Jakaya Kikwete aongoza Hafla ya Kutambua Mchango wa wadau kwenye Sekta ya Elimu, leo Agosti 31, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Fuatilia yanayojiri kwenye Hafla ya Kutambua Mchango wa wadau kwenye Sekta ya Elimu, leo Agosti 31, 2023 ambapo Rais Mstaafu wa Awamu ya 4, Jakaya Kikwete ni Mgeni rasmi.



Rais msitaafu Jakaya Kikwete ambaye ni Mgeni rasmi katika Hafla hiyo, amewapongeza Wizara ya Elimu kwa kubuni wazo la kutambua mchango wa wadau kwenye Sekta ya Elimu.

Hafla hii inawaleta pamoja wadau wa ndani na nje kuchangia Sekta ya Elimu. Itawezesha Serikali kukamilisha maombi yanayotolewa kama Motisha.

Taasisi ya Global Partnership for Education (GPE) ambayo Jakaya Kikwete ndiye Mwenyekiti wake, inatoa mchango wa dola moja kwa kila dola moja iliyochangiwa( Wadau wa Elimu wakichanga mfano dola 10 na GPE inatoa Dola 10 kama msaada) .

Kkwete amesema Shirika la GPE lilianzishwa miaka 20 iliyopita na Nchi za G7 ikiwa lengo ni kusaidia elimu msingi ya Chekechea, Shule za Msingi na Sekondari kwa nchi zenye mapato ya chini, zilizokumbwa na Vita mfano Ukraine na Afghanistan na zile zilizoathrika na Mabadiliko Tabia nchi. Na sharti moja wapo ya ili upate msaada ni kuzingatia usawa wa kijinsia.Ukibagua wasichana, hupati fedha za GPE.


Mwenyekiti wa Bodi ya GPE yenye Wajumbe 40 Dk. Kikwete ni Mwenyekiti amesema Desemba mwaka huu wanatarajia kufanya mkutano wa Bodi Visiwani Zanzibar Tanzania, itakuwa ni mara ya kwanza.

Kikwete amefafanua pia ili upate hela za GPE ni pale unaposamehewa mkopo kwa ahadi ya huo msamaha ili hela anbaye mngelipa mkaipeleka kwenye Elimu, basi kila Dola tatu GP inachangia dola moja. Kwahiyo akaomba Nchi iongee na wanaowadai wafutiwe mkopo ili hiyo hela ielekezwe kwenye Elimu. GPE itawaongezea dola moja kwa kila Dola tatu itakayosamehewa. Ametoa mfano kwamba Ivory Coast ilisamehewa Milioni 72 na Ufaransa, GPE ikiwapa Milioni 24 ambayo iliwafanya wawe na Milioni 96 ambazo walielekeza kwenye elimu.

GPE duniani inasaidia nchi 78 zikiwepo Syria Afghanistan na Ukraine.

Kipindi cha COVID-19, GPE ilitoa Msaada Dola Milioni 500 kwa Nchi 66 ambapo Tanzania ilipata Dola Milioni 15 kuwawezesha watoto kusoma kipindi cha COVID-19.

Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kazi kubwa ya hafla hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na TAMISEMI na wadau mbalimbali kuchangia sekta ya elimu.

“Sera ya elimu na mafunzo mwaka 2014 tuliangalia mambo ya msingi ambayo yamewekwa hayajafanyiwa kazi ikiwemo elimu ya msingi itakuwa miaka sita na minne sekondari jumla 10 anamaliza shule akiwa na miaka 16,”amesema Prof. Mkenda.

Amesema sera ya mwaka 2014 wapo kwenye mchakato watapeleka ipitishwe bungeni na mapendekezo mwezi ujao yatapishwa na baade kutangazwa.

Profesa Mkenda amesema lengo kubwa ni kuboresha elimu nchini na katika kuendeleza elimu kuna hitaji gharama wadau mbalimbali wakutane kuchangia.

Mgeni Rasmi Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwa ajili ya hafla ya kutambua Mchango wa Wadau wa Sekta ya Elimu iliyofanyika Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo Agosti 31, 2023.

857262341.jpg
26589003.jpg
1567391325.jpg
-1731870454.jpg
-431019611.jpg
651344936.jpg
1339422317.jpg
 
Back
Top Bottom