Rais Museveni amteua mwanae Muhoozi Kainerugaba kuwa CDF

..Mu7 anataka kuigeuza Uganda kuwa nchi ya Kifalme.

..Nini kitatoke iwapo Waganda wataamua kwamba hawataki tena kuongozwa Kifalme?

..Machafuko yakitokea Uganda athari zake zitasambaa mpaka kwetu Watanzania.
 

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amemteua Mtoto wake Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu mpya wa Majeshi (CDF) Nchini Uganda akichukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri anayehusika na masuala ya biashara kwenye mabadiliko mapya aliyofanya katika Baraza la Mawaziri la Nchi hiyo usiku huu.

Muhoozi aliwahi kuwa kwenye nafasi ya Ukamanda wa Jeshi la Ardhini la Uganda lakini October 04,2022 Museveni aliamua kumuondoa na nafasi yake ikachukuliwa na Meja Jenerali Kayanja Muhanga ambaye alikuwa Kamanda wa Opereshemi Shujaa inayoendeshwa Nchini DRC.

Millard Ayo

Pia soma:

Jenerali Muhoozi Kainerugaba ni dhahiri sasa amelewa madaraka. Ni kweli kwamba hajui madhara ya kauli aliyotoa kuhusu kuivamia Kenya?

Mtoto wa Museveni atangaza kugombea Urais 2026
Safi sana Mzee kaguta!
 
Yajayo yanafurahisha nchini Uganda.

Uteuzi wa Kainerubaga Muhoozi umetagazwa leo usiku wa manane. Aliyekuwa mkuu wa majeshi ameteuliwa kuwa waziri wa nchi.

Kuna tetesi nchini Uganda kuwa Rais anamuandaa mwanaye kuwa Rais.

Kabla ya hapo General Muhoozi alikuwa mkuu wa kikosi maalum cha ulinzi wa Rais na Special security force for installations.

Source: BBC Swahili.
Hamna la ajabu hapa, sana sana nyani haoni kundule. Kwani Hussein Mwinyi nae hakuandaliwa kimya kimya?? Mbona kuna mtoto wa rais mstaafu mmoja na mamaake wote ni wabunge?? Na mtoto kapewa uwaziri akiandaliwa baadae aje awe rais?? Ngozi nyeusi ni ile ile, imejaa ubinafsi na uroho wa kila kitu.Muacheni Museveni , nyie ya kwenu yanawashinda mnashadadia ya wenzenu.
 
Je akilazimisha nini kitatokea!

..tawala za aina hiyo mwisho wake huwa sio mzuri.

..Gaddafi alifanya ujinga wa kutowezesha utaratibu wa kubadilishana madaraka na matokeo yake ni instability aliyoko Libya.

..Mfumo wa demokrasia, chaguzi huru, na utaratibu wa kubadilishana madaraka, unasaidia kwa kiwango kikubwa uwepo wa amani ktk nchi husika.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Napenda tu kuwapeni taarifa wale ambao mlikuwa hamfahamu kuwa Rais wa Uganda Mheshimiwa Yoweli Kaguta Museveni Amemteua Mwanae Jenerali Muhoozi kuwa Mkuu wa majeshi ya Nchi hiyo. Uteuzi huo ambao una maana kubwa sana katika Taifa la Uganda na ambao umezusha maneno mengi sana kwa wachambuzi wa siasa na hata wananchi wenyewe wa Uganda.

Rais Huyo ambaye ndiye Rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu sana kuliko Rais yeyote yule katika ukanda huu wa Afrika mashariki na ambaye wengi wamezaliwa wamemkuta na bado ujana wao unaelekea kuisha bado Rais wao yupo madarakani akiendelea na kazi za kuwatumikia waganda.kwa kuwa Rais huyo alizaliwa mwaka 1944 na sasa amemteua mwanaye ambaye alizaliwa mwaka 1974 kuongoza Jeshi la Uganda.

Kwa wasiofahamu pia jambo lingine ni kuwa Rais Museveni ni kama ndugu yetu tu kwa kuwa amesoma hapa hapa Nchini elimu yake ya chuo kikuu katika chuo kikuu cha Dar es salaam yaani UDSM maarufu kama Mlimani. Kozi ya sayansi ya siasa..lakini ni miongoni mwa viongozi wanaoipenda na kuiheshimu sana Tanzania na watanzania.ni kiongozi ambaye yeye na serikali yake huwezi ukamsikia akiwafanyia hujuma watanzania wala kuwawekea vikwazo vya aina yoyote ile mpakani ,viwe ni vya kibiashara au nini. Ni kiongozi ambaye anaendelea pia kumuenzi sana Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius kambarage Nyerere.

Ni Kiongozi ambaye anaweza kutusaidia hata kijeshi ikiwa tupo na tumeingia vitani kupigana na nchi yoyote ile. Kwa ufupi ni kuwa uwepo wa Mheshimiwa Yoweli Kaguta Museveni madarakani ni sehemu pia ya usalama wetu katika mpaka wetu na yeye.maana hana shida na sisi wala ugomvi na sisi wala kinyongo au chuki au kisasi na sisi.ndio maana amekuwa akitupatia ushirikiano wote kwa kila jambo.Ni ndugu yetu wa Damu ambaye hawezi kutudhuru wala kututishia amani wala kutulaza macho wala kumhofia.

Tofauti na majirani zetu fulani hivi kama wawili hivi ambao kamwe siwezi kuwataja ni lazima tuishi nao kwa akili sanaaa maana hawaaminiki wala hatupaswi kubweteka wala kujisahau wala kuwaamini sana.maana hawatabiriki na wana chokochoko za chinichini na kujiona wao ni bora sana .japo sisi hawatuwezi kwa lolote lile,ndio maana tumekuwa tukiwachukulia hivyo hivyo na kuishi nao kwa akili kubwa na ya tahadhari kwa kila nyanja kuanzia uchumi,biashara,ulinzi na usalama, ushirikiano na mengine mengi tu.

Nimeona niwapeni habari hii kwa kuwa Uganda ni mshirika wetu kwa mambo mengi sana ya kiuchumi, kibiashara na mengine mengi tu.maana ni lazima ujuwe kesho nani anaweza kuja kuwa Rais wa nchi hiyo ili ujuwe mapema huyo atakaye kuja ni mtu na kiongozi wa aina gani na anamtizamo upi na msimamo upi juu ya masuala mbalimbali pamoja na vipi anaitizama nchi yetu na upi ni msimamo wake katika mambo mbalimbali.lazma ufahamu anasimamia nini na anaamini nini hasa kwa mambo yatakayogusa maslahi yetu ambayo kwa sasa tunaendelea vyema katika utawala wa Mheshimiwa Yoweli Kaguta Museveni. Siasa ni sayansi na sayansi ina kanuni zake ambazo ukizikosea huwezi kulipata jibu hata ungefanyeje.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Mpumbavu
 
Back
Top Bottom