Sheria mpya usalama barabarani: Mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya usalama barabarani sura ya 168

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,260
2,000
MAPENDEKEZO YA MABADILIKO YA SHERIA YA USALAMA BARABARANI SURA YA 168

Utangulizi
Leo 13.10.2017, kikao cha taasisi wadau wa usalama barabarani kimepokea na kutoa maoni juu ya mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya usalama barabarani sura ya 168, kama yanavyotarajiwa na serikali. Kikao kiliitishwa na Wizara ya mambo ya ndnai ya nchi. Haya hapa chini ni baadhi ya mapendekezo ya serikali katika kuboresha sheria hiyo.

Mapendekezo
1. Kifungu cha 5(1) Msajili atakuwa na mamlaka ya kusajili magari na kuhifadhi data base ya kieletroniki ya magari ili kuendana na mfumo wa faini za kielektroniki na leseni mpya.

2. Kifungu cha 8(2) inapendekezwa faini ya kutumia gari bila usajili kuwa shilingi 100,000/- na isiyozidi 500,000/

3. Kifungu cha 10(2) inapendekezwa mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 asiruhusiwe kumiliki gari.

4. Kifungu cha 13(2) inapendekezwa mtu ambaye hatakuwa na kadi ya usajili kwenye gari lake adhabu yake iwe kiasi kisichopoungua shilingi 50,000 na kisichozidi 100,0000

5. Kifungu cha 14(5) inapendekezwa mtu yeyote atakayeficha au kuharibu au kutoweka alama za utambulisho wa gari adhabu yake iwe kati ya shilingi 500,000 na 1000000.

6. Kifungu cha 18, inapendekezwa kuwa mtu yeyote ambaye atashindwa kusajili mabadiliko ya umiliki wa gari adhabu yake isipungua shilingi 500,000

7. Kifungu cha 19, inapendekezwa kuwa mtu yeyote atakayekutwa barabarani akiendesha gari bila kuwa na leseni halali kwa gari analoliendesha adhabu yake iwe ni faini kuanzia shilingi 100,000 na isiyozidi 300,000.

8. Kifungu cha 21(1) inapendekezwa kuwa mtu anayetaka kujifunza kuendesha pikipiki akate lesnei ya lena

9. Kifungu cha 23(3) inapendekezwa kufutwa kwa kipengele kinachomruhusu msajili kumpa mtu leseni ya udereva kutokana na uzoefu hata kama hata leseni ya udereva au ya lena na badala yake msajili anapewa mamlaka ya kubadilishia leseni mtu yeyote mwenye leseni iliyotolewa na nchi yoyote ya jumuiya ya madola, na kumpa leseni ya Tanzania

10. Kifungu cha 23(7) inapendezwa kumwajibisha afisa yeyote wa serikali au mtu yeyote aliyejihusisha katika kufanya udanganyifu wa kumtafutia mtu leseni ya udereva ambaye hana sifa stahili, na dhabu yake iwe kati ya shilingi 500,000 na 1,000,000/

11. Kifungu cha 27(1) inapendekezwa kufuta namba 40 inayojitokeza katika kifungu kidogo cha kwanza cha aya ya a-d. Pia inapendekezwa kipengele 'h' kifutwe chote. Lengo ni kutofautisha uzito wa makosa ili madereva hatari(dangerous drivers) wapewe adhabu kali Zaidi wakati wale wale madereva wapuuzi (careless or reckless drivers) wapate adhabu ya chini kidogo (less severe). Kufutwa kwa kipengele h ni kwa sababu kifuchu cha 44 hadi 49 kinahusu makosa yanayohusiana na ulevi;

12. Kifungu cha 27(2) inapendekezwa kifungu kidogo cha 2 kirekebishwe na kumlazimisha mtuhumiwa kurejesha leseni yake polisi baada ya kufungiwa.

13. Kifungu cha 28(1) inapendekezwa kufuta mamlaka ya kujiamulia kadiri hakimu anavyoona inafaa (discretionary powers) kwa kufuta neno discretionary linalotokeza kwenye kifungu hicho na kulibadilisha na neno (shall) ili kumlazimisha hakimu afungie leseni au kuifuta kwa kipindi husika;

14. Kifungu cha 28(4) inapendekezwa kifutwe kwakuwa kwa sasa endorsement ya leseni inafanyika kieletroniki

15. Kifungu cha 29 inapendekezwa kifutwe kwakuwa kinahusu leseni za makaratasi

16. Kifungu cha 30 inapendekezwa kirekebishwe kwa sababu ya kifungu cha 28 na 30 ili kuondoa cross reference, badala yake kisomeke “rufaa itaruhusiwa dhidi ya uamuzi uliotolewa chini ya kifungu cha 27 kwa njia ile ile kama rufaa dhidi ya hokum, na ikiwa rufaa imekatwa mahakama iliyotoa amri au ile ambako rufaa inapelekwa itasimamisha leseni huku rufaa ikisubiriwa kusikilizwa”

17. Kifungu cha 31(4) na (5) kinapendekezwa kurekebishwa ili kuondoa rejea inayofanywa na kifungu cha 29

18. Kifungu cha 32 kinarekebishwa ili kuenda a na mfuo wa kanzidata (database)

19. Kifungu cha 36(c) kinarekebishwa ili kijumuishe na kutambua leseni za nchi zote za jumuiya ya afrika mashariki

20. Kifungu cha 37 kinapendekezwa kurekebishwa ili mtu yeyote anayetaka kuwa mwalimu wa udereva awe na cheti cha ualim wa udereva (instructor’s certificate) na mtu yeyote atakayekutwa akifundisha mtu kuendesha gari bila kuwa na cheti hicho adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi 500,000.

21. Kifungu cha 39(11) na (12) inapendekezwa virekebishwe ili kumlazimisha abiria wa pikipiki kuvaa helmeti, na pia kulazimisha kila abiria afunge mkanda kukaa kiti cha mbele cha abiria na kuweka sharti la gari kuwa na vizuizi vya watoto (child restraint). Na pia kuweka adhabu kwa gari lolote kujaza mafuta kituoni huku likiwa na abiria.

22. Kifungu cha 40(1) kinarekebishwa ili kuweka sharti la kukataza dereva kuongea na simu wakati akiendesha. Adhabu inayopendkezwa kwa kosa hili kama ni kuandika message faini iwe shilingi 200,000

23. Kifungu kipya cha 41A kinapendekezwa kuongezwa ili mtu yeyote anayesababisha majeruhi au kifo kutokana na kuendesha pikipiki, guta, bajaji au basikeli awe ametenda kosana kutiwa hatiani, kama ambavyo dereva wa gari anatiwa hatiani.

24. Kifungu cha 43(1) kinapendekezwa kurekebishwa ili kuondoa neno obstruct na kulibadilisha na neno interfere

25. Inapendekezwa kuongeza kifungu cha 43(6) ili kuwabana watu wote wanaosababisha au kuzuia (hinder, obstruct or impede) magari mengine kutembea barabarani na matokeo yake kusababisha foleni, na dhabu yake inapendekezwa kuwa kati ya shilingi 50,000 na 100,000 au kifungo jela miezi 6;

26. Kifungu cha 45, inapendekezwa faini kwa makosa ya ulevi ianzie shilingi 500,000;

27. Kifungu cha 46(4) inapendkezwa mtu yeyote ambaye atakataa kupimwa ulevi ahesabike kuwa amelewa kupita kiasi;

28. Kifungu cha 49, inapendekezwa kiwango cha ulevi kishuke hadi kufikia 0.50BAC(Blooc Alcohol Concentration) kuliko kiwango cha sasa cha 0.80/100mls

29. Kifungu cha 56 inapendekezwa kuongeza adhabu kwa dereva anayeendesha kwa mwendo wa chini sana bila sababu ya msingi (unreasonably slowly) kuwa shilingi 50,000

30. Kifungu cha 57(7), inapendekezwa kuongeza kifungu kinachomtaka mmiliki wa gari lililopata ajali kumtafuta dereva wa gari hilo aliyesababisha ajali na kukimbia na kumfikisha polisi. Inapendekezwa mmiliki atakayeshindwa kufanya hivyo atozwe faini isiyopungua shilingi 500,000

31. Kifungu cha 58, inapendekezwa kuongeza kifungu kidogo cha 3 kuzuia gari za mizigo kubeba abiria

32. Kifungu cha 59 inapendekezwa kuweka adhabu kali kwa wanaopanda na kupakia mishkaki kuwa faini ya shilingi 100,000

33. Kifungu cha 61, inapendekezwa kifungu hiki kiwekewe adhabu kali kwa watu wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuharibu mali za watu hususani bodabodas, ikibidi kuwepo adhabu ya fidia.

34. Kifungu cha 62(1) inapendekezwa kifungu kirekebishwe kwa kuongeza adhabu kwa watu wasio madereva wanaopatikana wakiendesha magari bila ridhaa ya wamiliki wa gari. Hivyo adhabu isipungue shilingi 500,000 na isizidi 1,000,000

35. Kifungu cha 63(2) inapendekezwa kuongeza adhabu kwa makosa chini ya kifungu cha 40 yaani pamoja na kifungo cha miaka mitatu jela mtuhumiwa alipe faini isiyopungua shilingi 2,000,000 kwa kuendesha gari kwa njia ya hatari (dangerous driving)

36. Kifungu cha 77(1) inapendekezwa kuondoa mda wa saa 72 anaopewa dereva kuonesha leseni yake badala yake dereva apewe saa 24 tu kuonesha leseni, na ndani ya saa hizo 24 aliache gari lake kituo cha polisi hadi atakapooonesha leseni.

37. Kifungu cha 84(1) inapendekezwa kifungu kirekebishwe ili kupunguza muda anaopewa dereva aliyelitelekeza gari kuliondoa gari hilo barabarani au kwenye road reserve toka siku tatu hadi saa 24, hivyo askari aruhusiwe kuliondoa mara moja

38. Kifungu cha 85(4) inapendekezwa adhabu kwa mtu anayeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuondoa gari lililoharibika barabarani adhabu yake isipungue shilingi 100,000

39. Kifungu cha 113(1) (kosa na.23)inapendekezwa adhabu ipande kutoka 2,000 hadi 50,000 ya sasa hadi kuwa kati ya shilingi 50,000 na 100,000

ZINGATIA
Adhabu hizi ni zile zitakazokuwa zikitolewa na mahakama mtu akifikishwa mahakamani na kukutwa na hatia, na sio adhabu za papo kwa papo barabarani. Aidha haya ni mapendekzo ya awali kabisa (first draft) ambapo serikali itaendelea kukusanya maoni. Hivyo baada ya kuona mapendekezo hay ahata wewe unaruhusiwa kutoa maoni juu ya mapendekezo haya au kushauri kingine chochote unachoona chafaa kurekebishwa kwenye sheria ya usalama barabarani.
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,814
2,000
wataalamu wa sheria labda mtusaidie hapo inaposemwa "adhabu zitatolewa mtu akifikishwa mahakamani tu" je hawa wa barabarani wao wanatakiwa watoe adhabu gani?

Kipengele cha kuongea na simu, hapa panaweza kuleta shida sana hasa kwa wale polisi wasio waaminifu aka walarushwa maana ushahidi kwenye hili ni mgumu sana...
 
kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
5,929
2,000
Hii sheria ya ku- limit speed 80 km/h highway na 50km/h kwenye makazi iangaliwe upya. watu tunachelewa sana kufika. Mfano sasa ivi toka dar mpk arusha/dom au mwanza hakuna mapori ni makazi ya watu njia nzima. At least iachwe 120 kwenye sehemu ambazo hazina makazi ya watu au mbuga. otherwise izo faini nimezipenda
 
Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,502
2,000
Hizo adhabu mbona za kukomoana? Hivi kwann tunafikiria faini kubwa ndo kutibu makosa yasitokee? Au ndo kuongeza makusanyo ya maduhuli ya serikali kupitia barabara
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
6,862
2,000
sheria ya kuongeza mapato¡! hali tete sana naona mapato yanatafutwa kwa hali na mali
 
R Mbuna

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,184
2,000
Hizo adhabu mbona za kukomoana? Hivi kwann tunafikiria faini kubwa ndo kutibu makosa yasitokee? Au ndo kuongeza makusanyo ya maduhuli ya serikali kupitia barabara
Hapo ni mwendo wa kuongeza mapato ya nchi mkuu.

Adhabu zingekuwa vifungo au kufanya shughuli za kijamii ili watu wapate kujitambua tungejua kweli wanania ya kuleta maendeleo ya utii wa sheria bila shuruti.
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,762
2,000
Dawa ni kupaki magari na kutumia public transport, weekend unapoenda shambani ndiyo unatumia gari yako tuone hata hiyo kodi ya mafuta wataipataje
 
number41

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,018
2,000
Mbona akuna sheria ya ikiwa gari yng imewekwa kizuizini kwa muda then nikalipa fidia nikikuta vitu vyangu vimeibiwa polisi atausika kunilipa au sheria sio msumeno ni jino la mbwa unyofoa mtu wa mtu tu na sio wake
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,795
2,000
Leo 13.10.2017, kikao cha taasisi wadau wa usalama barabarani kimepokea na kutoa maoni juu ya mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya usalama barabarani sura ya 168, kama yanavyotarajiwa na serikali. Kikao kiliitishwa na Wizara ya mambo ya ndnai ya nchi. Haya hapa chini ni baadhi ya mapendekezo ya serikali katika kuboresha sheria hiyo.
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,795
2,000
5. Kifungu cha 14(5) inapendekezwa mtu yeyote atakayeficha au kuharibu au kutoweka alama za utambulisho wa gari adhabu yake iwe kati ya shilingi 500,000 na 1000000.

Msaada hapa: alama za utambulisho ni kama zipi?

8. Kifungu cha 21(1) inapendekezwa kuwa mtu anayetaka kujifunza kuendesha pikipiki akate lesnei ya lena

Je tunao askari wa kutosha kulisimamia hili? isijekuwa ni mwanya mwingine wa kuwapa askari rushwa kutokana na wingi wa vijana wanaojifunza pikipiki vichochoroni

21. Kifungu cha 39(11) na (12) inapendekezwa virekebishwe ili kumlazimisha abiria wa pikipiki kuvaa helmeti, na pia kulazimisha kila abiria afunge mkanda kukaa kiti cha mbele cha abiria na kuweka sharti la gari kuwa na vizuizi vya watoto (child restraint). Na pia kuweka adhabu kwa gari lolote kujaza mafuta kituoni huku likiwa na abiria.

Lakini kila kukicha tunashuhudia kikosi cha usalama barabarani kikishindwa kuwachukulia hatua madereva wanaozidisha abiria kwenye mabasi na na hawana wala hawafungi mikanda ya usalama je sheria hizi zinamsaada gani kama hazisimamiwi

38. Kifungu cha 85(4) inapendekezwa adhabu kwa mtu anayeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuondoa gari lililoharibika barabarani adhabu yake isipungue shilingi 100,000

Je kile kikosi cha road patrol hawaoni magari yanakaa barabarani zaidi ya wiki mbili yakiwa yameharibika na wala hawachukui hatua, au siyo kazi yao?

2. Kifungu cha 27(2) inapendekezwa kifungu kidogo cha 2 kirekebishwe na kumlazimisha mtuhumiwa kurejesha leseni yake polisi baada ya kufungiwa

Nashauri leseni zinazorejeshwa ziorodheshwe kwenye gazeti la serikali ili kuepusha rushwa, maana leseni ikirejeshwa kimyakimya siku ya pili dereva anatoa rushwa na kurejea barabarani na matokeo yake ajali haziishi

7. Kifungu cha 19, inapendekezwa kuwa mtu yeyote atakayekutwa barabarani akiendesha gari bila kuwa na leseni halali kwa gari analoliendesha adhabu yake iwe ni faini kuanzia shilingi 100,000 na isiyozidi 300,000.

Je kwa dereva aliyesahau leseni nyumbani kwa bahati mbaya haki zake kwa sasa ni zipi maana unakuta askari wa usalama barabarani wanaandika fine straight away
 
JWKRMM

JF-Expert Member
Sep 17, 2017
1,561
2,000
Hizo adhabu mbona za kukomoana? Hivi kwann tunafikiria faini kubwa ndo kutibu makosa yasitokee? Au ndo kuongeza makusanyo ya maduhuli ya serikali kupitia barabara
Kwani wewe unapanga kuvunja sheria mojawapo kati ya zilizotajwa.
 
Augustoons

JF-Expert Member
Oct 31, 2007
411
195
MAPENDEKEZO YA MABADILIKO YA SHERIA YA USALAMA BARABARANI SURA YA 168

Utangulizi
Leo 13.10.2017, kikao cha taasisi wadau wa usalama barabarani kimepokea na kutoa maoni juu ya mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya usalama barabarani sura ya 168, kama yanavyotarajiwa na serikali. Kikao kiliitishwa na Wizara ya mambo ya ndnai ya nchi. Haya hapa chini ni baadhi ya mapendekezo ya serikali katika kuboresha sheria hiyo.

Mapendekezo
1. Kifungu cha 5(1) Msajili atakuwa na mamlaka ya kusajili magari na kuhifadhi data base ya kieletroniki ya magari ili kuendana na mfumo wa faini za kielektroniki na leseni mpya.

2. Kifungu cha 8(2) inapendekezwa faini ya kutumia gari bila usajili kuwa shilingi 100,000/- na isiyozidi 500,000/

3. Kifungu cha 10(2) inapendekezwa mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 asiruhusiwe kumiliki gari.

4. Kifungu cha 13(2) inapendekezwa mtu ambaye hatakuwa na kadi ya usajili kwenye gari lake adhabu yake iwe kiasi kisichopoungua shilingi 50,000 na kisichozidi 100,0000

5. Kifungu cha 14(5) inapendekezwa mtu yeyote atakayeficha au kuharibu au kutoweka alama za utambulisho wa gari adhabu yake iwe kati ya shilingi 500,000 na 1000000.

6. Kifungu cha 18, inapendekezwa kuwa mtu yeyote ambaye atashindwa kusajili mabadiliko ya umiliki wa gari adhabu yake isipungua shilingi 500,000

7. Kifungu cha 19, inapendekezwa kuwa mtu yeyote atakayekutwa barabarani akiendesha gari bila kuwa na leseni halali kwa gari analoliendesha adhabu yake iwe ni faini kuanzia shilingi 100,000 na isiyozidi 300,000.

8. Kifungu cha 21(1) inapendekezwa kuwa mtu anayetaka kujifunza kuendesha pikipiki akate lesnei ya lena

9. Kifungu cha 23(3) inapendekezwa kufutwa kwa kipengele kinachomruhusu msajili kumpa mtu leseni ya udereva kutokana na uzoefu hata kama hata leseni ya udereva au ya lena na badala yake msajili anapewa mamlaka ya kubadilishia leseni mtu yeyote mwenye leseni iliyotolewa na nchi yoyote ya jumuiya ya madola, na kumpa leseni ya Tanzania

10. Kifungu cha 23(7) inapendezwa kumwajibisha afisa yeyote wa serikali au mtu yeyote aliyejihusisha katika kufanya udanganyifu wa kumtafutia mtu leseni ya udereva ambaye hana sifa stahili, na dhabu yake iwe kati ya shilingi 500,000 na 1,000,000/

11. Kifungu cha 27(1) inapendekezwa kufuta namba 40 inayojitokeza katika kifungu kidogo cha kwanza cha aya ya a-d. Pia inapendekezwa kipengele 'h' kifutwe chote. Lengo ni kutofautisha uzito wa makosa ili madereva hatari(dangerous drivers) wapewe adhabu kali Zaidi wakati wale wale madereva wapuuzi (careless or reckless drivers) wapate adhabu ya chini kidogo (less severe). Kufutwa kwa kipengele h ni kwa sababu kifuchu cha 44 hadi 49 kinahusu makosa yanayohusiana na ulevi;

12. Kifungu cha 27(2) inapendekezwa kifungu kidogo cha 2 kirekebishwe na kumlazimisha mtuhumiwa kurejesha leseni yake polisi baada ya kufungiwa.

13. Kifungu cha 28(1) inapendekezwa kufuta mamlaka ya kujiamulia kadiri hakimu anavyoona inafaa (discretionary powers) kwa kufuta neno discretionary linalotokeza kwenye kifungu hicho na kulibadilisha na neno (shall) ili kumlazimisha hakimu afungie leseni au kuifuta kwa kipindi husika;

14. Kifungu cha 28(4) inapendekezwa kifutwe kwakuwa kwa sasa endorsement ya leseni inafanyika kieletroniki

15. Kifungu cha 29 inapendekezwa kifutwe kwakuwa kinahusu leseni za makaratasi

16. Kifungu cha 30 inapendekezwa kirekebishwe kwa sababu ya kifungu cha 28 na 30 ili kuondoa cross reference, badala yake kisomeke “rufaa itaruhusiwa dhidi ya uamuzi uliotolewa chini ya kifungu cha 27 kwa njia ile ile kama rufaa dhidi ya hokum, na ikiwa rufaa imekatwa mahakama iliyotoa amri au ile ambako rufaa inapelekwa itasimamisha leseni huku rufaa ikisubiriwa kusikilizwa”

17. Kifungu cha 31(4) na (5) kinapendekezwa kurekebishwa ili kuondoa rejea inayofanywa na kifungu cha 29

18. Kifungu cha 32 kinarekebishwa ili kuenda a na mfuo wa kanzidata (database)

19. Kifungu cha 36(c) kinarekebishwa ili kijumuishe na kutambua leseni za nchi zote za jumuiya ya afrika mashariki

20. Kifungu cha 37 kinapendekezwa kurekebishwa ili mtu yeyote anayetaka kuwa mwalimu wa udereva awe na cheti cha ualim wa udereva (instructor’s certificate) na mtu yeyote atakayekutwa akifundisha mtu kuendesha gari bila kuwa na cheti hicho adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi 500,000.

21. Kifungu cha 39(11) na (12) inapendekezwa virekebishwe ili kumlazimisha abiria wa pikipiki kuvaa helmeti, na pia kulazimisha kila abiria afunge mkanda kukaa kiti cha mbele cha abiria na kuweka sharti la gari kuwa na vizuizi vya watoto (child restraint). Na pia kuweka adhabu kwa gari lolote kujaza mafuta kituoni huku likiwa na abiria.

22. Kifungu cha 40(1) kinarekebishwa ili kuweka sharti la kukataza dereva kuongea na simu wakati akiendesha. Adhabu inayopendkezwa kwa kosa hili kama ni kuandika message faini iwe shilingi 200,000

23. Kifungu kipya cha 41A kinapendekezwa kuongezwa ili mtu yeyote anayesababisha majeruhi au kifo kutokana na kuendesha pikipiki, guta, bajaji au basikeli awe ametenda kosana kutiwa hatiani, kama ambavyo dereva wa gari anatiwa hatiani.

24. Kifungu cha 43(1) kinapendekezwa kurekebishwa ili kuondoa neno obstruct na kulibadilisha na neno interfere

25. Inapendekezwa kuongeza kifungu cha 43(6) ili kuwabana watu wote wanaosababisha au kuzuia (hinder, obstruct or impede) magari mengine kutembea barabarani na matokeo yake kusababisha foleni, na dhabu yake inapendekezwa kuwa kati ya shilingi 50,000 na 100,000 au kifungo jela miezi 6;

26. Kifungu cha 45, inapendekezwa faini kwa makosa ya ulevi ianzie shilingi 500,000;

27. Kifungu cha 46(4) inapendkezwa mtu yeyote ambaye atakataa kupimwa ulevi ahesabike kuwa amelewa kupita kiasi;

28. Kifungu cha 49, inapendekezwa kiwango cha ulevi kishuke hadi kufikia 0.50BAC(Blooc Alcohol Concentration) kuliko kiwango cha sasa cha 0.80/100mls

29. Kifungu cha 56 inapendekezwa kuongeza adhabu kwa dereva anayeendesha kwa mwendo wa chini sana bila sababu ya msingi (unreasonably slowly) kuwa shilingi 50,000

30. Kifungu cha 57(7), inapendekezwa kuongeza kifungu kinachomtaka mmiliki wa gari lililopata ajali kumtafuta dereva wa gari hilo aliyesababisha ajali na kukimbia na kumfikisha polisi. Inapendekezwa mmiliki atakayeshindwa kufanya hivyo atozwe faini isiyopungua shilingi 500,000

31. Kifungu cha 58, inapendekezwa kuongeza kifungu kidogo cha 3 kuzuia gari za mizigo kubeba abiria

32. Kifungu cha 59 inapendekezwa kuweka adhabu kali kwa wanaopanda na kupakia mishkaki kuwa faini ya shilingi 100,000

33. Kifungu cha 61, inapendekezwa kifungu hiki kiwekewe adhabu kali kwa watu wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuharibu mali za watu hususani bodabodas, ikibidi kuwepo adhabu ya fidia.

34. Kifungu cha 62(1) inapendekezwa kifungu kirekebishwe kwa kuongeza adhabu kwa watu wasio madereva wanaopatikana wakiendesha magari bila ridhaa ya wamiliki wa gari. Hivyo adhabu isipungue shilingi 500,000 na isizidi 1,000,000

35. Kifungu cha 63(2) inapendekezwa kuongeza adhabu kwa makosa chini ya kifungu cha 40 yaani pamoja na kifungo cha miaka mitatu jela mtuhumiwa alipe faini isiyopungua shilingi 2,000,000 kwa kuendesha gari kwa njia ya hatari (dangerous driving)

36. Kifungu cha 77(1) inapendekezwa kuondoa mda wa saa 72 anaopewa dereva kuonesha leseni yake badala yake dereva apewe saa 24 tu kuonesha leseni, na ndani ya saa hizo 24 aliache gari lake kituo cha polisi hadi atakapooonesha leseni.

37. Kifungu cha 84(1) inapendekezwa kifungu kirekebishwe ili kupunguza muda anaopewa dereva aliyelitelekeza gari kuliondoa gari hilo barabarani au kwenye road reserve toka siku tatu hadi saa 24, hivyo askari aruhusiwe kuliondoa mara moja

38. Kifungu cha 85(4) inapendekezwa adhabu kwa mtu anayeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuondoa gari lililoharibika barabarani adhabu yake isipungue shilingi 100,000

39. Kifungu cha 113(1) (kosa na.23)inapendekezwa adhabu ipande kutoka 2,000 hadi 50,000 ya sasa hadi kuwa kati ya shilingi 50,000 na 100,000

ZINGATIA
Adhabu hizi ni zile zitakazokuwa zikitolewa na mahakama mtu akifikishwa mahakamani na kukutwa na hatia, na sio adhabu za papo kwa papo barabarani. Aidha haya ni mapendekzo ya awali kabisa (first draft) ambapo serikali itaendelea kukusanya maoni. Hivyo baada ya kuona mapendekezo hay ahata wewe unaruhusiwa kutoa maoni juu ya mapendekezo haya au kushauri kingine chochote unachoona chafaa kurekebishwa kwenye sheria ya usalama barabarani.

Ni vizuri mnapopost habari kutoka sehemu nyingine muwe mna-acknowledge hata kidogo kwa kutaja source. Hii habari iliandikwa na RSA(Road safety ambassadors) TANZANIA kwa kutafsiri mapendekezo hayo kutoka kiingereza kwa faida ya umma. hata hivyo tunashukuru kwa kuusambazia umma ujue kinachoendelea
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom