Rais Magufuli: Upinzani wa sasa umebadilika

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mwenyekiti wa CCM na Rais John Magufuli amekionya chama chake kisibweteke kwani upinzani wa sasa unatisha kutokana na mikakati yake

Akiwahitubia viongozi wa wilaya na mikoa kote nchini jijini DSM hapo jana Rais amesema wapinzani wa leo wamebadilika na wana mikakati ya hadharani na ya siri katika mapambano ya kutwaa madaraka

Ingawa Rais hakutaja chama chochote kwa jina lakini ni hivi karibuni chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kilifanya mkutano mkuu wake uliovunja rekodi kwa jinsi ulivyopangiliwa vyema na hatimaye ikagundulika kwamba kwa sasa chama hicho kina wanachama wenye kadi milioni 6 na nusu kutokana na operesheni yake ya Chadema ni Msingi iliyofanyika nchini kote kimyakimya kwa miaka miwili.
IMG-20200125-WA0022.jpg
IMG-20200125-WA0023.jpg
IMG-20200125-WA0021.jpg
 
Wewe na Kiongozi aliyesema nani anajua zaidi?
Hajaitaja Chadema bwashee.

Kikwazo cha CCM kwa sasa ni ACT wazalendo Zanzibar.......huku bara upinzani umeshazikwa ndio maana serikali nzima ilihamia Zanzibar nyakati za sherehe za mapinduzi ili kuweka mambo sawa.
 
Bwashee ndiyo nini?
 
Molemo,
Chadema hii hii iliyokimbiwa na madiwani wake juzi pale Arusha na kuhamia CCM?!!!

ACT wazalendo walau wana umakini kidogo!
Ndio maana wanakuita vuvuzela! Mwenyekiti anaonyesha hadharani woga wake lakini wewe huna habari unakata mauno tuu kama Lugola?
Yeye ndiye anavyanzo vingi ndani ya chama na kesha jua kuwa ngoma inapasuka hivyo anatahadharisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale wanaohama vyama malengo yao niya masilahi zaidi wasitegemee uchaguzi unaokuja watatoboa kupitia kura za debe wananchi watajali zaidi wagombea watakao watetea sio hao wanaojali zaidi matumbo yao.
 
Hajaitaja Chadema bwashee.

Kikwazo cha CCM kwa sasa ni ACT wazalendo Zanzibar.......huku bara upinzani umeshazikwa ndio maana serikali nzima ilihamia Zanzibar nyakati za sherehe za mapinduzi ili kuweka mambo sawa.
Mkuu ukiamka nikuambie tafsiri ya ndoto yako
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom