Rais Magufuli: Majizi yamehamia CHADEMA

Rais Magufuli: Majizi yamehamia CHADEMA

Anasema majizi yamehamia CHADEMA. Hii kauli inatoka kwa Rais wa nchi.

Ina maana wezi anawajua na hawachukulii hatua yoyote?

Pia anasema "Tanzania Oyee" na hana uchama na anaona vyama vinamchelewesha akitaka tushikamane.

Upande wa pili yeye ni mwenyekiti wa CCM. Kama hapendi mambo ya chama ajivue uenyekeiti, aende mbele zaidi na kufuta vyama vya siasa ili tusichelewe. Anawapa madaraka wale wote wanaopambana na upinzani. Huu ni unafki wa hali ya juu.

Pia anasema amewabana wezi wazungu. Hakuna mwizi wa kizungu amefikishwa mahakamani mpaka sasa. Wamesema wanatupa 0.16% ya tunachowadai. Na wanatupa in "good faith". Sasa wewe unamdai mtu na anakupa 0.16% ya unachodai na unasema umembana? Huyu si mzima kichwani.

Anatumia nguvu sana kuongea na kujieleza. Hii ni sifa ya mtu anayeongea kutokana na hisia zake na si maarifa. Kuongozwa na hisia ni kuzama kwenye shimo.
 
Chadema ni kikapu cha majizi...no other way of puting it...hamjajifunza 2015...
 
hahahahaha hata nasari alishasema Nyalandu ni fisadi
 
Nimemuelewa inamaana kwa kauli yake hii CCM kwasasa haina majizi wamekwisha ,ni safi kabisa.

Sasa tuje kuwasikia mnaropoka tena siku mbunge mwingine kahamia chadema kwamba ni mwizi
Hayanaga aibu
 
CCM ni mtambo wa kuzalisha mafisadi ndiyo maana nchi inazidi kuzama katika lindi la umasikini chini ya utawala dhalimu wa ccm.
 
Back
Top Bottom