Rais Samia amesahau hili la umeme ni yeye amelileta, tumkumbushe

Kumbe yeye alikuwa anamsapoti mwendazake kinafiki, hii dhambi mbaya sana; ndio maana sasa amekutana na anaehoji hadharani anamuona adui, badala ya kumjibu hoja zake anamuagizia kikundi cha mipasho toka mikoani waende kumsuta ikulu.
ndugu yangu teuliwa kuwa mbunge hlafu upewe uwaziri kama hutakuwa mnafiki namba moja. kwa afrika hii ni kujipendekeza kwa mkulu hata kama hutaki utakubali tu ingawa moyoni utakuwa unagugumia. THIS IS AFRICA bhaana, gombea urais tukupe kama utakubali kupingwa waziwazi!!!! acha usitud................... hapa
 
Kwanza kabisa mimi ni muumini wa kumkosoa mtu yoyote kwa staha, siamini kwenye kudhihaki Wala kutukana.
Kama raisi kuna sehemu amekosea basi tumkosoe kwa staha tumkosoe bila kumvunjia heshima, yeye ni binadamu anapitiwa.
Hili la umeme wa kuunganisha watu wote kwa 27,000 ni yeye amelileta.
Mwanzo 27,000 ilikua kwa watu wa REA tu ila kwa watu wa mijini ilikua 321,000.
Baada ya mama Samia kuwa raisi wote tulianza kulipa 27,000 mwezi June mwaka jana na kwa kweli tulimpongeza kwa hili.
Leo mama anasema hii 27,000 kwa wote haiwezekani. Sawa, Ila ina maana amesahau miezi michache nyuma alileta hili?
Akiwa njiani kuelekea Dodoma alisimama na kuwaambia wananchi kuwa tumepunguza gharama ya kuunganisha umeme kwa watu wote, watu wakashangilia sana.
Leo watu hawa watakuaje?
Chini nimeweka video, mama Samia akizungumzia kupunguza gharama za kuunganisha umeme.
Huenda amesahau.........tumkumbushe.

View attachment 2069248

Nawe tukukumbushe: "The entire system is not credible".
 
Ukweli nikwamba kuunganishiwa Umeme kwa 27 elfu ni hasala kwa Tanesco,maana lazima tujue kwamba hivyo vitu vina nunuliwa .
.
Hata hivyo inafaa kuweka Bei nafuu kiasi ,mfano nguzo si sahihi mteja kulipia sawa na mteja kulipia miundombinu ya simu ,Kama simu hatulipi inafaa na Tanesco kuondoa gharama hiyo .

Pili Meter luku isizidi tsh 150,000\=
 
Ukweli nikwamba kuunganishiwa Umeme kwa 27 elfu ni hasala kwa Tanesco,maana lazima tujue kwamba hivyo vitu vina nunuliwa .
.
Hata hivyo inafaa kuweka Bei nafuu kiasi ,mfano nguzo si sahihi mteja kulipia sawa na mteja kulipia miundombinu ya simu ,Kama simu hatulipi inafaa na Tanesco kuondoa gharama hiyo .

Pili Meter luku isizidi tsh 150,000\=
Kwani mita ni mali ya nani?
 
Kwani mita ni mali ya nani?
Meter imeandikwa ni Mali ya Tanesco ,lakini mtumiaji na mwangalizi Ni mteja husika, ndiyo maana hata ikisumbua anaye hangaika kuhakikisha inafanya kazi ni mteja.
Bahati mbaya serikali haijaweka mazingira sawa ju ya maswala ya Umeme .

Inafaa Sasa iruhusu kampuni binafsi ziwekeze kwenye sector hii. Ili kuondoa ubabaishaji na unyonyaji unao fikiriwa na wananchi!
 
Back
Top Bottom