Rais Magufuli: Majizi yamehamia CHADEMA

Rais Magufuli: Majizi yamehamia CHADEMA

KWA HIYO, WAKATI WAPO HUKO CHAMA DOLA ALIWAFANYA NIN? AU WAKIHAMA CHAMA NDO WANAONEKANA UFISAD WAO?

HALAFU MKUU ANAFANYA KAMPENI YA UCHAGUZ UPI KWA SABABU ALISHASEMA UCHAGUZ UMEPITA TUACHE KAMPEN, SASA MBNA ANAPGA KAMPEN!
 
Chadema ni chaka salama la majizi na sasa majangili
Kweli mkuu! Sasa tungeanza pia kulishinikiza lile fisadi lililo fisidi Nyumba za serikali na kuwagawia wajomba na mahawara zake liondoke kwenye ccm yetu haraka!likaungane na wenzake huko chadema!! Lazima wajue kuwa hii ni ccm mpya! Haiwezekani tumwache mtu aliyepiga dili la kununua kivuko kilichooza kwa mabilioni ya shilingi eti aendelee kutamba ndani ya chama chetu! Ahamie huko chadema haraka! Na mwenzake aliyekiri kumiliki chombo kinachotumika kusafirishia pembe za Tembo na Faru wetu naye pia aondoke! Hatuwezi kuvumilia mtu unajulikana ni jangili halafu eti tukuache tu!!aende chadema bwana,huko ndiyo kwao,bado na mwingine mwizi kabisa eti anajiita Nyoka makengeza!! Sasa mwambieni ccm hii mpya haifugi Nyoka!! Aende chadema haraka kabla hatujamwitia migambo wamsombe! Wapo pia wale wa Escrow!!eti milioni elfu moja na mia sita ni hela ya mboga! Kha! Tumechoka! Waende chadema! Haya kuna lile jingine lenge tumbo kuuubwa,limhenga lililoleta ule msamiati wa Malofa!! Lile si ndiyo liliuza viwanda vyetu vyote? Si ndiyo lilibinafsisha hadi benki mpaka mzee wetu mchonga meno akalia machozi?hapana aisee! Tusimame pamoja! Tuhakikishe yote yamehamia chadema!na yule aliyeuza lolio---!
 
Miaka miwili anaishi naye akiwa kimya leo katoka kawa JIZI.Mbona hakumshughulikia kama alijua hivyo
Hilo ndilo tatizo mkuu,sawa na hadithi ya Sungura sizitaki mbichi hizi,kama kweli Nyarandu ni mwizi walimchukulia hatua gani?yaleyale unaunda mahakama ya mafisadi halafu inakosa watuhumiwa huku yeye kila kukicha anasema nchi inatafunwa na mafisadi hii ndio Tanzania.
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 akiwa ziarani mkoani Mwanza ambapo alikuwa akiongea na wananchi wa Mkuyuni na Butimba jijini Mwanza na kusema kuwa yeye anataka maendeleo kwa kuwa anaamini Tanzania inahitaji kujengwa na Watanzania wote na kudai ndani ya vyama vya siasa kuna wezi ambao hao ndiyo wamechelewesha maendeleo ya nchini.

“Tunataka Tanzania mpya hilo ndiyo lengo langu kwa sababu yapo yalikuwa ni majizi makubwa sana Chama Cha Mapinduzi (CCM) yakakimbilia CHADEMA ndiyo maana sijasema CUF oyeee kwa sababu wapo waliomo CUF wengine ni wabaya sana. Mimi nataka maendeleo kwa sababu maendeleo yanaletwa na Watanzania wote tushikamane ndugu zangu tutachelewa tushikamane sasa hivi tuipeleke Tanzania yetu mbele” alisisitiza Rais Magufuli

======

My Take:
Eti sasa anasema majizi yame hamia CHADEMA!!!!! Aibu kubwa hii....

Hivi Magufuli anatuchukuliaje Watanzania?

Yaani mko na mafisadi na bado mkasema mahakama ya mafisadi imekosa kesi? Aibu kubwa hii.

Nyie endelezi kasi ya chuki na dhuluma by the time mnaamka usingizini mmebak wawili.

Ahsantee kwakuwa wote wanaohamia CHADEMA ni majizii lakini wanohamia CCM si majiziiiii
 
Chadema ni kichaka kipya cha mafisadi; Siasa za nchii ni za aina yake; Iba; Kimbilia Chadema watakuficha ipasavyo, kwa jasho na damu.

Kwani wanatokea kichaka gani?!, it is a one way street? Isn’t it?

Yaani wanadamu ukungu na udumazi wa kutofikiria wanachokisema ni sawa na kujitia kidole cha macho, kila wanapovaa miwani.

How can someone throw a sense by making sense of what you are saying?! Hasara na janga kubwa kwa hili taifa!
 
Wadau tunaomba mtusaidie jibu la hilo swali kwani limekuwa linatutatiza sana wananchi.
 
Wadau tunaomba mtusaidie jibu la hilo swali kwani limekuwa linatutatiza sana wananchi.


"..Mheshimiwa Spika, aina au dalili ya serikali iliyochoka ni serikali yenye mawaziri kama hawa akina Lazaro Nyalandu hawa, ambao kazi yao leo waziri wa maliasili na utalii kazi yake ni kupiga picha na mbwa wa wazungu, kazi yake kupiga picha ameshika risasi, kazi yake kupiga picha na helikopta; kazi yake kwenda na mamiss Marekani kupiga nao picha kina Aunt Ezekiel, kazi yake kupiga picha amembeba askari kamshika makalio, kamshika bega.

Waziri, unamshika askari wanyamapori kwa staili ile? Mimi ningekuwa Rais wa nchi hii tungekuwa tunazungumza habari nyingine leo. Nasubiri hili tu, Oktoba inakuja. Nimwambie Dr. Slaa anipe uwaziri wa mambo ya ndani kwa wiki mbili tu halafu baada ya hapo aniachie, awape watu wengine tuwafundishe adabu.." kwa hisani ya Joshua Nassari.
 
Chadema ni kichaka kipya cha mafisadi; Siasa za nchii ni za aina yake; Iba; Kimbilia Chadema watakuficha ipasavyo, kwa jasho na damu.
Hv akiwa kule anakuwa sio fisadi au mpaka uhamie Chadema ndio unakuwa fisadi...???

Kama ni fisadi vp ile mahakama ya mafisadi iliyoanzishwa kwa mbwembwe imeshalithibitisha hilo...????

Mwacheni Nyalando ametumia haki yake ya kikatiba,mkianza kuongea mtaonekana mnaweweseke...!!!!
 
Mheshimiwa rais wetu kipenzi, tuliamka asubuhi kukupigia kura ili uyashughulikie hayo majizi na mafisadi kwa mujibu wa sheria za nchi..

Mbona unaendelea kutulalamikia?
 
kuwa wapo watu ambao walikuwa ni wezi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema saizi watu hao wamekimbilia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kwa sababu yoyote iliomfanya aachane na ccm pamoja na hizo za kwenu ameachana nao kwa hiari yake kumbukeni alijiunga nao kwa hiari yake na sasa kaachana nao kwa hiari yake nyie si mmebaki kelele za nini wacheni maneno kashaachana nanyi
 
Mahakama zipo na zinafanyakazi.
Kwa nini watu hao mnaowaaita wezi msiwapeleka huko kujibu tuhuma zao mnazowatuhumu.

Au mfute basi mfumo wa vyama vingi, maana kila anaehama ccm ni mwizi wakati ndilo lichama lililowaibiwa watanzania na kutufikisha hapa tulipo leo.

Mbona matahira wanalifanya taifa hili kuwa taifa la kuhubiri chuki tu?
Mmeanzisha hadi mahakama ya mafisadi uchwara na kubaki kuwa stori tu.
Hatutaki kusikia hayo, zaidi serikali ijipambanue kutekeleza shughuli za maendeleo na kutatua changamoto za watanzania. Sio mipasho na matusi majukwaani.
Wewe ni nafasi yako sasa kubadilisha unachokiamini na sio muda wote kuumaliza kwa kulalama na kulaumu tu.

Ninachokiamini ni kwamba Nchi hii imepata uhuru toka mwaka 1961 na sio leo. Hivyo tusichafuliane taswira eti kisa ukubalike, kubaliana na matindiga hao hao, big shame on you.........
 
Back
Top Bottom