Rais Magufuli ni chaguo la Mungu amebeba maono ya nchi siyo CCM ni vema Chadema na wapinzani wamuunge mkono

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Kiukweli kila nikimtazama Rais Magufuli naona dhahiri amevuka level ya siasa za vyama na sasa anaitumikia nchi katika mustakabali mpana.

Kwa namna anavyoenenda ni ukweli ulio wazi Rais Magufuli anatumikia maslahi ya nchi japo kwa kuongozwa na Ilani ya CCM lakini kwa ubunifu binafsi wa kuleta maendeleo kwa haraka.

Nimetoka kuzipitia ilani za uchaguzi za ACT wazalendo, Nccr mageuzi, TLP, Chadema na Cuf ni dhahiri malengo yote ya maendeleo yaliyoainishwa kwenye ilani hizo yameshafikiwa.
Kwa upande wa ilani ya CCM ambayo imebeba mambo makubwa zaidi yenyewe imetekelezwa kwa takribani 99%

Sasa kwenye ubunifu binafsi hapo mwenye macho haambiwi tazama, miradi yote imeshika kasi na hapa ndipo wabunge wengi hata kama hawaipendi CCM lakini Juhudi za Rais Magufuli wameziona na kwa hiyari yao wameamua kumuunga mkono ama kupitia hiyo hiyo CCM au Nccr mageuzi na hata TLP.

TLP wao wameshamteua Dr Magufuli kuwa mgombea wao wa urais.

Nawatakia Sabato yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Wapi Azory, wapi Ben sanane wapi Mawazo?
Naunga mkono hoja.
 
Huyu jamaa hatari sana kawafanya,wapinzani kila uchao wanajimaliza wenyewe.Mabeberu nayo yanaweweseka kwa kumkosoa na kumsifia kwa wakati mmoja,

amini! amini! nawaambieni Mbowe ni ccm aongozaye chadema
 
Ukiwa Dar;

1. Unaweza sema nchi hii hakuna mtoto anaetembea uchi bila nguo.

2. Utapenda kusema nchi hii ajira za kumwaga wahitimu wanachagua kazi za kufanya.

3. Unaweza sema maji yanapatikana ya kutosha wamama na watoto hawakeshi wala hawatembei umbali mrefu kutafuta maji kwa ajili ya maisha yao.

4. Unajikuta tu ukiamini Dar ndio ina wasomi, watu maarufu, matajiri na viongozi wanaofaa kuiongoza Tanzania.

NB

Vijana nyinyi bado wa moto sana.
 
Back
Top Bottom