Rais Samia amtembelea Mzee Warioba. Je, Katiba Mpya kupata kiki?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Salaam Wakuu,

Leo rais Samia amemtembea Waziri Mstaafu Jaji Warioba na Mawaziri Wastaafu wengine.

Kwasababu Jaji Warioba anapigania Katiba Mpya, Je, rais kasikia kilio cha Watanzania? Jaji Warioba ataua ndege Wawili kwa Jiwe moja?

Mawaziri Wakuu wasitaafu wamekuwa Msitari wa Mbele kupambania Katiba Mpya.

Mwaka Ujao unaweza kuwa wa neema kwa Wapigania Katiba Mpya.

Aji Joseph Warioba alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Hivi karibuni, August 09 2021 Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba aliwataka viongozi wa Serikali kutegua kitendawili cha lini mchakato wa mabadiliko ya Katiba utahitimishwa ili Taifa liwe na utulivu.

Pia soma alichokisema Waziri Mkuu Msitaafu Msuya: Mzee Cleopa Msuya: Suala la Katiba Mpya haliepukiki kwani Katiba siyo Jiwe au Amri ya Mungu
20211202_163355.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumjulia hali leo tarehe 2 Desemba, 2021.
20211202_163758.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa David Msuya mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumjulia hali leo tarehe 2 Desemba, 2021.
 
Salaam Wakuu,

Leo rais Samia amemtembea Waziri Mstaafu Jaji Warioba na Mawaziri Wastaafu wengine.

Kwasababu Jaji Warioba anapigania Katiba Mpya, Je, rais kasikia kilio cha Watanzania? Jaji Warioba ataua ndege Wawili kwa Jiwe moja?
Hao wazee wasipokuwa wanafiki wakamwambia ukweli, wazo la katiba mpya litamsaidia aonekane shujaa kwataifa. Hilo litamfanya atengwe na inzi wa kijani. Akikataliwa ccm aende upinzani akagombee huko, na atapokelewa japo kwa masharti.
 
Hizi shughuli za kuwatembelea watu angekuwa anafanya weekend au awaite Ikulu.
 
Katiba si agenda ya CCM kwa sasa, Rais Samia lwenye hili la katiba CCM washampigia mstari. Kama akilianzisha litakuwa la kwake si la chama.
 
Back
Top Bottom