benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameielekeza Wizara ya Ujenzi kufanya usanifu wa kina wa barabara za Mwanza Mjini hadi Round about ya Usagara na barabara ya Mwanza Mjini hadi Igoma ili zipewe kipaumbele katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya kujenga barabara ya njia nne.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema hayo Mkoani Mwanza leo November 12, 2023, wakati wa ziara ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Paul Makonda ambapo ametembelea ujenzi wa daraja la JP Magufuli (Kigongo- Busisi) ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 80.
“Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amenielekeza kufanya haraka sana usanifu wa kina wa barabara mbili, barabara ya Mwanza Mjini Kwenda Usagara Kilometa 22 na Mwanza Mjini kuelekea Igoma ili ziwekwe kwenye vipaumbele vya bajeti ya 2024/25 kujengwa kwa njia nne”
Bashungwa amesema kwa kutambua umuhimu wa daraja la JP Magufuli katika kuunganisha ushoroba wa Ziwa Viktoria unaoanzia Sirari mpakani mwa nchi ya Tanzania na Kenya hadi Mutukula Mpakani mwa Tanzania na Uganda, barabara hiyo itapanuliwa na kuwa na njia nne ili kupunguza msongamano wa magari.
Kwa upande wake Makonda amesema daraja la JP Magufuli ni la kimkakati kwani Mkoa wa Mwanza ni katikati ya Nchi za Afrika Mashariki, hivyo itakuwa ni njia ya mkato wa kufikia Nchi jirani.
#MillardAyoUPDATES