Rais Samia aambiwe ukweli, vinginevyo Taifa litaangamia

Rais Samia aambiwe ukweli, vinginevyo Taifa litaangamia

Duh, kauli nzito sana hii.
Referee kwenye hiyo nafasi huwa wananchi wa kawaida sio JF kwa majority. Kauli za angekuwepo fulani haya mambo yasingekuwepo au tulishaanza sahau zinarudi kwa kasi mtaani.

Asilimia kubwa ya JF members awawakilishi maisha halisi ya watanzania ambao wengi hawapo kwenye ajira rasmi, wanafunzi au wakulima; wanaotegemea efficiency kwenye utendaji serikalini kupata nafuu ya changamoto zao

Muda unavyoenda wataongea, Magufuli aliwazoesha mazingira yanayotabirika, tunarudi kule kule kwenye uzembe wa mtendaji mmoja unaleta chain reaction yenye madhara kwa watu wengi sana.

Juzi TRA na server sijui kama washa sort, leo bandari, kesho TANESCO; kila siku jipya. Enzi za hayati sasa hivi ungeona mawaziri wanakimbilia kwenye media kabla mtu ajapoteza ajira, siku hizi mambo ya kazi na bata.
 
Amesikia ila je hao CCM watakubali? maana akitaka kufanikiwa kwa hayo hapo juu ni lazima afute baadhi ya sheria kandamizi ambazo CCM imezitunga makusudi
 
Pls guy's give our President Samia a break,Rais Samia anajitahidi mno na kwa kipindi kifupi ameonyesha she is a superb,kelele za mtoa hoja hii mbona hukuileta wakati wa kipindi cha mwendazake?elewa uelewa wa Rais wa sasa ndio umekupa wewe nguvu wa kuandika haya bila woga.Give credits inapositahili usiwe kama spoiled child.
Amafenya nini kuonyesha she’s superb zaidi ya kuuza sura tu, kwa sasa hatuna Rais labda 2025 CCM wakipata akili watatupa Rais.
 
Eneo la kwanza ni kuheshimu katiba na sheria, hili ni eneo ambalo kama nchi tunataka kudumisha upendo na amani ni la kuzingatia kwa nguvu zote. Samia ameapa kulinda katiba asipofanya hivyo ni uhaini na lazima atakuja kuchukuliwa hatua bila kujali kinga za Urais. Mila na utamaduni wa Taifa lo lote hudumisha na kuimarishwa na katiba yake.

Eneo la pili na uhuru na haki ya wananchi wote bila kujali cheo cha mtu au nafasi yake katika jamii. Hivi sasa kuna watu wanajiona wana haki zaidi ya wengine na hivyo kufanya vitendo vya uonevu na dhuluma dhidi ya wengine. Kuna watu wanasota magerezani bila kuhukumiwa na wengine wamehukumiwa kwa uonezi na husda. Hii si sawa kabisa, Rais Samia anapaswa kuchukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kuunda tume huru ya kijaji kuchunguza haki za wote waliopo mahabusu na gerezani.

Eneo la tatu ni kusikilizwa kwa maoni na vilio vya wananchi bila kujali itikadi zao za kisiasa. Pamoja na kuwa na katiba na sheria zilizopo lakini watu wengi wamekuwa wakiathirika na baadhi ya vifungu vya sheria hizo kwa sababu ni za uonevu na zimetungwa kulinda maslahi ya baadhi ya watu.

Aidha kuna sheria zimetungwa kudhibiti baadhi ya watu na vyama vya siasa bila kuzingatia haki zao za msingi za kikatiba. Kwa hiyo kilio cha kupata katiba mpya ambayo itaendana na wakati wa sasa ni muhimu kusikilizwa na pia kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ambayo itatoa haki sawa kwa kila mtu na vyama vyote vya siasa.

Baada ya miaka mitano tutakuja kuangalia tena hizi graph kuona alipofikia
JamiiForums355102718.jpg
 
Amesikia ila je hao CCM watakubali? maana akitaka kufanikiwa kwa hayo hapo juu ni lazima afute baadhi ya sheria kandamizi ambazo CCM imezitunga makusudi
Siyo suala la CCM kukubali bali itategemea kelele za wananchi na uhalisia wa maisha yao!
 
Ameshatoa maagizo mengi lakini mrejesho wa maagizo hayo hatujapata mfano ni ripoti ya uchunguzi wa fedha za Benki kati ya mwezi January hadi March.

Pia Samia ajue kuwa sheria ina nguvu kuliko maagizo yake ya hapa na pale anayoyatoa kwenye hotuba zake tamutamu, ili tumuelewe basi abadilishe sheria kandamizi zikae vizuri, nje ya hapo tunakuwa tunaishi kwa hisani ya wema wake na wala siyo sheria. Sasa hatuwezi kuwa na amani mpaka afanye reforms za maana kwenye sheria mbovu.

Suala la katiba mpya hilo halikwepeki!
 
Eneo la kwanza ni kuheshimu katiba na sheria, hili ni eneo ambalo kama nchi tunataka kudumisha upendo na amani ni la kuzingatia kwa nguvu zote. Samia ameapa kulinda katiba asipofanya hivyo ni uhaini na lazima atakuja kuchukuliwa hatua bila kujali kinga za Urais. Mila na utamaduni wa Taifa lo lote hudumisha na kuimarishwa na katiba yake.

Eneo la pili na uhuru na haki ya wananchi wote bila kujali cheo cha mtu au nafasi yake katika jamii. Hivi sasa kuna watu wanajiona wana haki zaidi ya wengine na hivyo kufanya vitendo vya uonevu na dhuluma dhidi ya wengine. Kuna watu wanasota magerezani bila kuhukumiwa na wengine wamehukumiwa kwa uonezi na husda. Hii si sawa kabisa, Rais Samia anapaswa kuchukua hatua za haraka ikiwa ni pamoja na kuunda tume huru ya kijaji kuchunguza haki za wote waliopo mahabusu na gerezani.

Eneo la tatu ni kusikilizwa kwa maoni na vilio vya wananchi bila kujali itikadi zao za kisiasa. Pamoja na kuwa na katiba na sheria zilizopo lakini watu wengi wamekuwa wakiathirika na baadhi ya vifungu vya sheria hizo kwa sababu ni za uonevu na zimetungwa kulinda maslahi ya baadhi ya watu.

Aidha kuna sheria zimetungwa kudhibiti baadhi ya watu na vyama vya siasa bila kuzingatia haki zao za msingi za kikatiba. Kwa hiyo kilio cha kupata katiba mpya ambayo itaendana na wakati wa sasa ni muhimu kusikilizwa na pia kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ambayo itatoa haki sawa kwa kila mtu na vyama vyote vya siasa.

Mama aachwe afanye kazi hakuna haja ya kumtishatisha! Mbona kwa Jiwe mliufyata! Msimjaribu!!
 
Miezi miwili hii makelele mengi.

Wakati watu mliu fyata kimyaa Kwa miaka mitano. Huu ni unafiki.

Saa hizi kila mtu rais. Kila mtu kukitia ujuaji.
Kuna kipindi wengine wakawa wamekaa eti kulihutubia Taifa wakati siyo rais. Hii ni shidaa.
 
Back
Top Bottom