Samia, Mamlaka ya Mwanamke na Somo kwa Taifa

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
709
Reaction score
634
Tumtazame Rais Samia kama jaribio la Taifa letu kujifunza kitu ambacho hatukuwa tumekifanyia mazoezi kabla yake - Jinsi ya kumruhusu mwanamke kuwa na mamlaka.

Kuna mjadala unaoendelea ambao, ukiuangalia kwa juu, unaonekana kama mjadala wa dini lakini ukiuchambua vizuri, ni mjadala mkubwa zaidi kuhusu mwanamke, mamlaka na namna tunavyotafsiri nafasi yake kwenye dola.

Swali, ni kweli eda ya mjane ni miezi minne na siku kumi, na kama ni hivyo, uongozi wa nchi utakuwa “deputized” kwa kipindi hicho? Swali hili ni zito kwa sababu linagusa mahali ambapo tunachanganya mifumo miwili tofauti: eda ni hukumu ya kidini kuhusu mwanamke aliyefiwa na mume; Urais wa Tanzania ni ofisi ya kikatiba yenye mamlaka na taratibu zake.

Qur’an inaweka eda ya mjane kuwa miezi minne na siku kumi, lakini hakuna kwenye aya hiyo inayosema mjane anavuliwa kazi, mamlaka au nafasi yake ya kikatiba. Na Katiba ya Tanzania haijaweka kifo cha mume wa Rais kama sababu ya Rais kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Lakini hapa ndipo historia ya Samia inakuwa interesting zaidi. Samia mwenyewe amewahi kueleza kwamba alipoingia Urais mwaka 2021, hofu kubwa haikuwa tu kwamba alikuwa mwanamke; bali kwamba alikuwa anaingia kwenye nafasi ambayo pia ni ya Amiri Jeshi Mkuu, na kulikuwa na watu waliokuwa wakijiuliza kama mwanamke anayefunga hijabu angeweza kubeba mamlaka hayo.

Alisema mwenyewe kwamba alitambua kulikuwa na minong’ono ya “ataweza kweli huyu?” na akalazimika kuwaambia Watanzania kwa lugha rahisi kwamba “Urais hauna jinsia, Rais ni Rais, mamlaka ni mamlaka.” Samia amekuwa akilazimisha Tanzania kutenganisha mwanamke anayeshika nafasi na nafasi yenyewe.

Mwanamke anaweza kuwa na hijabu bila Urais wake kupungua; anaweza kuwa mama bila mamlaka yake kupungua; na sasa, anaweza kuwa mjane bila Katiba kuacha kumtambua kama Rais.
 
Attachments

  • HRr6xpubwAAtzB-.jpg
    HRr6xpubwAAtzB-.jpg
    169.3 KB · Views: 3

Dr.Samia Suluhu Hassan ameandika na kuweka historia ya kiongozi na Rais mwanamke shupavu na madhubuti zaidi barani Africa 🔥
 
Urais unazingatia zaidi katiba na sio dini. Kama katiba haiongelei mambo ya Edda basi hiyo edda haitazingatiwa.
 
Tumtazame Rais Samia kama jaribio la Taifa letu kujifunza kitu ambacho hatukuwa tumekifanyia mazoezi kabla yake - Jinsi ya kumruhusu mwanamke kuwa na mamlaka.

Kuna mjadala unaoendelea ambao, ukiuangalia kwa juu, unaonekana kama mjadala wa dini lakini ukiuchambua vizuri, ni mjadala mkubwa zaidi kuhusu mwanamke, mamlaka na namna tunavyotafsiri nafasi yake kwenye dola.

Swali, ni kweli eda ya mjane ni miezi minne na siku kumi, na kama ni hivyo, uongozi wa nchi utakuwa “deputized” kwa kipindi hicho? Swali hili ni zito kwa sababu linagusa mahali ambapo tunachanganya mifumo miwili tofauti: eda ni hukumu ya kidini kuhusu mwanamke aliyefiwa na mume; Urais wa Tanzania ni ofisi ya kikatiba yenye mamlaka na taratibu zake.

Qur’an inaweka eda ya mjane kuwa miezi minne na siku kumi, lakini hakuna kwenye aya hiyo inayosema mjane anavuliwa kazi, mamlaka au nafasi yake ya kikatiba. Na Katiba ya Tanzania haijaweka kifo cha mume wa Rais kama sababu ya Rais kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Lakini hapa ndipo historia ya Samia inakuwa interesting zaidi. Samia mwenyewe amewahi kueleza kwamba alipoingia Urais mwaka 2021, hofu kubwa haikuwa tu kwamba alikuwa mwanamke; bali kwamba alikuwa anaingia kwenye nafasi ambayo pia ni ya Amiri Jeshi Mkuu, na kulikuwa na watu waliokuwa wakijiuliza kama mwanamke anayefunga hijabu angeweza kubeba mamlaka hayo.

Alisema mwenyewe kwamba alitambua kulikuwa na minong’ono ya “ataweza kweli huyu?” na akalazimika kuwaambia Watanzania kwa lugha rahisi kwamba “Urais hauna jinsia, Rais ni Rais, mamlaka ni mamlaka.” Samia amekuwa akilazimisha Tanzania kutenganisha mwanamke anayeshika nafasi na nafasi yenyewe.

Mwanamke anaweza kuwa na hijabu bila Urais wake kupungua; anaweza kuwa mama bila mamlaka yake kupungua; na sasa, anaweza kuwa mjane bila Katiba kuacha kumtambua kama Rais.
Kwangu mimi kuhusisha sijui "Eda" na "Urais" ni ujinga mtupu! Na wanachangia mawazo kwenye hoja hii ni wajinga watupu!
 
Back
Top Bottom