Mjadala: Tundu Lissu, Zitto Kabwe, Nape Nnauye na James Mbatia, wawasha moto hatima ya Tanzania na Rais Samia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Salaam wakuu,

Nitaweka Update hapa. Karibuni.

Topic: Vyama vya siasa na haki ya kuendesha mikutano na shughuli za kisiasa.

Wanaochangia mada ni James Mbatia, Zitto Kabwe, Tundu Lissu na Nape Nnauye &Ashura K

===
UPDATES

=====

JAMES FRANCIS MBATIA, Mwenyekiti Taifa NCCR Mageuzi anasema:

Sisi NCCR MAGEUZI Tunaamini katika haki. Kamati ya mabadiliko ya KATIBA ua wakina Kasanga Tumbo, wakina Mapalala na Antony Komu, Lingo tenga, na Kidambwage, waliunda kamati ya taifa ya mabadiliko ya Katiba. Tume ya Francis Lucas Nyalali nayo ikaja na mapendekezo.

CCM hawakulidhia, Sherie ibara ya 3 na ibara ya 10 iliyosema CCM ndo chama pekee kuongoza Tanzania ilibadilishwa. Zilibadilishwa lakini sheria namba 5 ya 1995 ikabaki vilevile.

Tumefanya kazi za siasa katika mfumo wa chama kimoja cha siasa kwa miaka yote. Kamati ya ulinzi na usalama inaongozwa na mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa. Mkuu wa mkoa na Wilaya ndo Wenyeviti wa Kamati za Usalama na Wajumbe wa kamati kuu ya CCM taifa.

Rais Mstaafu Jakaya kikwete baada ya shinikizo kubwa, mwaka 2014, akaanzisha mchakato wa Katiba Mpya. Alijitahidi kwa uwezo wake.

Kwakuwa CCM walikuwa wengi, hawakutaka Katiba mpya na mawazo ya wananchi lakini Mwalimu Nyerere akalazimisha vianzishwe vyama.vingi baada ya 20% kukubaliana na vyama vingi.

Katika siasa za vyama vingi, Awamu ya tano ilikuwa ni matatizo. Rais ya awamu ya tano akafuta shughuli za kisiasa na akasema 2020 atahakikisha anafuta vyama vyote vya Siasa. Akasema hadi 2020 atakuwa amefuta vyama vya kisiasa.

Kwa muda huo watu wameuawa watu wamepotea, Watu wametekwa na mashehe wa Uamusho hawapewi haki. Yaani ukiukwaji mkubwa haki za binadamu ulitokea kipindi cha Magufuli. Ila Kwa matakwa ya Mungu akafariki dunia.

Mungu ni mwema tukapata rais Mpya Samia. Samia akasema tusahau yaliyopita tusonge mbele. Sisi hatuamini kusonga mbele sababu bado mfumo ni uleule.

Mbaya zaidi bado anakili yeye na awamu ya tano ya Magufuli anasema wapo pamoja.

Tunatakiwa tuwe na suruhu ya pomoja, Tuwe na meza ya mazungumzo. Tanzania ni yetu sote. Tuna chuki tuna hasira na maumivu makubwa. Yote hii sababu ni kukosekana na mifimo ya haki. Kuna sheria kandamizi nyingi sana. Tukikaa tukakubaliana na kuondoa mifumo inayo tegemea haki kutoka kwa mutu, nchi itasonga mbele.

Tuwe na mifumo endelevuimara ili tuponye majerahana taifa lisonge mbele

Zitto Kabwe Kiongozi wa Chama chama ACT-Wazalendo

Leo Watu muhimu katika demokrasia ya nchi yetu tunajadiliana. Nape, Lissu na Mbatia

Miaka 5 na miezi mitano nchi imepita kwenye Jaribio kubwa sana ambalo limevunjavunja misingi na matakwa ya demokrasia. Tulizoe chama cha siasa kikifanya mikutano yake na kuitisha mikutano ya kuandikisha wanachama wapya na kukosoa serikali. Tangu 1992 hadi 2015 tulijenga utamaduni wa kidemokrasia ambao ulihimili hata changamoto na ushindani na hoja kinzani na mijadala iliboreka ya kidemokrasia.

Toka mwala Nov 2015 tukiwa pale Mbagala Zhakiem 05 Juni 2016 ndo ulikuwa mkutano wetu wa misho wa hadhara k
Kwa ACT Wazalendo. Aliyekuwa rais wa Tanzania Hayati Magufuli akapiga marufuku Mikutano ya kisiasa Kinyume na katiba na Baadaye akasema 2020 hakutakuwa na vyama vya upinzani.

Watu wanadai Tukubalije jambo ambalo si la kisheria kulitekeleza? Niwakumbushe Tulipinga hadi mahakamani, tulienda Mahakamani kupinga kukatazwa mikutano ya hadhara, lakini mahakama zilikuwa captured. Hadi mikutano ya wabunge wa kuchahuliwa wa upinzani ndani ya majimbo yao ilikuwa hairuhusiwi.

Mbunge haombi kibali bali anatoa taarifa Polisi ili watoe ulinzi. Lakini Polisi walikataa mikutano ya wabunge ya upinzani, tulikatazwa kufanya Siasa.

Sababu zilitolewa ni dhahili zilikuwa zinatolewa na mtu ambaye haelewewi demokrasia. Hajui kuna vyama havina wabunge, kuna vyama vipya vinaanza. Tatizo kila kauei ya Wanasiasa ambayo sio Sheria, Polisi walikuwa wanatekeleza.

Nini tufanye?

Kuna azimio la Zanzibar la kuelekeza tufanye mikutano. Lakini vyama vikatishiwa na kila mbinu ikafanyika tusifanye mikutano ya kisiasa.

Kwa kawaida si kazi ya rais kuruhusu mikutano ya kisiasa. Kwakuwa Rais ni mpya, Tuendelee m na siasa tuone kitakachofanyika. Vyama vinafanya mikutano lakini polisi wanakataa kwamba hawajapewa taarifa. Polisi waliomba mikutano iahirishwe pale Iringa eti ni amri kutoka juu.

Napendekeza rais Samia aache mikutano ya Kisiasa iendelee

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye(CCM)

Demokrasia ni mchakato ambao haukamiliki. Ukuaji wake si wa mara moja.

Demokrasia ni pamoja na kuheshimu Taasisi zinazounda Demokrasia. Taasisi zinazounda Demokrasia ni pamoja na vyama vya kisiasa. Sasa hivi kuna Wanachama wapo Bungeni wa Chadema lakini chadema ilishawafukuza. Kwanini wapo Bungeni? Wanatakiwa wasiwepo. Tufuate Sheria.

Kusema kwamba Wakati vyama vingi vinarudi miaka ya 90 eti CCM haikuwa tayari, Si kweli. Mwalimu Nyerere alikuwa CCM na bado akakubaliana na Wenzake kuruhusu vyama vingi, wengeweza kukataa.

Katiba ilibadilishwa na tume mbalimbali zilipendekeza namna ya kuendesha vyama vingi ikiwemo ya jaji Nyalali.

Je kasi ya Demokrasia tuliyoenda nayo inatosha? Tufanyeje?

Siasa za mkapa si ya Kikwete, na Siasa za Kikwete si sawa na Siasa za Hayati Magufuli na Magufuli style haiwezi kuwa ya Samia. Tumepitia Milima na mabonde kwenye Siasa hadi hapa tulipfikia. Wapo walioumia na Wengine kufurahi. Ipo haja kuangalia kesho yetu kama Nchi, tujifunze kutokana na milima na mabonde tuliyopitia. Raisi Samia katoa Uwanja wa Meza ya Mzungumzo. Kwakuwa yupo tayari kukaa meza moja, basi tusikatae mazungumzo

Twende mezani tuzungumze. Nlishiriki mazungumzo mbalimbali, hata katiba ilipokwama. Tulifanya mazungumzo na vyama vya Siasa virudi Bungeni.

Ni vizuri tusahau yaliyopita na tuaminiane tukae Meza moja. Tukitoka mezani ndo tuambiane mtu kakosea wapi. Hayati Magufuli katufundisha mengi, katuonesha Mashimo mengi ambayo bila yeye tusingeyaona. Kasaidia kuonesha kwamba tunatakiwa kujenga taasisi imara zaidi. Demokrasia ni mchakato kulingana na wakati na watu.

Ni vizurituielezee demokrasia kwa mazingira yetu. Tunamshukuru rais Samia kwa kuruhisu kuzungumza. Tusinyosheane vidole bali tukatengeneze yasijirudie yaliyotokea.

Tundu Lissu

Kila Ijumaa kuanzia Novemba mwaka jana nafanya mikutano hii bila kukosa, tunawakaribisha Wageni.

Hapa tulipofika ni matokeo ya kuingia vyama vingi bila demokrasia.

Kama tunataka tusonge mbele lazima tutengeneze Demokrasia

Tuliingia bila kufanya Mabadiliko katika sheria. Na taasisi zilizopo zilijengwa kama taasisi ya chama kimoja na hazikufanyiwa mabadiliko. Ndio maana kukikuwepo Mkoa wa majeshi wa CCM. Hadi leo Mkoa wa Majeshi wa CCM Bado upo. Majaji, mahakimu, nk bado wapo kwa mfumo wa chama kimoja.

Tulipoingia kwenye mfumo wa chama cha siasa. Tuliondoa sheria na Kanuni bali mfumo ulibakia kama ulivyo.

Nyalali alisema sheria 40 hazipaswi kuwepo. Tume ya Nyalali ilisema katiba hii ya 77 kimsingi ni katiba ya chama kimoja. Ilipendekeza katiba mpya ya kuingiza mfumo wa vyama vingi na muundo mpya wa Muungano wa serikali tatu. Mapendekezo yalikataliwa na waliokuwa madarakani.

Katiba inaruhusu mikutano na maandamano ya Kisiasa lakini Polisi wana sheria mpya ya kukataza Mikutano. Katika mfumo wa Vyama vingi bado sheria za tawala za mikoa ni ya Chama Kimoja. Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wanaweka watu ndani. Rais ana mamlaka ya kuweka watu kizuizini bila kupelekwa mahakani. Na sheria Kandamizi hazikufanyiwa marekebisho.

Mfumo wa uchaguzi ni Mfumo wa chama kimoja ya 1985. Ilitungwa kwa mazingira ya chama kimoja tangu 1962 hadi leo.

Tuliingia vyama vingi bila demokrasia. Vya. Vyote vilitakiwa kusajiliwa. CCM imesajiliwa kwa sheria. Kisheria, msajili hawezi ifuta CCM. Kwani imesajiliwa kisheria. CCM ni mchezaji na refarii. Hadi 2015 yote yamfahamika.

Kwa miaka mitano rais anasema kamata huyu unakamatwa. Nlikamatwa mara 8 kwa mwaka, Nikiuliza kwanini nakamatwa? naambiwa ni amri kutoka juu. Sijawahi ambiwa nani katoa hiyo Amri kutoka juu. Ukweli wa amri kutoka juu ni amri za Ikulu.

Katika mazingira haya, Katika Hotuba ya Samia, ilikuwa si mbaya kutamka mambo ambayo hayahitaji mabadiliko ya Sheria. Kusema vyama vifanye mikutano kama Kawaida haihitaji mabadiliko ya Sheria. Zaidi ya watu 4000 wanachama wa Chadema wapo mahabusu, haikuhitaji Sheria kusema waachiliwe huru.

Nimekimbia nchi sababu kila mara nlikuwa naambiwa tunakuja kukuua, na nimeponea chupuchupu kuuawa 2017. Kwenye hotuba yake Bungeni angesema walio nje waje tujenge Nchi tutawalinda, haikuhitaji mabadiliko ya Sheria.

Nina kesi 6 Mahakamani za kusingiziwa. Gari nliyopigiwa nayo risasi ambayo ni mali yangu binafsi nmenyang'anywa. Sijapewa kiunua mgongo wala posho kwa miaka nlotumikia bunge. Jana kwenye Hotuba ya rais Bungeni ulikuwa ni muda wa kuweka sawa mambo mengi.

Watu tusio CCM ni mateka wa CCM. Hatufanyi siasa zozote.

Mandela aliambiwa ili tukuachie huru sema hadharani hutaki mapambano wala kuwapinga makaburu. Ezekia Wenje na Godbless Lema wapo Canada Uhamishoni baada ya kutishiwa kuuawa, mimi nipo uhamishoni.

Sisi tunaotishiwa tutakosaje kuwa na hofu? Ili tusiwe na wasiwasi. Haya nlosema wayafanye. Tunahitaji haki zetu.

Nape Nnauye

Wakati Vyama vingi vinaanzishwa, watu waliootoshwa hivyo wakawa walijua vyama vingi ni machafuko. Lakini mwalimu akasema hawajaeleweka na akasema twende na vyama vingi. Nmesimamka maktaba ya CCM hayo yote yapo

Rais kashasema, twende mezani tuongee haya. Tusianze kusema watu hawana njia njema wakati hatujaenda mezani.

Waingereza wana Malkia na hawafanyi uchaguzi wa Malkia bali Wanafanya wa Waziri mkuu tu. Hivyo ndivyo Demokrasia yao ilivyo.

Uarabuni hawajui mambo ya Uchaguzi China kuna chama kimoja.

Hao Wote wameamua mfumo wa kuongoza nchi zao. Tusi-copy na ku-paste demokrasia kutoka sehemu nyingine.

Haki za kujieleza kupata maoni nk hayo ni ya Msingi. Sisi sio nchi ya kifalme. Tutengeneze Demokrasia kutokana na Mazingira yetu.

Kwa mazingira yetu, Zanzibar ni Serikali ya kitaifa tofauti na huku bara. Demokrasia ya Uingereza na tanzania haiwezi kufanana..

James Mbatia

Nyerere alisema watanzania ni ndugu. Ndugu gani ambao tunabaguana? Kwa miaka 5 CCM imebagua vyama vingine, wamefanya Mikutano ya kisiasa na Kampeni peke yao.

Watu wanaitwa Wanyonge. Wanyonge ni watu fukara, shaifu nk. Kwanini tuweke pressure ya kumwaga damu hadi watu wanakimbia Nchi?

Tufanye nini?

Rais ni zao la katiba basi katiba iheshimiwe. Ukiita mtoto Suluhu ataleta Suluhu, Ukimuita Mtoto Amani ataleta amani, na Mtoto ukimuita masumbuko ataleta usumbufu. Sasa tuna Suluhu. Suluhu awe mama wa taifa atutoe hapa tulipo. Amuite Lissu arudi Nchini ajenge Nchi. Sababu Raia Suluhu alimtembelea Lissu alipokuwa amelazwa Nairobi. Tuna ukabila hapa Tanzania. Tusikubali huu ukabila ukue.

Tundu Lissu

Nape anachotuambia sio sahihi. Demokrasia ni uwepo wa ushimdani wa kisiasa. Vyombo vya habari mahakama na bunge viwe huru. Tofauti na hapo sio demokrasia.

Mwaka 1964 tulivunja vyama vingi. Uchaguzi wa Chama kimoja sio wa kidemokrasia. Saudi Arabia hakuna Demokrasia

Makatazo ya kisiasa yaondolewe. Nchi hii ina sheria za ajabu tulizotoka nazo kwa Wakoloni Waingereza. Magufuli na Kikwete wakaongeza nyingine kandamizi. Vyombo vya habari na vyama Vya kiraia tupigamie katiba mpya. Rais yupo juu ya katiba na sheria.

Kwa mfumo huu hata malaika atakataa.

Mfumo huu tulionao ukipitiwa upya vyama vingi vitakuwa na maana.

Zitto Kabwe

Nmeulizwa eti Mbona tulikuwa hatuchuki hatua Polisi wakikataza mikutano?

Hilo ndo kosa kubwa tumefanya. Kuruhusu agizo lisilo la kisheria kuonekana ni la kisheria. Tulienda Mahakamani Jaji mwacha alisema rais anashitakika katika swala la CAG. Wakapeleka haraka haraka mswada wa sheria bungeni kukataza na kufanya rais kutoshitakiwa. Kwenye uongozi wa Hayayi Magufuli, Sio vyama tu bali taasisi za Kiraia na Wanahabari wote walishughulikiwa.

Kuna matatu ya kujifunza.

1. Lazima tukatae demokrasia ya kupewa sababu si endelevu.

2. Tuhakikishe tunaimalisha mifumo. Na rais samia alizingatie. Tuheshimu hii katiba na haki zake kwanza

3. Tuimalishe vyama vyetu. Tusiruhusu Mtu aamue anavyotaka. Miaka mitano tulipigwa ganzi

4. Chadema hawashiriki uchaguzi. Sisi tunashiriki kata 18 na muhambe na buhigwe tutashiriki na tunafanya documentations ili tumpime rais Samia kama hali ni ile ile au la!

James Mbatia

Kuaminiana ni tatizo Tanzania. Tumezungumza sana lakiniVitendo ni matatizo. Awamu ya nne kidogo Kikwete alijaribu kurudishaKatiba mpya. Mama Samia sawa ameongea Vizuri. Hata Magufuli alisema uchaguzi wa 2020 utakuwa wa haki, wote mliona kilichofanyika. Uongozi wa Magufuli hadi Dola ilidhibiti chama kilicho madarakani.

Kinachotakiwa ni kiongozi aaminiwe kwa maneno na matendo. Miaka 30 inatosha. Kudai katiba mpya Isiwe jukumu la wanasiasa tu bali kila Mtanzania. Sio watu wanauliza wapinzani mnafanya nini? Kupigania haki na Uhuru sio swala la Wanasiasa pekee.

Nape:

Ccm mwenyekiti kukaa miaka 20 sio demokrasia kwa wenzetu ni demokrasia.

Nakubali demokrasia, lazima. Tujenge taasisi imara. Hata ccm. Tumejifunza. Tawala zijazo tutajarobu kuofanyia kazi

Ningekosoa kuondoa wapinzani wa uchaguzi. Cdm baadala ya chadema anaomdolewa si sawa. Tulikuwa tunajipima. Kutoka kwao. Kuna upungufu wa shwria kwemye sheria za mitaa. Mtu anakosea kidogo anaomdolewa. Hili nalipinga. Local government wanajuama

Covid-19 : tuheshimu taasisi zinazo tengeneza demokrasia. Kama vyama. Vimefukuza wanachama tuheshimu hilo. Nakera watu ila linaeleweka. Mtu hana chama kafukuzwa, hawezi kuwa mbinge

Twende mezani tujue ccm wapo thabiti au la! Twende mezani.

Lissu:

Hakuna aliyekataa kwenda mezani. Hatiwrzi kwenda wakati tumefumba macho. Wewe nape huvai kiatu tunachokivaa sisi. Tumelala ndani, tumepigwa, tumepknea kifp. Mimi nipo unelgiji. Lazima kuwe na mazingi5ya mazungumzo kufanyika. Tunaenda tukiwa mateka wenu

Mahakama ya Tanzania inahitaji kukombolewa. Mahakama inaamuliwa na mtu. Sijawahi kuona demokrasia onapatikana mahakamani na majaji hawa bali mitaani na Porini.

Miaka 5 ya magufuli ilitutengeneza kuanzia chadema ni Msingi. Tukajifunza kuishi na dikitekta. Kama Magufuli tumeweza, mama Samia hatutashindwa. 99% wagombea wetu walipofika tukasema tutapigania demokrasia kwanza na Tume ya uchaguzi

Mamlaka ya rais yakidhibitiwa, pengine ni rahisi.

Demokrasia inatuhusu sisi wote. Namkumbusha nape. Nlimwambia sisi tunashughulikiwa kesho ni wewe. Wafanyakazo mishahara wamefukuzwa wamenomolewa nyumba nk. Demokrasia si wanasiasa bali ni kila mtu. Tushikamane tupiganie demokrasia. Tusimpe nafasi mama samia ya kusubiri demokrasia. Tusubiri hadi lini?

Mbatia:
Utu wa mwanadamu uheshimike. Tukiheshimiana yote tutayaweza. Tuaminiane.

Zitto

Tuna firsa ya kujenga demokrasia ili kuepusha hatari. Demokrasia yetu haikuweza kuzuia mtu mmoja kubomoabomoa jinsi alivyotaka. Tujenga demokrasia ambayo itafanya mtu kama Magufuli akitokea tena asilete madhara.

Nape Nnauye:

Kila jambo chini ya jua lina sababu zake. Kuja kwa Magufuli tumejifunza mengi. Tanzania ni kubwa kuliko vyama na itikadi zetu. Tuilinde Tanzania kwa kila tunachokifanya. Sina mashaka na ndugu zetu pamoja na tofauti za kisiasa.

Tundu Lissu

Haki huinua taifa. Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi. Bali mwovu atawalapo, watu huugua

Bila haki hakuna amani. Wanaolia kwa njaa ya haki, hatuwezi kulia milele. Hata wewe uliye salama hauko salama. Nani alifikilia Kinana angepigwa kodi ya bilioni 3? Nani alifikiria Nape angetolewa bunduki hadharani?

Samia atenegeneze Tanzania yenye haki. Sababu ipo siku atatoka hapo alipo. Tupiganie haki na demokrasia.

Mwisho

Kama hao ndio wanajadili mustakabari wa taifa basi .hoja zao ni upuuzi mtupu
 
Ni hoja zenye mashiko
 
Back
Top Bottom