Rais hujui nini cha kufanya ili tuendelee?! Unataka kukopi historia ya nchi nyingine?! Duh!Rais Samia Suluhu Hassan anasema :
"Sote tunafahamu kuwa miaka ya 1960/70 nchi yetu na nchi za bara la Asia zilikuwa na uchumi unaolingana, lakini 'baada ya muda' wenzetu wametupita tena sana. Mfano Thailand kwa miaka hiyo ilikuwa na 'GDP Per Capita' ya Dola 166 na Tanzania tulikuwa 165. Leo Thaliland wako Dola 7,495 na sisi tuko 1,227.
Kwa hiyo hao mnaokwenda upande huo (Mabalozi) mtuambie wenzetu wamefanya uchawi gani kwenda haraka hivyo na sisi tunakosa nini? 'mentality' au vitu gani? Tuna 'resource' hatuzitumi? Mtuambie wenzetu
wamefanya nini na sisi tufanye nini."
Yaani Rais kushindwa kuelewa suala kama Hilo, why nchi kama Thailand imepaa kiuchumi? Kweli hapa katiba imetukatili..ndio maana nchi zingine Rais akifariki wanaitisha uchaguzi mkuu ili wananchi wampime kama anatosha kukalia hicho kiti na je ana uelewa mpana wa dhana ya maendeleo?