Rais akishachaguliwa siyo lazima afate Ilani ya Chama chake kwa sababu aliyechaguliwa ni yeye siyo Chama!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,036
Watu wengi hawalielewi na walimshangaa sana Magufuli alivyokuwa akitekeleza Ilani ya CHADEMA na ile ya ACT Wazalendo badala ya CCM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge na Madiwani wakishachaguliwa wanakuwa Watumishi wa Umma siyo Chama, kwasababu wanachaguliwa na Wananchi wote siyo Wanachama wa Vyama vyao pekee.

Chama ni mdhamini tu na kimsingi hii kanuni inapataga nguvu kwa vile hatuna sheria ya Mgombea Binafsi.

Nawakumbusha Viongozi wote wa kuchaguliwa Maono na Ubunifu wao ndio vitawafanya wachagulike 2025 hivi vyama vimeshapitwa na nyakati.

Ahsanteni sana 😄

Mtanishukuru 2026 panapo Uzima!
 
Siasa ina mambo mengi Mkuu.

Kuna watu wameshajiandalia ushindi mapema kabla ya kura kupigwa.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Kwa kuwa hatuna utaratibu wa mgombea binafsi na Kwa utaratibu uliopo Sasa Kiongozi yeyote wa kuchaguliwa anawajibika Kwa chama chake
 
Yaaani vijana wa hii nchi ni viazi sana yaani hasa vijana wenzangu wa ccm .Mimi mccm damu ila hizi siasa za kutafuta uteuzi zimeharibu kabisa vijana .

Jaman vijana wapinzani tafadhali vijana wa ccm tuliomakin tupo na kamwe msitujumuishe na wa aina hii.skuiz vijana hawapewi elimu ya siasa .yaan wanaamini rais ni mungu msaidizi.

Ukiniambia usheik mkuu au ukardinar ni maalumu ntakubali maana ni amethibitishwa na wengi anastahili.

Lakini uraisi ukishakuwa na degree na una miaka 40 na sio chizi .hata uwe na
-totoo mwili mzima
-mpagani
Kahaba.
Mlevi etc ilimradi apitishwe na Chama na ashawishi apite kwa kura.so asilimia 40 ya watu wote wanafaa kuwa marais

Turudi kwa upumbafu wa huyu kijana.
Bosi mkuu wa watanzania wote ni momoja tu anaitwa KATIBA Narudia KATIBA.sio ccm sio chadema sio yesu sio viongozi wa dini na sio rais(ndo maana huwa anaapishwa kumtii) na asipotii katiba imeelekeza jinsi ya kumfuta kazi.

Kwa mantiki hiyo rais hana uhuru wa kujiamulia anchotaka .Je kuhusu Ilani ya chama chake na uhuru wa rais kujifanyia lolote nje yake inasemaje?

Twende taratibu.Katiba inasema mamlaka zote zitatoka kwa wananchi.
Yaani serikali huwa hotel kubwa ambayo wenye hisa zote ni wananchi ambao pia ni wafanyakazi hotel hiyo.vyama huwa ni makundi madogo(vyama vya siasa) ya wafanyakazi ambayo huomba yapewe yawe management (kushika hatamu) ili yawavutie wanahisa huja na mpango wa utekelezaji wakiahidi maslahi yatapanda vipi ya wanahisa (wananchi) na hotel (nchi) .mpango huo ndo huwa wanajinadia (ilani ya chama ya uchaguzi) ndani yao huteuana nani atashika u CEO (URAIS) nani atakuwa mhasibu( waziri wa fedha) kwa kujuana uwezo wao .
Sasa kama una akili raisi hata akiwa anampa mtu uteuzi huwa anampa yafuatayo
1.Katiba ya nchi
2.Ilani ya uchaguzi wa ccm
2 .Barua ya kukasimiwa mamlaka .

Ina maana hata mtendaji hapaswi hoji ilani bali kuitekeleza .

ILANI HUTENGENEZWA NA NANI?
Chama cha kisiasa huwa kinahitaji kipendwe na kuaminiwa na wananchi ili kishike dola.

Siku miezi michache kabla ya uchaguzi vyama huzurula kwenye mijadala ya nini shida yao na huzurula kwa watafiti kujua waje na mpango gani kumaliza shida na matarajio ya wananchi.
Kisha chama huteua wataalamu wachache baada ya mijadala toka shina la mtaa hadi ngazi ya taifa na hata kimataifa(hata walionje huhojiwa)

Kisha chama huandaa kitabu cha mkakati na ahadi zao iwapo itapewa dhamana kwa kipindi kingine cha kutawala na kamati kuu hupitisha na kukigawa kwa wanachama wote .

Kisha chama huanzisha mchakato wa kusaka kwenye wanachama wake ni kina nani wakae nafasi gani kugombea ambao WANAUWEZO WAKUTEKELEZA ILANI YA CHAMA CHAO .
Tujikite kwenye urais tu sasa.chama hustisya wanachama wote wenye vigezo kuomba (kijana Soma tena KUOMBA) ridhaa(yaani mgombea hutia huruma kama kijana wa chuo anaomba kazi) Kisha huwapa nafasi ya kufanya jambo moja naliandika kwa herufi kuu
"KUELEZA NA KUONESHA UWEZO WAO WA KUTEKELEZA ILANI YA CHAMA KINACHOOMBWA RIDHAA"
Hebu usipotee hapa
Namaanisha mgombea huwa sio anaomba kusema maendeleo atavyoleta yeye au anavyoona sahihi NOOOO
Mgombea sio anakuwa sijui chaguo la mungu kuja kukomboa watanzania
NOOOO
Mgombea sio genius anaekuja na mikakati mipya
NOOOO
MGOMBEA URAISI NI MTU ANAYEOMBA KAZI KWENYE CHAMA CHAKE YA KUWA NAFASI YA RAISI KWENYE SELIKALI YA CHAMA HICHO KIKISHINDA.
YAANI CHAMA HAKIJAMLETA KUJA NA MIKAKATI YA KULETA MAENDELEO
NOOOO
KIMEMLETA KUTEKELEZA MIKAKATI YA CHAMA TUU AMBAYO INAITWA ILANI YA UCHAGUZI YA MWAKA HUSIKA..

Kwa hiyo magufuli kama ulivosema kwa kukosea et alitekeleza ilani ya chadema na act umeniangusha sana kama kijana wa ccm mwenzangu .kama alifanya hivo alikosea .
Ifahamike ilani ya uchaguzi ni list ya ahadi na utekelezaji waliyoingia mkataba CHAMA TAWALA NA WANANCHI.Rais ni mtekelezaji tu hapaswi kuhoji wala krekebisha maagizo toka kwa bosi wake.
Kwa kukuongezea huwa hakuna kitu kinachoitwa serikali ya mama Samia
NOOO
NI SERIKALI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.mama Samia ni mfanyakazi tu ila mkuu wa serikali hiyo kiprotocol.yaani kampuni iliyoshinda tenda ya ufagiaji bot ni CHAMA CHA MAPINDUZI ila wafagiaji kiongozi wao ndo RAIS.Je mfagiaj mkuu anaweza kopy sera za walioshindana tenda na ccm?
 
Watu wengi hawalielewi na walimshangaa sana Magufuli alivyokuwa akitekeleza Ilani ya CHADEMA na ile ya ACT Wazalendo badala ya CCM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wabunge na Madiwani wakishachaguliwa wanakuwa Watumishi wa Umma siyo Chama, kwasababu wanachaguliwa na Wananchi wote siyo Wanachama wa Vyama vyao pekee.

Chama ni mdhamini tu na kimsingi hii kanuni inapataga nguvu kwa vile hatuna sheria ya Mgombea Binafsi.

Nawakumbusha Viongozi wote wa kuchaguliwa Maono na Ubunifu wao ndio vitawafanya wachagulike 2025 hivi vyama vimeshapitwa na nyakati.

Ahsanteni sana

Mtanishukuru 2026 panapo Uzima!
Si kweli, wakati anaomba kura, alitumia ilani ya chama chake, aliinadi vyema wanannchi wakamuelewa, iweje tena apuyange na hamsini zake?
 
Back
Top Bottom