Rais Magufuli: Majizi yamehamia CHADEMA

Rais Magufuli: Majizi yamehamia CHADEMA

Ni kweli kabisa majizi yamehamia huko
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba jijini Mwanza na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini.

“Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele” alisisitiza Rais Magufuli

======

My Take:
Eti sasa anasema majizi yame hamia CHADEMA!!!!! Aibu kubwa hii....

Hivi Magufuli anatuchukuliaje Watanzania??

Yaani mko na mafisadi na bado mkasema mahakama ya mafisadi imekosa kesi?????? Aibu kubwa hii.....

Nyie endelezi kasi ya chuki na dhuluma by the time mnaamka usingizini mmebak wawili.

Anaendelea na kampeni...
 
Hahahahahaaaa Wenye JALALA lazima wahitaji TAKA ili JALALA liwepo.Kwao TAKA ni FAIDA na WATAZIFURAHIA[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]...big up PREZIDAA.
 
NIMEGUNDUA KWAMBA MAGUFULI AMEKATA TAMAA KUPAMBANA NA HAO MAJIZI YALIYOTOKA CCM KWENDA CHADEMA.
NI AIBU KUSEMA ETI CCM KUNA MAJIZI.
WEWE KAMA RAIS UMECHUKUA HATUA GANI DHIDI YA HAO MAJIZI?
 
Tuna raisi wa ajabu kupata kutokea toka uhuru. Kwa Mara nyingine anakiri wazungu wa barick ni majizi Ila wamefikia makubaliano na hayo majizi. Kwa mara nyingine ametamka kuwa wanakimbili chadema ni majizi. Yaani ukitaka uitwe mwizi hama ccm uende chadema!
 
Kuna chuki inajengwa ya kiitikadi ya vyama ikiiva watakula matunda,hawatoamini busara ni muhimu kutangulizwa katika kila jambo
 
Naomba nijue idadi ya kesi ktk mahakama ya mafisadi na vyama wanavyotokea halafu nitarudi kutoa maoni
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba jijini Mwanza na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini.

“Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele” alisisitiza Rais Magufuli

======

My Take:
Eti sasa anasema majizi yame hamia CHADEMA!!!!! Aibu kubwa hii....

Hivi Magufuli anatuchukuliaje Watanzania??

Yaani mko na mafisadi na bado mkasema mahakama ya mafisadi imekosa kesi?????? Aibu kubwa hii.....

Nyie endelezi kasi ya chuki na dhuluma by the time mnaamka usingizini mmebak wawili.

hivi wapinzani wangesema hii kauli si wangekuwa washazungushwa vituo vyote vya polisi dar, inachekesha kweli yani, wakisema wao ni poa wakisema wapinzani wanaambiwa wachochezi, sasa uchochezi wao siujui kama ni uchochezi wa maendeleo au ni uchochezi wa aina gani
 
Back
Top Bottom