Rais Magufuli: Upinzani wa sasa umebadilika

Ila wanavyowanyanyasa wapinzani kwa uonevu, kuwabambikia kesi, kuwahujumu, kuwapiga, kuwadhulumu na wengine 'kupotea' kunafanana kabisa na ule uovu waliofanyiwa mashahidi wa imani ktk vitabu vitakatifu. anyway, Mola hulipa uovu kwa uovu na upanga juu ya upanga.
 
Mwenyekiti wa CCM na Rais John Magufuli amekionya chama chake kisibweteke kwani upinzani wa sasa unatisha kutokana na mikakati yake

Akiwahitubia viongozi wa wilaya na mikoa kote nchini jijini DSM hapo jana Rais amesema wapinzani wa leo wamebadilika na wana mikakati ya hadharani na ya siri katika mapambano ya kutwaa madaraka

Ingawa Rais hakutaja chama chochote kwa jina lakini ni hivi karibuni chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kilifanya mkutano mkuu wake uliovunja rekodi kwa jinsi ulivyopangiliwa vyema na hatimaye ikagundulika kwamba kwa sasa chama hicho kina wanachama wenye kadi milioni 6 na nusu kutokana na operesheni yake ya Chadema ni Msingi iliyofanyika nchini kote kimyakimya kwa miaka miwili.
View attachment 1333871View attachment 1333872View attachment 1333873
Yani hapo mmeshafarijika na mta relax tu, badala ya kufuatilia kuna jambo gani nyuma ya pazia kuhusu mkutano huo IKULU! 🤔
 
Ukweli wa Moyo hutamkwa bila hadhari.. Hutamkwa bila kujipanga... Hutamkwa bila taraji... Na mtamkaji daima huwa hana uwezo wa kuyarudisha kinywani yale aliyokwishatamka
Mwenyekiti wa CCM na Rais John Magufuli amekionya chama chake kisibweteke kwani upinzani wa sasa unatisha kutokana na mikakati yake

Akiwahitubia viongozi wa wilaya na mikoa kote nchini jijini DSM hapo jana Rais amesema wapinzani wa leo wamebadilika na wana mikakati ya hadharani na ya siri katika mapambano ya kutwaa madaraka

Ingawa Rais hakutaja chama chochote kwa jina lakini ni hivi karibuni chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kilifanya mkutano mkuu wake uliovunja rekodi kwa jinsi ulivyopangiliwa vyema na hatimaye ikagundulika kwamba kwa sasa chama hicho kina wanachama wenye kadi milioni 6 na nusu kutokana na operesheni yake ya Chadema ni Msingi iliyofanyika nchini kote kimyakimya kwa miaka miwili.
View attachment 1333871View attachment 1333872View attachment 1333873

Jr
 
Hajaitaja Chadema bwashee.

Kikwazo cha CCM kwa sasa ni ACT wazalendo Zanzibar.......huku bara upinzani umeshazikwa ndio maana serikali nzima ilihamia Zanzibar nyakati za sherehe za mapinduzi ili kuweka mambo sawa.
Ilihamia Mwanza kutoka na hofu
 
Ndio maana wanakuita vuvuzela! Mwenyekiti anaonyesha hadharani woga wake lakini wewe huna habari unakata mauno tuu kama Lugola?
Yeye ndiye anavyanzo vingi ndani ya chama na kesha jua kuwa ngoma inapasuka hivyo anatahadharisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Fahamu huyu anaandika chochote ili mkono uende kinywani
 
Wale wanaohama vyama malengo yao niya masilahi zaidi wasitegemee uchaguzi unaokuja watatoboa kupitia kura za debe wananchi watajali zaidi wagombea watakao watetea sio hao wanaojali zaidi matumbo yao.
Umenena ukweli mtupu
 
CCM ilishakufaga kitambo sana, aletete tume huru ya uchaguzi athibitishiwe kuwa hata yeye akubaliki, haya mengine ni kelele za alieshiba kupunguza gesi tumboni.
 
Wameanza lini kumbia? Muda mrefu sana

1. Kila wakati chama kinaimarika zaidi

2. Wapo waliosema 2020 hakifi, kimefika tena kwa tija.

Kumbia sio hoja,
Hoja ni jee kinaimarika? Kinapanuka na kutamalaki?
Mkutano Mkuu wa CDM mwaka jana umeacha kitisho kikubwa CCM
 
Kidumu Chama cha Mapinduzi

Kule Znz kuleee, inahitajika umakini Mkubwa sana kulinda Mapinduzi ya 1964, Tukifanya Mchezo au masihara yatanajisiwa maana jamaa safari hii Wako kimya sana mwaka huu wa Uchaguzi na hii si kawaida yao

Kuna harufu ya Usaliti visiwani
 
Back
Top Bottom