kwa hiyo tuwasaidie kutafuta au kupata haki zao” mwisho wa kunukuu.
  14. Hii sii mara ya kwanza kwa Rais Samia kuzungumzia changamoto ya haki kwa Watanzania wengi wasiojua haki zao, mwaka jana siku maadhimisho ya miaka 10 ya taasisi ya mtandao wa watetezi wa haki za binaadam, THRDC inayoongozwa na mwanasheria, Onesmo Ole Ngurumwa.
  15. Rais Samia alisema, “Mtetezi mkubwa wa haki za binaadamu ndani ya Tanzania ni katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo serikali ndiyo inaitekeleza, ndio sheria mama ambayo haki zote za binadamu wanaoishi Tanzania”.
  16. Rais Samia anaendelea, “swala langu kwenu ni “jee hawa wanadamu tunao watetea, wanaijua hiyo katiba?, na nataka niache kazi kwenu katika eneo la elimu kwa umma, muifanye kazi hii ya kuwaelekeza watu waijue katiba yao, kwasababu wanapodai haki, lazima wajue na wajibu wao, haki ziko kwenye katiba na wajibu uko kwenye katiba wakielekezwa vizuri wataujua na wajibu wao nini kikatiba”, mwisho wa kunukuu.
  17. Hivyo hiki ambacho makala hizi zinafanya, kuwaelimisha Watanzania kuhusu haki zao na katiba yao, ni kuwasaidia Watanzania, kulisaidia taifa, na kumsaidia Samia kutimiza nia Njema yake.
  18. Hivyo natoa wito kwa wanasheria kote nchini, haijalishi wewe ni nani kuanzia JM, majaji, mahakimu, mawakili na wasaidizi wa sheria, na bila kujali uko wapi ni mahakamani, serikalini, taasisi za umma, mashirika au wanasheria binafsi, tukiwemo sisi mawakili, sote tumuunge mkono Rais Samia katika kutimiza azma njema ya Rais Samia, kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki.
  19. Tume hiyo ya haki jinai inayoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande, akisaidiawa na Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, ameipa tume hii miezi 4 kuangalia mifumo ya utendaji wa taasisi zote za utoaji haki na kuahidi kuyafanyia kazi matokea ya Tume hiyo,
  20. Yakiwemo lile “zumari” fulani ambalo Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma, alilizungumzia kuhusu zumari hilo lililopigwa kutokea Zanzibar, mlio wake ufike na huku bara,
  21. Rais Samia amesisitiza, kwa vile na yeye ametokea Zanzibar, “Lile zumari litalia, na mimi ni Mpemba, najua sana kupuliza zumari, kwa lile zumari litapulizwa, nitakapo pokea taarifa ya tume, na kusema ndio, mama puliza zumari, nitakwenda kufanya hivyo”,
  22. Hivyo sasa taasisi za haki serikali, pingeni kongole sana kwa Rais Samia, kusikia kilio chenu kilichowasilishwa kwa Rais Samia, na Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, sasa kaeni mkao wa kula!.
  23. Kauli za vingozi wa kisiasa zinazotolewa kwenye hotuba, ziko za aina mbili, kwanza kiongozi anaandikiwa hotuba, kisha anapewa kuipitia, katika kuipitia huko, huongeza yale yak wake ya moyoni ambayo hakuandikiwa, na pili inawezekana hayo aliyoandikiwa, akakubaliana nayo na kuyangiza mayoni kwake hivyo akihutubia yanakuwa ni ya kwake.
  24. Sisi wasikilizaji wa hotuba za viongozi, pia tuko wa aina mbalimbali, kuna baadhi yetu tumejaaliwa uwezo wa ziada, unaposikiliza hotuba ya kiongozi, unakuwa na jicho la rohoni na sikio la ndani, ambapo kiongozi akisoma hotuba aliyoandikiwa, lakini anayoyasoma hayatoki moyoni kwake, baadhi yetu tunajua!.
  25. Kiongozi anayesoma hotuba aliyoandikiwa, huku hayo anayoyasema, hayatoki moyoni, bali yanatoka mdomoni tuu, wenzetu wazungu wanaita kwa Kiingereza, “paying lip services”, kuna wanasiasa wengi wanatoa hotuba za kuandikiwa, au hata bila kuandikiwa, bali wanasema kile kitu watu wanachotaka kusikia, lakini hakitoki moyoni mwao!.
  26. Ndio maana kwenye mikutano mingi ya kampeni, wanasiasa, wanaahidi vitu vingi, vingine ni vya uongo, au hata vya kweli lakini havitekelezwi!.
  27. Mimi nikimuangalia Rais Samia, na kusikiliza kauli za Rais Samia katika hili la haki, kusema la ukweli kabisa, Rais Samia, ana nia ya dhati kutoka moyoni mwake kuhakikisha Watanzania wanatendewa haki.
  28. Kauli za Rais Samia kuhusu haki sio paying lip services, anamaanisha kabisa hicho anachoongea.
  29. Na kuna msemo “haki huinuia taifa”, hivi hiki anachokifanya Rais Samia kwenye utoaji wa haki Tanzania, Rais Samia ataliinua sana Taifa la Tanzania, hivyo atabarikiwa sana, na Tanzania itabarikiwa sana!.
Mungu Mbariki Rais wetu Samia

Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Msaidie.
 
Binafsi nina wasiwasi hata Rais mwenyewe unayemsifia kuitoa haki nae haijui hiyo haki, kwani ni kawaida kwa Rais kuwaambia polisi watoe haki kwa watuhumiwa wakiwa vituoni, lakini Rais huyo huyo hukaa kimya pae wapinzani wakinyimwa haki zao na polisi wale wale kwa maslahi ya CCM.

Hili somo lako nakushauri ulitoe kwa wote, japo hata nawe bado nakufanyia uchunguzi, kwani inaweza kabisa, hata wewe unayejiita mwalimu wa haki, bado ukawa huijui hiyo haki yenyewe, hasa nikikumbuka unavyopenda kuwabeba wale wanawake 19 wasio na chama waendelee kuwepo bungeni.

Naona inawezekana tunahitaji kumpata mwalimu wa haki toka nje..
 
Binafsi nina wasiwasi hata Rais mwenyewe unayemsifia kuitoa haki nae haijui hiyo haki, kwani ni kawaida kwa Rais kuwaambia polisi watoe haki kwa watuhumiwa wakiwa vituoni, lakini Rais huyo huyo hukaa kimya pae wapinzani wakinyimwa haki zao na polisi wale wale kwa maslahi ya CCM.
Mkuu denooJ , kuna vitu huvijui kuhusu Wazanzibar na haswa wanawake wa Kizanzibari waliofunzwa wakafunzika!, hawa sio ropo ropo kusema sema kila kitu!.
Tena hata katika mambo yetu yale, kule Zanzibar, wadada wa Bongo ndio hupanga bei na kudai kwanza "nipe changu" ndipo uhudumiwe, lakini mabinti wa Kizanzibari wao wana aibu, hawapangi bei, unahudumiwa tuu na kutoa asante ya chochote ulicho nacho!.

Hivyo lile jicho la Mama Samia, japo linaonekana kama limeregea lakini linaona sana!. Hivyo kuna vitu kibao Mama anaona na kunyamaza lakini vinafanyiwa kazi. Mfano aliona vyote kwenye kesi ya Mbowe, mnaodhania aliyemuachia ni DPP endeleeni kudhani hivyo!. Chadema ilishindwa kufanya vikao vyake vya ndani kwasababu fulani, na mara ghafla ikafanya, aliyewezesha tunamjua kanyamaza!. Alipotoka kuzungumza na Lissu Belgium hakusema kitu bali ghafla Lissu kalipwa haki zake zote!.
Hizi ziara za Mbowe nje ya nchi watu mnaona tuu watu wanasafiri lakini hamjui nani amegharimia!. Usikute hata watu kurejea nchini nauli wamelipiwa!, na fedha za kuzindua mikutano wamefadhiliwa!.
Hili somo lako nakushauri ulitoe kwa wote
Nalitoa kwa wote
japo hata nawe bado nakufanyia uchunguzi, kwani inaweza kabisa, hata wewe unayejiita mwalimu wa haki, bado ukawa huijui hiyo haki yenyewe,
Hakuna mtu yeyote anayejua kila kitu!. Hata mimi hii haki ninayojua ni kama punje ya mchanga au tone tuu la maji ya bahari
hasa nikikumbuka unavyopenda kuwabeba wale wanawake 19 wasio na chama waendelee kuwepo bungeni.
Wale bado ni wanachama wenu halali na wabunge halali wa Bunge la JMT mpaka mahakamani itakapo tamka otherwise.
Naona inawezekana tunahitaji kumpata mwalimu wa haki toka nje..
Naunga mkono hoja.
P
 
Asante kwa andiko lako zuri.
Katika andiko hili kitenzi kikuu ni KUTOJUA, watanzania hatujui, hatujui, hatujui nk.

Nini kimepelekea watanzania wengi kutokujua? Mjadala natamani uanzie huku. Mfumo unaotaka watu wajue unapatikana katika elimu.

Mfumo wetu wa elimu huenda ndio tatizo linalozaa kutokujua maana hata wale waliopaswa wawe wanajua, kwa bahati mbaya hawajui.

Umewataja wanasheria na wasomi mbalimbali ambao nao hawajaonyesha ujuzi uliokusudiwa.

Siamini kama hili ni jambo la makusudi bali ni 'chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna'. Elimu yetu haizai watu wadadisi, wabishi wa hoja, wenye shauku ya jambo jipya, nk.

Imekuwa ni elimu inayozaa waoga na washangiliaji tu na hivyo kupelekea hata wasomi wetu kuangukia humohumo. Wasomi hawawazi kukosoa kisayansi bali kiitikadi.

Najaribu kuwaza kama tunaamanisha kumkomboa kifikra mtanzania kwa elimu tumpayo au ni kumfanya mateka wa matamanio yetu tu kupitia tukiitacho elimu yetu.

Kwa namna gani tunaandaa vijana wakaidi kifikra kwa elimu tuwapayo darasani? Tunawafunza vitabu vyenye maandishi yanayokataa unyonge ila hatutaki wawe mashujaa!

Mashuleni na vyuoni ukipata mwanafunzi mbishi kwa hoja huyo tutamwita 'mpinzani' na bora iishie kuwa mpinzani' tu bali asiyetakiwa!

CAG aliyeondolewa madarakani kinyume na katiba licha ya kwamba alionyesha ufanisi sana ofisini lakini aina yetu ya maisha haikumtaka huyo, ni kwa sababu elimu yetu haitaki ujuzi ukupe uhuru huo.

Nihitimishe kwa kusema kuwa ktk hili huenda huo moyo wa rais ni picha tu ya chakula kitamu kisichoondoa njaa.

Haki ifunzwe kimfumo. Mfumo wetu wa elimu utafsiri kuwa haki ya mtu ni utu wake, kuzumzuilia kwa namna yeyote ni kuwa kinyume na utu hivyo mwenye kuzuia haki huzuia utu pasi kujalisha ni nani katika jamii.

KUPENDA HAKI KUWE TUNDA LITOKANALO NA UJUZI WA NDANI.
Asante.
 
Mkuu denooJ , kuna vitu huvijui kuhusu Wazanzibar na haswa wanawake wa Kizanzibari waliofunzwa wakafunzika!, hawa sio ropo ropo kusema sema kila kitu!. Lile jicho la Mama Samia, japo linaonekana kama limeregea lakini linaona sana!. Hivyo kuna vitu kibao Mama anaona na kunyamaza lakini vinafanyiwa kazi. Mfano aliona vyote kwenye kesi ya Mbowe, mnaodhania aliyemuachia ni DPP endeleeni kudhani hivyo!. Chadema ilishindwa kufanya vikao vyake vya ndani kwasababu fulani, na mara ghafla ikafanya, aliyewezesha tunamjua kanyamaza!. Alipotoka kuzungumza na Lissu Belgium hakusema kitu bali ghafla Lissu kalipwa haki zake zote!.
Hizi ziara za Mbowe nje ya nchi watu mnaona tuu watu wanasafiri lakini hamjui nani amegharimia!. Usikute hata watu kurejea nchini nauli wamelipiwa!, na fedha za kuzindua mikutano wamefadhiliwa!.

Nalitoa kwa wote

Hakuna mtu yeyote anayejua kila kitu!. Hata mimi hii haki ninayojua ni kama punje ya mchanga au tone tuu la maji ya bahari

Wale bado ni wanachama wenu halali na wabunge halali wa Bunge la JMT mpaka mahakamani itakapo tamka otherwise.

Naunga mkono hoja.
P
- Lissu kulipwa haki zake ni stahili yake, hilo halihitaji huruma ya jicho la kizanzibari, lakini la Mbowe kugharimiwa safari za nje bado nataka ushahidi, na Lissu kurudi nchini nae nataka ushahidi wa kulipiwa nauli, naona umeshaanza kuingiza maslahi ya CCM yako hapa.

- Hapo ulipolazimisha wale wanawake 19 waendelee kuwa wanachama halali wa Chadema ndio imebidi nicheke tu, naamini haya yatakuwa maagizo mmepewa makada wote ili kukibeba chama chenu.

Ninachojua; bunge halipo juu ya maamuzi ya vikao halali vya Chadema.
 
Back
Top Bottom