Haki yyt inatakiwa iendane na wajibu. Je unafikiri kwa kauli zinazotolewa na wapinzan zinaakisi UZALENDO DHIDI YA SERIKALI NA NCHI YAO?Wengi wanadai haki lkn wajibu hawajui uko vipi.Kila mtu anahaki ya kutoa maoni bila kuingiliwa na mtu yyt.lkn je nini wajibu wake ktk kutoa maoni?Je anatimza wajibu wa kulinda heshima ya mtu?Je anatimiza wajibu wa kuhakikisha haleti sintofaham ktk jamii?Mtu anaulizwa nini kazi za chama cha UPINZANI anajibu ni kuwachochea wananchi waione SERIKALI yao haifai,kweli?Kiongoz kama huyu anadai haki ya mikutano ya kisiasa.
Kingine Mbunge kachaguliwa awatetee wananchi wa Jimbo lake lkn pia anaweza kuwatetea wananchi nje ya Jimbo lake.Mbunge jimbo lake la kawe linashida tele,badala ya kupambana awasaidie yy analilia kwenda kufanya mkutano mbeya. Ni vitu vya ajabu.Kwanini kila mbunge asisimame kwenye Jimbo lake kila siku apaze sauti kuwapigania wananchi wake na kushirikiana ktk kutatua changamoto zaid anataka aende Arusha akafanye siasa?Kuna mattz yanahitaji utashi wa mbunge na wananchi ili kuyatatua,kwanini hawafanyi hivo kila siku wako DAR kukimbizana na POLISI?Shule haina choo,mbunge anahimiza kila mwananchi aje na tofari mbili kwa ajili ya ujenzi,inashindikana nn?Au hapo panahitaji uende kwenye majukwaa ndio upige kelele?
Yako mengi sana.mimi naona wanaolilia mikutano ya kisiasa hawana hoja za mcng ktk kumkomboa mtanzania zaid ya kujinufaisha wao kisiasa. Umeambiwa piga siasa kwenye Jimbo lako,we hutak unataka uende kwenye Jimbo la mwenzio. Kwamba Jimbo lako mattz hamna?Kwamba Jimbo lako huwezi kusikilizwa au sababu ya mcng mbunge kulilia kupiga siasa kwenye Jimbo la mwenzie ni nn?