Shaka: Wenzetu wa vyama rafiki njoo tumuunge mkono Rais Samia kwani maendeleo anayofanya hayana jina la Chama chochote

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,519
2,132

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema ni jukumu la Watanzania wote kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo nchini.

Shaka ameyasema hayo leo Oktoba 30, 2022 Msalato mkoani Dodoma alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua ni kwa kiasi gani CCM inaridhishwa na utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi (2020-2025 baada ya Rais Samia kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato mkoani humo.

"Wote tuna jukumu la kujenga nchi bila ya kuangalia itikadi zetu za kisiasa, haya yanayofanyika ni kwa maslahi mapana ya Watanzania. Ni imani yetu kwamba wenzetu wa vyama vingine wataunga mkono jitihada hizi.

"Ni kweli Ilani inayotekelezwa ni ya Chama Cha Mapinduzi lakini maendeleo yanayoletwa ni ya Watanzania wote kwa ujumla, kwa hiyo nitoe wito tumeanza vizuri, Mheshimiwa Rais Samia tangu ameingia madarakani ametuunganisha pamoja, tunakwenda vizuri kikubwa ni kuendelea kusisitiza kuwa umoja wetu ndio ushindi wetu," amesema.

Aidha, Shaka amesema kuimarika kwa ujenzi wa miradi ya kimkakati ni kufungua fursa za kiuchumi kwa Watanzania hivyo ni ana imani kwamba wananchi watatumia vyema fursa ambazo zinatolewa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
 
Hivyo vyama vyenye miaka 30 bila hata Ofisi unadhani vinafahamu maana ya maendeleo?

Kidogo ACT nawaona kuwa ni watu waungwana
 
Ujinga wa Mwafrika. Anawakataza wasifanye siasa kwa mujibu wa sheria

Anawataka wasimame majukwaani kumsifia, na wahuni wataunga mkono
 
Hivyo vyama vyenye miaka 30 bila hata Ofisi unadhani vinafahamu maana ya maendeleo?

Kidogo ACT nawaona kuwa ni watu waungwana
Jengo Zitto analo jinasibu nalo ni mali ya Maalim Seif Foundation na akileta ule usaliti wake kwa Wapemba wataondoka na jengo lao.
 
View attachment 2402837
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema ni jukumu la Watanzania wote kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo nchini.

Shaka ameyasema hayo leo Oktoba 30, 2022 Msalato mkoani Dodoma alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua ni kwa kiasi gani CCM inaridhishwa na utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi (2020-2025 baada ya Rais Samia kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato mkoani humo.

"Wote tuna jukumu la kujenga nchi bila ya kuangalia itikadi zetu za kisiasa, haya yanayofanyika ni kwa maslahi mapana ya Watanzania. Ni imani yetu kwamba wenzetu wa vyama vingine wataunga mkono jitihada hizi.

"Ni kweli Ilani inayotekelezwa ni ya Chama Cha Mapinduzi lakini maendeleo yanayoletwa ni ya Watanzania wote kwa ujumla, kwa hiyo nitoe wito tumeanza vizuri, Mheshimiwa Rais Samia tangu ameingia madarakani ametuunganisha pamoja, tunakwenda vizuri kikubwa ni kuendelea kusisitiza kuwa umoja wetu ndio ushindi wetu," amesema.

Aidha, Shaka amesema kuimarika kwa ujenzi wa miradi ya kimkakati ni kufungua fursa za kiuchumi kwa Watanzania hivyo ni ana imani kwamba wananchi watatumia vyema fursa ambazo zinatolewa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Huyu mpemba ameugua ugonjwa wa usamia, hakuna la maana analoongeaga zaidi ya kuimba na kumsifia samia kila mahali anapokwenda.
 
Hivyo vyama vyenye miaka 30 bila hata Ofisi unadhani vinafahamu maana ya maendeleo?

Kidogo ACT nawaona kuwa ni watu waungwana
Tatizo ni ofisi tu? Kwani kukua na kuimarika kwa chama ni ongezeko la ofisi au wanachama na watu wanaokiunga mkono.? Ofisi inaweza kujengwa kwa siku chache lakini kuwajenga watu huchukua muda mrefu. Elewa hili.
 
..Ccm iunde serikali ya mseto na vyama rafiki vinavyowaunga mkono.

..kinyume cha hapo ni kudanganyana na kutumiana.
 
View attachment 2402837
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema ni jukumu la Watanzania wote kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo nchini.

Shaka ameyasema hayo leo Oktoba 30, 2022 Msalato mkoani Dodoma alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua ni kwa kiasi gani CCM inaridhishwa na utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi (2020-2025 baada ya Rais Samia kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato mkoani humo.

"Wote tuna jukumu la kujenga nchi bila ya kuangalia itikadi zetu za kisiasa, haya yanayofanyika ni kwa maslahi mapana ya Watanzania. Ni imani yetu kwamba wenzetu wa vyama vingine wataunga mkono jitihada hizi.

"Ni kweli Ilani inayotekelezwa ni ya Chama Cha Mapinduzi lakini maendeleo yanayoletwa ni ya Watanzania wote kwa ujumla, kwa hiyo nitoe wito tumeanza vizuri, Mheshimiwa Rais Samia tangu ameingia madarakani ametuunganisha pamoja, tunakwenda vizuri kikubwa ni kuendelea kusisitiza kuwa umoja wetu ndio ushindi wetu," amesema.

Aidha, Shaka amesema kuimarika kwa ujenzi wa miradi ya kimkakati ni kufungua fursa za kiuchumi kwa Watanzania hivyo ni ana imani kwamba wananchi watatumia vyema fursa ambazo zinatolewa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
YUPO ZITTO KABWE
 
Maendeleo haya chama hii ni kaulimbiu ya Rais Samia Suluhu
 
Back
Top Bottom