Rais Magufuli: Ni aibu Shule za Zanzibar kuwa za mwisho, Wakandarasi wakikupa 10% kula ila simamia Sheria

Kabla ya mapinduzi Zanzibar ilikuwa ya kwanza kielimu Afrika Mashariki na ya kati kama si Afrika nzima.

Elimu mpaka vifaa vyote vya elimu pamoja na uniform za wanafunzi ilikuwa bure.
Reference tafadhali
 
Kwa hiyo tusikamate wapokea rushwa Bali tuangalie kwanza matokeo.
Kama umepokea 10% tunasubiri tuone, ukifuata sheria basis ruksa hiyo 10% kuwa huru kwako. Ole wako tukigundua hujasimamia sheria basi ile 10% uliyochukuwa lazima tukukamue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jpmmmm.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema ni sa aibu kuona shule za Zanzibar zinakuwa miongoni ambazo hazifanyi vizuri pindi inapofika wakati wa kutangaza matokeo ya Shule za Sekondari.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mwanakwerekwe iliyopo visiwani Zanzibar.

Rais Magufuli amesema kuwa "Nasikitika sana wanapotangaza matokeo unakuta Shule za Zanzibar zinafuatana kuwa za mwisho hii ni aibu, viongozi mpige vita hii aibu, najua wengine hawawezi kuwaeleza mimi lazima nitawaeleza"

Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa "Nataka mpaka Machi kabla ya tarehe 30, jengo hili wanafunzi wawe wanaingia ndani, hii hela inayotumika hapa ni hela ya Wazanzibar na watailipa, nakuomba Mkandarasi ukamilishe kwa wakati, Katibu Mkuu marufuku kuwatetea Wakandarasi"

"Tunakopesheka kwasababu sisi ni Matajiri tusingekuwa na uwezo wa kulipa tusingekopeshwa, mpaka March jengo hili wanafunzi wawe wanaingia, hela inayotumika hapa ni ya Wanzanzibar na watailipa, Katibu Mkuu marufuku kuwatetea Wakandarasi wakikupa 10% kula ila simamia Sheria”-JPM

Kwa sasa Rais Magufuli yuko visiwani Zanzibar kwa ajili ziara ya kikazi ambapo kesho atashiriki Sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hela ya wazanzibar au watanzania ?
 
Elimu haina hamasa yoyote.
Tangu 2016 hakuna ajira mpya kwa kada nyeti halafu uwashauri wafauru.
Elimu haina tena manufaa yaliyomo katika imani na misingi yake(yaani matumizi yake katika kukabili changamoto za kimaisha)
ELIMU ISIYO NA AJIRA,NANI AHANGAIKE NAYO?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani lazima uajiriwe? Kwani huwezi kujiajiri?
 
Kabla ya mapinduzi Zanzibar ilikuwa ya kwanza kielimu Afrika Mashariki na ya kati kama si Afrika nzima.

Elimu mpaka vifaa vyote vya elimu pamoja na uniform za wanafunzi ilikuwa bure.
Elimu ya mkoloni au mwingereza sio?
 
Kabla ya mapinduzi Zanzibar ilikuwa ya kwanza kielimu Afrika Mashariki na ya kati kama si Afrika nzima.

Elimu mpaka vifaa vyote vya elimu pamoja na uniform za wanafunzi ilikuwa bure.
Ningeshangaa wewe kutochangia huu uzi... Kumbuka huyo ni Rais wetu kwahiyo amewatembelea nyie nchi jirani na sasa anawakumbusha ilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom