Rais Samia amesahau hili la umeme ni yeye amelileta, tumkumbushe

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,960
Kwanza kabisa mimi ni muumini wa kumkosoa mtu yoyote kwa staha, siamini kwenye kudhihaki Wala kutukana. Kama raisi kuna sehemu amekosea basi tumkosoe kwa staha tumkosoe bila kumvunjia heshima, yeye ni binadamu anapitiwa.

Hili la umeme wa kuunganisha watu wote kwa 27,000 ni yeye amelileta. Mwanzo 27,000 ilikua kwa watu wa REA tu ila kwa watu wa mijini ilikua 321,000.

Baada ya mama Samia kuwa raisi wote tulianza kulipa 27,000 mwezi June mwaka jana na kwa kweli tulimpongeza kwa hili.
Leo mama anasema hii 27,000 kwa wote haiwezekani. Sawa, Ila ina maana amesahau miezi michache nyuma alileta hili?

Akiwa njiani kuelekea Dodoma alisimama na kuwaambia wananchi kuwa tumepunguza gharama ya kuunganisha umeme kwa watu wote, watu wakashangilia sana. Leo watu hawa watakuaje?

Chini nimeweka video, mama Samia akizungumzia kupunguza gharama za kuunganisha umeme.

Huenda amesahau, tumkumbushe.
 
Kumbe yeye alikuwa anamsapoti mwendazake kinafiki, hii dhambi mbaya sana; ndio maana sasa amekutana na anaehoji hadharani anamuona adui, badala ya kumjibu hoja zake anamuagizia kikundi cha mipasho toka mikoani waende kumsuta ikulu.
 
Mkuu hii tayari mama samia ameshakua raisi, ilikua mwaka jana mwezi wa 6.
 
Kwani kile kikundi cha taarabu kipo ukumbini tayari kutumbuiza?
 
Nyie Ni watheenge,simlikuwa mnalaumu humu kuwa kwann bei ya umeme kuunganishiwa imeshushwa? Tena Kuna mjinga mwenzenu aliinzisha na thread kabisa ya kulaumu, kenge nyinyi
Unatukana sana,
 
Hakika pale TANESCO panajambo gumu. Samia hajapajua vizuri, naamimi ipo siku atakuja kujichanganya tena.

Mwaka jana June 2021 Rais Samia mwenyewe akiwa katika ziara zake alisema yafuatayo.

Rais Samia : Lakini pia upande wa umeme si ndio?
Wananchi: Ndioo!
Rais Samia : Umeme tumeshusha bei ya kuunganuisha umeme.
Wananchi: wakapiga ndelemo na makofi!
Rais Samia : Mulikuwa Munaunga umeme kwa laki ngapi?
Wananchi: Laki tatu wengine taki nne!
Rais Samia : Tumeshusha mpaka shiling elfu 27.
Wananchi: wakapiga ndelemo na makofi!
Rais Samia : Hiyo ndio kazi ya serikali ya Chama cha mapinduzi.

Wananchi: wakapiga ndelemo na makofi!

Jana 4th January 2022 tena akasema tuliharibiwa. "Tulihariniwa katikati hapa kwa kusema, kila mwananchi ataungiwa umeme kwa shilingi Elfu 27, Sio hivyo".

Siku akikutana na ESCROW na DOWANS ndio atajua hajui.
 
Hapo wanamtuhumu Kalemani wakati ilikiwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM na wao wakainadi..Sasa wakati CCM wanashusha hawakujua kuwa hawanahera?
 
Mkuu hii tayari mama samia ameshakua raisi, ilikua mwaka jana mwezi wa 6.
Msanii anajipinga mwenyewe, lakini sio kosa lake, anasubiri mpaka afundishwe cha kusema ndio anasema, angalau angekuwa anajua a,b,c...
 
Kumbe yeye alikuwa anamsapoti mwendazake kinafiki, hii dhambi mbaya sana; ndio maana sasa amekutana na anaehoji hadharani anamuona adui, badala ya kumjibu hoja zake anamuagizia kikundi cha mipasho toka mikoani waende kumsuta ikulu.
Sasa akikutana na wanafiki wenzake, anakuja juu.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom