beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema ni sa aibu kuona shule za Zanzibar zinakuwa miongoni ambazo hazifanyi vizuri pindi inapofika wakati wa kutangaza matokeo ya Shule za Sekondari.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyopo visiwani Zanzibar.
Rais Magufuli amesema kuwa "Nasikitika sana wanapotangaza matokeo unakuta Shule za Zanzibar zinafuatana kuwa za mwisho hii ni aibu, viongozi mpige vita hii aibu, najua wengine hawawezi kuwaeleza mimi lazima nitawaeleza"
Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa "Nataka mpaka Machi kabla ya tarehe 30, jengo hili wanafunzi wawe wanaingia ndani, hii hela inayotumika hapa ni hela ya Wazanzibar na watailipa, nakuomba Mkandarasi ukamilishe kwa wakati, Katibu Mkuu marufuku kuwatetea Wakandarasi"
"Tunakopesheka kwasababu sisi ni Matajiri tusingekuwa na uwezo wa kulipa tusingekopeshwa, mpaka March jengo hili wanafunzi wawe wanaingia, hela inayotumika hapa ni ya Wanzanzibar na watailipa, Katibu Mkuu marufuku kuwatetea Wakandarasi wakikupa 10% kula ila simamia Sheria”-JPM
Kwa sasa Rais Magufuli yuko visiwani Zanzibar kwa ajili ziara ya kikazi ambapo kesho atashiriki Sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.