Hawa watakataa unayoyasema.
1. Wale waliopotea na waliopotelewa na ndugu zao katika mazingira tata
2. Wale waliochukuliwa mali zao kidhalimu na ma-task force
3. Wale walipelekwa magerazani kwa miezi na miaka kwa kesi za kubumba
4. Walipoteza maisha katika chaguzi kama Akwilina
5. Waliopoteza biashara kama Kwanza TV na Mbowe
6. Walionyang'anywa passports kama Eyakuze
7. Waliochafuliwa wanafanya biashara za madawa na kipendwa chake Bashite
8. Waliopoteza kazi zao kwa mkono na nia ovu kama Fatma Karume
9. Wakulima Ambao hawakupewa pesa zao za korosho
10. Waliobomolewa nyumba zao Kimara
11.Wastaafu wanaopigwa na jua kutwa wakifuatilia mafao yao ya pensheni
12.Vyombo vya habari binafsi ambavyo viligeuzwa kwa nguvu kuwa state propoganda media.
13.Waliochafuliwa na Musiba pamoja na genge lake
Wengine hao sikia madereva wanakwambia hayo mambo walishaanza kusahau kipindi cha Magufuli yanarudi upya na rushwa juu.
Mama badala ya kubaki na team yenye mafanikio analeta ubinifu wake. Huu moto bado nasubiri mishahara kuanza kuchelewa ndio watu wataanza kuelewa kazi ya kuendesha nchi sio lelemama kama wanavyodhani, mama viatu kwenye hiyo nafasi vinapwaya.
Alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuaminika angeendelea na team ya Magufuli especially kwenye kusimamia mapato na teama Magufuli ndani ya CCM hasa Bashiru kwa nafasi yoyote ile walishaanza kuelewa jinsi ya kuwamudu wanachama wao na watendaji serikalini. Vitu ambavyo vilikuwa aviwezekani kwa miaka 30 ya utawala wa Mwinyi, Mkapa na JK.
Moto wenyewe huko njiani huo moshi tu. Make no mistake it’s coming mama hiyo kazi sio size yake kabisa.